Dk. Tizeba, utaweza kufanya kazi na Magufuli aliyekufukuza pale Mwanza City Council!?

theophilius

Senior Member
Nov 19, 2010
150
54
Kwa wanaokumbuka kisa cha kuvunjwa kwa kituo cha mafuta huko Mwanza, katika eneo lililodaiwa kuwa la hifadhi ya barabara, hawatakuwa wamesahau kwamba Dk Tizeba alikuwa miongoni mwa wakuu wa idara waliofukuzwa kwa amri ya Magufuli kwa madai ya uzembe wa kuruhusu kitua hicho kujengwa barabarani

Sasa ni uso na pua, sijui wataangalianaje kwenye vikao vitakavyowakutanisha! au ndiyo kusema kwamba anayosimamia Magufuli aanayasimamia yeye peke yake ndani ya serikali ya Kikwete ndyo maana haya yanatokea! au Mhe Rais umesahau mara hii?

Tuombe Mugu, ndugu yetu Eng. Dk Tizeba iwe alisingiziwa, na hata kama hakusingiziwa, hilo la kufukuzwa na Magufuli kwa tuhuma za kuhogwa na mhindi wa kituo cha mafuta, liwe lilikuwa funzo kwake na hivyo kuamua kufanya kazi kwa uadilifu, katika unaibu waziri wa uchukuzi ambapo tunaambiwa watangulizi wake, walilambishwa asali
 
Theo,

..mahakama ilimkuta Magufuli na makosa kwa kuvunja kituo cha mafuta mwanza.

..serikali iliamriwa na mahakama imlipe mmiliki wa kituo cha mafuta kiasi cha sh bilion 14 hivi.

kumbe! ndiyo maana rafiki yangu Manssor baada ya hapo mambo yalimnyookea hadi ubunge na sasa mwenyekiti wa tenda bodi ya kuagiza mafuta kwa pamoja... Tanzania ni zaidi ya unavyoijua
 
hata Mh. Lema alikutwa na hatia na mahakama na kuvuliwa ubunge wa Arusha mjini Makongoro Mahanga hakuwa na hatia pamoja na ushahidi uliokuwepo.

Go figure . . .

Theo,

..mahakama ilimkuta Magufuli na makosa kwa kuvunja kituo cha mafuta mwanza.

..serikali iliamriwa na mahakama imlipe mmiliki wa kituo cha mafuta kiasi cha sh bilion 14 hivi.
 
Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,
Au ulimaanisha kufanya nae kazi katika baraza as a whole?
 
kumbe! ndiyo maana rafiki yangu Manssor baada ya hapo mambo yalimnyookea hadi ubunge na sasa mwenyekiti wa tenda bodi ya kuagiza mafuta kwa pamoja... Tanzania ni zaidi ya unavyoijua

Theo,

..pamoja na kuvunja sheria, mahakama ilieleza kwamba Magufuli pia alidharau ushauri wa wataalamu na wanasheria na kuendelea na ubabe/uhuni wake kuvunja kituo cha mafuta.

..nadhani hukumu hiyo ndiyo iliyosababisha JK amteua Mwakyembe[mtaalamu wa sheria] kuwa naibu wa Magufuli pale wizara ya ujenzi.

..nakumbuka jaji Mwesiumo naye aliteuliwa kuwa Naibu waziri mambo ya ndani kumsaidia Mrema aliyekuwa hafuati taratibu wala sheria sawa na Dr.Magufuli.
 
Manaibu mawaziri hawaingi kwenye vikao vya Cabinet, hivyo kamwe magufuli hawezi fanya kazi na fisadi Tizeba!
 
Huyu jamaa alionyesha uwezo mdogo sana wa kiongozi na utawala alipokuwa pale Sikonge kama mkuu wa Wilaya!! achilia madudu aliyofanya akiwa Mhandisi pale MZA,nashangaa kwa uwezo wake huo mdogo leo amekuwa Naibu waziri... au tuamini yale maneno yake kuwa jamaa ni mshikaji wake kauli ambayo alikuwa anaitoa mara kwa mara akiwa DC?
KWELI TZ NI ZAIDI YA UIJUAVYO!!
 
Tulokuwa Mwanza enzi hizo tunajua kuwa huyu Tizeba ni corrupt na alilambishwa kitu kikubwa na Mansoor ili apewe hati ya eneo hilo la mtaa wa misheni. Iliamriwa na mahakama Mansoor alipwe kwa kuwa tayari Mansoor alishapewa hati ya hilo eneo. Tena huyu huyu Mansoor mhindi na watu wa City walimpatia eneo lilokuwa limejengwa soko kwa ajili ya watu wa Ilemela, Pansiasi, iloganzala, kiseke na Lumala kujenga kituo cha mafuta. CCM kumejaa maizi tupu.
 
Muda muda mwingi wa kuongea uongo uongo kuliko vitu vya msingi! Tizeba aliyekumbwa na hiyo kashfa siyo huyu naibu waziri,ni mdogo mtu ambaye kwa sasa ni diwan huko kwao buchosa,sengerema.punguzeni udaku basi,tutawachoka.
 
pitia upya orodha ya mawaziri na manaibu waziri wote waliotajwa jana,huyo Dr tizeba mbona sio naibu waziri wa magufuli ?yeye ni na NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI NA WAZIRI WAKE NI DR HARRISON MWAKYEMBE!
 
Muda muda mwingi wa kuongea uongo uongo kuliko vitu vya msingi! Tizeba aliyekumbwa na hiyo kashfa siyo huyu naibu waziri,ni mdogo mtu ambaye kwa sasa ni diwan huko kwao buchosa,sengerema.punguzeni udaku basi,tutawachoka.

Mkuu, Unamaanisha yule diwani wa Buchosa aliyevua gamba aliyetambulishwa na Dr Slaa Viwanja vya Sahara jijini Mwanza?
 
Muda muda mwingi wa kuongea uongo uongo kuliko vitu vya msingi! Tizeba aliyekumbwa na hiyo kashfa siyo huyu naibu waziri,ni mdogo mtu ambaye kwa sasa ni diwan huko kwao buchosa,sengerema.punguzeni udaku basi,tutawachoka.

Wewe ni wa kuhurumiwa sana kwani hata hujielewi sembuse kuelewa kinachotokea kwa wengine?
Endelea kuchapa usingizui tu siku ukiamka utauliza majirani watakusaidia.
 
Theo,

..mahakama ilimkuta Magufuli na makosa kwa kuvunja kituo cha mafuta mwanza.

..serikali iliamriwa na mahakama imlipe mmiliki wa kituo cha mafuta kiasi cha sh bilion 14 hivi.

Makosa ya Magufuli kisheria yalitokana na kuwa mmiliki wa kituo alikuwa amepewa kiwanja kile kihalali na mamlaka husika ya halmashauri ya jiji la Mwanza; ambapo mamlaka hiyo ilihusisha akina Tizeba na wenzake. Kwa hiyo kisheria kosa halikuwa la mmiliki wa kituo bali lilikuwa la serikali iliyompa kiwanja kile, na ndiyo maana alikuwa na haki ya kufidiwa hasara ile.

Makosa yalikuwa siyo kwa Magufuli kuvunja ujenzi ule bali yalikuwa ni kwa Halmashauri ya jiji kumruhusu mfanya biashara yule ajenge pale. Mhandisi Tizeba aliamua ile ya Makongoro ipindishwe kwa makusudi ili kuacha nafasi ya kutosha kwenye kituo kile.

Muda muda mwingi wa kuongea uongo uongo kuliko vitu vya msingi! Tizeba aliyekumbwa na hiyo kashfa siyo huyu naibu waziri,ni mdogo mtu ambaye kwa sasa ni diwan huko kwao buchosa,sengerema.punguzeni udaku basi,tutawachoka.

Hapana, alikuwa huyu waziri; wakati huo alikuwa mhandisi wa jiji la Mwanza.
 
JK ni mtu wa ajabu sana............. siamini kwamba hayo yote alikua hayajui

Anyway, labda watafanya kazi pamoja vizuri
 
  • Thanks
Reactions: kai
Tunahitaji katiba mpya ambayo itatuhakishia mahakama iliyo huru na isiyohongeka. Right now we are very far from there.
 
kumbe! ndiyo maana rafiki yangu Manssor baada ya hapo mambo yalimnyookea hadi ubunge na sasa mwenyekiti wa tenda bodi ya kuagiza mafuta kwa pamoja... Tanzania ni zaidi ya unavyoijua

Mansour mashallah...naona Ngereja alikuwa upande wake. Muda mfupi tayari alimeshaandikiana barua kali kali na makampuni ya mafuta yanayounda hiyo PIC. JK amebadili formation nzima ya mashambulizi bila kutegemea,lol!
 
Wewe ni wa kuhurumiwa sana kwani hata hujielewi sembuse kuelewa kinachotokea kwa wengine?
Endelea kuchapa usingizui tu siku ukiamka utauliza majirani watakusaidia.

Mkuu nahisi hii ni ID nyingine ya Kigwangala!!

Cant you figure it out, check the clue!
 
Back
Top Bottom