Ajali ya ndege Bukoba ni matokeo ya uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.Tuwajibishane ili tusirudie makosa

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Yamesikika mengi kuhusiana na ajali ya ndege ya PW kule Bukoba, yamesemwa mengi na wanasiasa na wasio wanasiasa. Kila mtu anasema la kwake, lakini moja na lenye uhakika ni kuwa, kuna watu wanapaswa kuwajibishwa kwa ajali ya ndege Bukoba.

Tumepoteza ndugu, marafiki na jamaa zetu kwa sababu ya uzembe na mazoea (bussiness as usual). Tuliowapa dhamana ya kusimamia viwanja vyetu vya ndege, tunawatengea bajeti kila mwaka katika kitengo cha majanga na uokozi na wale tunaowategemea katika ulinzi na usalama wa nchi,wanapaswa kuwajibika.

Tuwapuuze wanasiasa aina ya wale wa zambarau ambao wanaingiza siasa na kubeza juhudi za wavuvi katika uokozi. Ni mtu asiye na shukrani ndio atashindwa kutambua nafasi ya kijana Majaliwa katika kuwanusuru wale wote walionusurika. Ni ajabu pia hata wale walionusirika kuikosa pumzi ya dunia hii, wanaingia katika mkumbo wa kuona "walijiokoa" kwa juhudi zao, na sio msaada wa wavuvi aina ya Majaliwa.

Ingetokea Majaliwa amekufa, tusingekuwa na shukrani... kuumia kwake na kuzimia kwake katika harakati za kufanya uokozi, ni jambo kubwa kuliko hata kuanza kumshambulia kwa kuingiza siasa za kijinga. Ni ajabu sana kukuta kuna wanasiasa wanapitia katika "kick" ya kutoona ushiriki wa Majaliwa katika uokozi.

Uwanja wa ndege Bukoba, ni moja kati ya viwanja vya Tanzania vilivyo katika Code 3C inayotambuliwa na ICAO (International Civil Aviation Organization). Code 3C ni kiwanja chenye uwezo wa kuchukua ndege size ya kadi kama vile Dash8-Q400 na ATR42 na hata ATR72 ni kiwanja kinachofanya kazi kwa mawio na machweo kwa siku 7 za week.

Hivyo tukio linalotokea saa 08:45 asubuhi ni tukio ambalo linapaswa kukuta watu wapo ofisini katika maandalizi ya kuona lolote linaweza" kutokea.

Kwa kadili ya dodoso za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, kikosi cha Zimamoto kilichopo Bukoba kinadondokea katika Category 5, na Category inayotaka RFFS (Rescue and Fire Fighting Services) iwe na gari lenye uwezo wa kubeba lita za ujazo 5800(?), na kama kiwanja kipo kando ya ziwa au mto basi wafanyakazi wa uokozi wawe na mafunzo ya uogeleaji na respiratory equipments za kutosha. Na uwanja unapaswa kuwa na nguvu kazi isiyopungua wafanyakazi 25.

Zaidi ya hapo, inatakiwa wakati wa kutua na kupaa kwa ndege, gari la zimamoto linatakiwa kufanya huduma ya "standby" kwa kutumia taxway na wakati wa kuruka gari la zimamoto linatakiwa kufanya "escort".

Hili ni swali la kujiuliza, Je uwanja wa Bukoba lina gari la zimamoto lenye uwezo wa kubeba maji lita ngapi? kuna wafanyakazi wangapi katika kituo cha Zimamoto uwanja wa ndege? na je askari wa uokozi waliopo wana mafunzo ya uogeleaji endapo ndege imetokea kudondoka katika maji? Au wote wanasubiri watokee akina "Majaliwa" kuokoa? Ni ajabu sana kuona hata wanasiasa aina ya yule wa Zambarau anataka kuifanya ajenda ya Majaliwa kuwa kubwa na ya kupigia siasa badala ya kushukuru kazi na jitihada za kijana yule.

Tunapoona kuwa ndege ilishindwa kutua kwa zaidi ya mara moja, Je kitengo cha Zimamoto na uokoaji kilijiandaaje? Kulikuwa na gari eneo la Airside likiwa "standby" kufanya uokozi?

Annex 14 ya ICAO inanukuliwa ikisema “ The principal objective of a rescue and fire fighting service is to save lives”. Airports need a RFFS/ARFF even during “periods of reduced activity, irrespective of the number of movements” because accidents happen… when they happen


Meneja wa Uwanja na kamanda wa Zimamoto/Msimamizi wa kamandi ya Jeshi la Zimamoto uwanja wa Bukoba wanatakiwa wajibu hitaji hili la kiviwango.

Kama ulivyo uwanja wa Lindi unaotegemea Control Tower kutoka Mtwara au uwanja wa Nachingwea nyumbani kwa Waziri Mkuu unavyotegemea Control tower kutoka Mtwara mjini, ndivyo ilivyo kwa Bukoba na Mpanda.

Kwa miaka mingi marubani wengi katika uwanja wa Bukoba wamekuwa wakishuka kwa kutumia "uzoefu", na uzoefu unakuwa na umuhimu sana katika nyakati zenye hali mbaya ya hewa. Unapokuwa na kiwanja chenye "scheduled Flights" na huazingatii kufuata viwango vya kuwa na mnara wa kuongoza ndege, ajali ya aina hii ikitokea, mwanasiasa mwenye uweledi, hapambani na Majaliwa, anatakiwa kupambana na wale wenye bajeti na dhamana ya kukamilisha hayo yanayotakiwa.

Mjadala kuwa "nani alifungua mlango au nani hakufungua" ni mjadala wa aibu sana. Majaliwa angeweza kupoteza uhai ama kwa kuzama wakati akiwaokoa abiria au kwa kuumia. Kwa wanaoujua "scene" ya eneo la ajali, maelezo ya Majaliwa yamenyooka kabisa. Panapokuwa na ajali ya ndege, kama ambavyo emergency drill hufanyika, lazima kuwepo na "On Scene Commander" au "Incident Commander". Huyu anakuwa na kipaza sauti na hutoa muongozo wa nini kufanyike. Kwa hiyo Majaliwa anaposema kuna "mtu alikuwa ana kipaza sauti" alinikataza nisivunje kioo kumtoa rubani, basi huyu ni "Incident Commander".

Mtiririko huu wa maongezi unaonyesha jinsi bwana mdogo huyu alivyojitoa kuokoa maisha ya watu. Rubani alikufa sababu Bukoba hakuna control Tower, alikosa mawasiliano ya moja kwa moja ya nini afanye na msaada gani apate. Mawasiliano ya Walkie Talkie Radio ambayo hutumika tu na wafanyakazi wa Precision Bukoba tena wasio na uzoefu wa kazi hiyo yasingetosha kuweka uimara wa taarifa kati ya rubani na walio nje. Ni uzembe mkubwa sana kupoteza watu waliopata ajali mita 500 toka kwenye threshold, mita 500 ni vacinity ya aerodrome. NI AIBU SANA.

Mlango wa ATR42 unafungukia kwa nje, anayefungua anapaswa kuwa ndani, lakini ni lazima apate msaada wa mtu wa nje. Sababu unapoufungua mlango wa ATR42 hutumika kama mlango na ndio ngazi pia ya kuingia na kutoka katika ndege. Hivyo unapofunguliwa mtu wa nje ni lazima auishike, aweke stabilize stick itakayofanya mlango usijifunge.

Hii ni hata katika nchi kavu ndege inapokuwa uwanjani. NI LAZIMA MTU WA NJE AUSHIKE NA KUWEKE STABILIZE STICK... hata kama walifungua abiria na muhudumu, kwa nature ya mlango-ngazi wa ATR42 isingewezekana kufunguka kama hakuna mtu nje, tena katika maji. Hapa ndio Majaliwa anaposema alitumia kasia kuufungua, ili watu watoke. Hata katika hili kuna watu wanataka mashindano na Majaliwa.

Ni mambo ya aibu sana... tushukuru sana akina Majaliwa na wavuvi wengine, kama ndege hii ingedondoka mita 1500 kutoka uwanjani, hata hao waliodhani ni abiria tu na mhudumu wa ndege ndio walifungua mlango na kutokea wangekuwa wanaongea mengine. Tuwaache hawa akina Majaliwa, tuwashukuru na tafadhali tusiwaingize katika mjadala unaoelekea kuwa na aina ya kutokushukuru msaada wao. Watu waliojitolea tu kwanini wasimangwe? hao wenye mafunzo, hao wenye kitengo cha dharula na majanga na wanaotengewa bajeti walifika masaa 6 baada ya ajali wakiwa na boti iliyo na mafuta kidogo na hawakuwa na mitungi.

Ni bahati mbaya kuwa jambo hili limebebwa kisiasa, ili kufunika udhaifu wa wanasiasa. Ajali ya mita 500, tena ndani ya maji katika kiwanja ambacho ndege ni "!scheduled Flight" ni aibu sana kumpoteza rubani na abiria.Kama tungekuwa na control tower, jeshi imara la zimamoto na uokozi maanake wakati ndege ikifanya orbiting(kuzunguka angani kutafuta uwezekano wa kutua) maanake team nzima ya kiwanja, ambayo miezi kadhaa nyuma ilishatumia zaidi ya milioni 20 kuandaa igizo la uokoaji(emergency drill) tena kwa kuhusisha hadi watu wa makao makuu waliokula posho na marupurupu na kuitangazia dunia kuwa wapo tayari kukabiliana na ajali muda wowote. Ni ajabu sana kama hizi roho za watu zilizopotea hazitaondoka na watu... Yaani kwanza katika dhana ya uwajibikaji, mpaka sasa kuna watu walitakiwa kuwa wameshawajibishwa.

USHAURI:
i)Serikali ifanye hima kwa kushirikiana na Tanzania Civil Aviation Authority ambao ndio wamepewa dhamana ya kusimamia usafiri wa anga kuweka control tower katika uwanja wa Bukoba ambao unapokea ndege ambazo ni "scheduled Flights". Ni aibu sana kukosa huduma hii.

ii)Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika viwanja vya ndege liboreshwe. Na ikiwezekana ili kufuata Standard za ICAO kwa uzuri, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege iachiwe kitengo hiki kwa 100% ili iweze kuwasimamia na pengine kuwawajibisha wafanyakazi wa kitengo hiki kwa asilimia zote. Kama ilivyo Mamlaka ya Bandari au Zimamoto KIA. Zimamoto za Viwanja vilivyo chini ya TAA ni waajiliwa wa Wizara ya mambo ya ndani, na sio TAA kwa hiyo mamlaka ya kinidhamu inakuwa Wizara ya Mambo ya ndani, kumekuwa na ugumu wa kuwawajibisha hata kama mtu anakuja kazini saa 4 badala ya saa 07:30 kwa sababu Meneja wa kiwanja sio mamlaka yake ya nidhamu. Hili liangaliwe kwa mapana. Kuna udhaifu mkubwa sana katika Kitengo cha Zimamoto na uokoaji katika viwanja vya ndege.

iii) Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tz(TAA) ifanye kwa mkazo zoezi la emergency drill kwa umakini na sio mazoea. Ni aibu kuwa Bukoba ndani ya miezi 10 ilifanya emergency drill lkn ajali imetokea na imeonyesha kuwa kiwanja hakikuwa tayari kabisa katika kukabiliana na majanga. Watu wanafanya kazi kwa mazoea, na hii imedhirika baada ya ajali hii kutokea.Ukiangalia records za mtoa taarifa kutoka katika ofisi ya operations kwenda kwa wadau wengine na ule mtiririko wa mawasiliano, inaonyesha TAA bado ina staffs ambao wanafanya kazi kama wapo sokoni tu. Training ziongezwe ili kuwajengea uwezo wafanyakazi.

iv)Serikali ione umuhimu wa kuweka control towers katika viwanja ambavyo ndege hutua mara kwa mara.

v)Serikali ihakikishe inaboresha vituo vya zimamoto katika viwanja vya ndege, magari ya kisasa na askari walio na mafunzo. Vifaa vya zimamoto kama vile foam na horse za kutosha. Na kwenye maeneo ya mwambao mwa maji, wakati wa kutua na kuruka kwa ndege kuwepo na ushirikiano wa kutosha na askari wa majini kuwa na utayari wa uokozi mara tu ajali inapotokea. Hii ni kwa aina ya viwanja kama Bukoba na Mwanza.

Ikumbukwe kuwa ndege kuahirisha kutua au kuruka sababu ya hali ya hewa mbaya, hakuna uhusiano na ubovu wa kiwanja. Sehemu nyingi duniani kwenye viwanja vilivyo bora,bado ndege hushindwa kutua. Ni ajabu kuona mwanasiasa aina ya Lugangila kuhusisha hali ya hewa na ubovu wa kiwanja.

Pole kwa manusura, na pole kwa wafiwa na Mungu awapokee wote waliopoteza maisha yao mita 500 kutoka uwanjani.
 
Sitashangaa kama hao wafanyakazi wa Zimamoto waliopo uwanja wa ndege wa Bukoba wakiwa hawana mafunzo ya uogeleaji, nahisi mindset zao zitakuwa zinasubiri moto tu, labda hili tukio la hiyo ajali ndio liwaamshe, ahsante pia kwa darasa.

Ajabu zaidi nimeona taarifa ya Msigwa twitter akisema serikali itatoa ripoti/maelezo yake, ni kama vile Msigwa anajaribu kuzima kile kilichoandikwa na kuripotiwa kwenye ripoti iliyopo sasa. Nashindwa kuelewa nini hasa malengo ya Msigwa, nahisi watakuwa wanataka kuingiza jina la muokozi Majaliwa ambalo kwenye ripoti ya kwanza halipo.

Kwa mwendo huu sijui mwisho wa siku tumuamini nani, Msigwa amegeuzwa kuwa "propagandist" wa serikali, anayegeuza uongo kuwa ukweli, au ukweli kuwa uongo, ili kuendana na mapenzi ya mabosi wake kwa jambo na wakati husika, kwa namna hii ataifanya kazi yake pamoja na yeye mwenyewe kudharaulika.

Zaidi, kitendo cha kuwa na ripoti mbili tofauti kuhusu tukio moja ni cha ajabu na kushangaza, kinaonesha vile watanzania hatupo serious kwenye kufanya mambo yetu, na jinsi tulivyo tayari kuingilia kazi za kitaalamu tusizokuwa na ujuzi nazo kwa maslahi tofauti.
 
Karibu Jamvini Ndugu yetu Barafu..

Nakubaliana na wewe, Majaliwa ashukuriwe kwa ujasiri na kujitoa kwake.

Mengine yote ni yaleyale katika nchi yetu tunayolalamikia kila siku Uzembe na upumbavu na kuchekeana chekeana.

Miezi kadhaa nyuma watu wamekula perdiem wamefanya "emmergency drill" lakini watu hao hao wameshindwa kuokoa watu kwenye real scene, aibu sana
 
Mengine yoote umeyaainisha kitalaam kwa uzoefu na ukongwe wako kwenye Aviation industry, wahusika wanapaswa kujitathmini na Wenye mamlaka wanapaswa kuwajibisha wazembe na hata kuwafungulia mashitaka ya kusababisha vifo kizembe wakiwa na dhamana ya kufanya uokozi.

Kama ulivyosema, all important aspect for safety katika uwanja huo ni mashaka mashaka tu na watu kila siku wako maofisini kuanzia Mawaziri mpaka wakurugenzi na hata baada ya kupotea roho za watu bado wanaleta blah blah tu..
 
Yamesikika mengi kuhusiana na ajali ya ndege ya PW kule Bukoba,yamesemwa mengi na wanasiasa na wasio wanasiasa.Kila mtu anasema la kwake...

Zitto Kabwe .. Erythrocyte

Mko wapi mlambwe za Uso hizi.
Maana kwa Uchwara wenu!

Mnaishi Siasa kwa kutumia Matukio badala ya "Hoja" na "Sera!"

Mnaishi Siasa kwa kutafuta Wachawi badala ya Ufumbuzi!

Mnaishi Siasa kwa kutafuta Riziki zenu binafsi badala ya Wapiga kura wanaovifanya vyama vyenu viendelee kuwepo!

Mnaishi Siasa kwa kuangalia "Political Mileage",badala ya "Political Influences!"

Huyu Member barafu amekuja wakati muafaka na sahihi kabisa!

barafu amekuja kuondoa mzizi wa Fitina kwenu team Sumu!

Hatujui kama yoote hii,ilikuwa dhidi ya Majaliwa mkubwa au Majaliwa mdogo?

Hongera sana barafu Mtanzania mwenye uwezo wa kujenga hoja yenye Mashiko na wenye kuelewa Tumekuelewa!

Wasiokuelewa ni wale tu waliolewa Majungu!
 
Barafu, ni nani mwenye mamlaka ya kukagua na kupitisha matumizi ya kiwanja cha ndege kwa level ya uwanja wa Bukoba.

naamini lazima kuna chombo kinapaswa kujiridhisha kiwanja kinakidhi vigezo ndio kitoe idhini labda na certificate.
Je hizo kaguzi zinafanywa kila muda gani na taasisi gani?
 
uzi mzuri ila kujifunza it's no kwa uzuzu wa watanzania, tungejifunza baada ya ajali ya MV BUKOBA, ziwa lile halina kabisa life saver boats, wala hakuna kikosi maji cha police, PM alitakiwa ajiuzuru as soon as possible, but maisha yataendelea na mazuzu watasahau issue hii kama ile ajali ya Mh.Mbunge wa Ludewa (rip)
 
uzi mzuri ila kujifunza it's no kwa uzuzu wa watanzania, tungejifunza baada ya ajali ya MV BUKOBA, ziwa lile halina kabisa life saver boats, wala hakuna kikosi maji cha police, PM alitakiwa ajiuzuru as soon as possible, but maisha yataendelea na mazuzu watasahau issue hii kama ile ajali ya Mh.Mbunge wa Ludewa (rip)
Bora useme Serikali na Bunge lake kujiuzuru,badala ya kutafuta kujiuzuru kwa waziri mkuu!

Ilhali ukijua wazi kwamba Mtunga sera Ni serikali na mleta Bajeti ni wizara ya fedha na wapitisha bajeti ni Wabunge wa CCM!

Majaliwa Mungu aendelee kumjaalia!
 
Tanzania Civil Aviation Authority(TCAA) ndio regulator wa ubora wa viwanja vya ndege Tanzania,wakati Tanzania Airports Authority(TAA) ndio operators wa Viwanja vya ndege Tanzania isipokuwa vya Zanzibar na KIA ambacho kipo mbioni kurudishwa TAA
Barafu, ni nani mwenye mamlaka ya kukagua na kupitisha matumizi ya kiwanja cha ndege kwa level ya uwanja wa Bukoba.

naamini lazima kuna chombo kinapaswa kujiridhisha kiwanja kinakidhi vigezo ndio kitoe idhini labda na certificate.
Je hizo kaguzi zinafanywa kila muda gani na taasisi gani?
 
Yamesikika mengi kuhusiana na ajali ya ndege ya PW kule Bukoba,yamesemwa mengi na wanasiasa na wasio wanasiasa.Kila mtu anasema la kwake..
Barafu umerudi?? Nimekutafuta muda mrefu sana Kaka.

Hii post yako nitaisoma kesho nikiwa nimetulia.

Sijasoma ripoti wala taarifa yoyote ya Ajali ya ndege ile. Naamini kwa uandishi wako nitapata points na nitaisoma kwa makini sana.

Siku njema
 
Tanzania Civil Aviation Authority(TCAA) ndio regulator wa ubora wa viwanja vya ndege Tanzania,wakati Tanzania Airports Authority(TAA) ndio operators wa Viwanja vya ndege Tanzania isipokuwa vya Zanzibar na KIA ambacho kipo mbioni kurudishwa TAA

Kama ni hivyo TCAA kuna uzembe na haifai kuaminiwa maana kwa maelezo uliyotoa ya kitalaam huo uwanja haukupaswa kuwa in operation maana haukidhi viwango.

TAA nayo kama operator inapaswa kuadhibiwa na kuwekewa jicho kali kuhakikisha wanakuwa makini na day to day operation za viwanja vya ndege.

Kwa mustakabali huu huko kwingine ni Mungu tu anasaidia maana inaonekana kabisa ujinga ni huo huo kama wa Bukoba.
 
Yote umenena vyema kabisa, ila la shujaa Majaliwa na lilivyokuzwa big NO.
Kukuzwa ni siasa,ila kwa aliyoyatenda ni ushujaa.Sasa inategemea unaweza kuona lipi linazidi uzito kwa jingine.Kwangu mimi la kukuzwa sababu ya siasa nimelipuuzia,nimeamua kuchukua la ujasiri wake wa kusaidia watu na kujitolea mpaka akapata akafikwa na majanga yaliyomfanya awe hospitali.Nimechagua upande wake mzuri..
 
Back
Top Bottom