Mwanza: Watu 6 wafariki kwa kugongwa na gari wakifanya mazoezi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Watu 6 wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari binafsi, ambalo limewagonga wananchi waliokuwa wakifanya mazoezi kandokando ya barabara eneo la Sabasaba Ilemela Mwanza leo Julai 22, 2023 majira ya asubuhi.

picha-ajali.jpg

=====
Taarifa za awali ni kwamba Watu 6 wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari binafsi, ambalo limewagonga wananchi waliokuwa wakifanya mazoezi kandokando ya barabara eneo la Sabasaba Ilemela, Jijini Mwanza.

Chanzo cha ajali ni mwendokasi na Dereva kutozungatia Sheria na alama za barabarani.

Miili ya Waliofariki na Majeruhi wa ajali wamepelewa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure.

============

UPDATES...
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya “Imetokea katika Wilaya ya Ilemela, gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T476 DZL ikitoka Sabasaba kuelekea Buswelu ilipoteza mwelekeo kutokana na mwendokasi na kusababisha ajali iliyoua watu 6, kujeruhi 14 waliokuwa wakifanya mazoezi ya kukimbia ambapo jumla yao walikuwa 27.

"Majeruhi wanne wapo Hospitali ya Bugando, wengine 10 wapo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou Toure.

“Juhudi za kumtafuta Dereva zinaendelea kwa kuwa alikimbia mara baada ya tukio hilo.”

UPDATES
======

Mwanza. Watu sita wamefariki papo hapo na wengine 16 wakijeruhiwa baada ya kugongwa na gari aina ya Hilux double cabin eneo la Shule ya Msingi Lumala Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Gideon Msuya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo asubuhi ya leo Julai 22, 2023 wakati kikundi cha vijana kilichotambulika kwa jina la Adden hotel kikiwa kinafanya mazoezi ya kukimbia katika barabara ya sabasaba kuelekea Kiseke wilayani humo.

Msuya amesema msako wa dereva wa gari hiyo unaendelea baada ya kulitelekeza kwenye kituo cha mafuta kisha yeye kutokomea kusikojulika.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekouture, Dk Bahati Msaki amesema wamepokea miili ya watu watano huku mmoja akifariki akipatiwa matibabu hospitalini hapo na majeruhi 8 wanaendelea na matibabu huku 8 wakipatiwa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa uangalizi maalum.

“Vijana hao walikuwa wanafanya mazoezi ya mwendo wa pole wakiwa na kundi lao Linalotambulika kwa jina la Adden hotel,”amesema Dk Msaki

Dk Msaki amesema miili ya marehemu ipo katika Hospitali ya Mkoa Sekou Toure huku taratibu za kuikabidhi kwa ndugu zinaendelea kuratibiwa na hospital ya Sekou Toure na Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza.

“Nitoe pole kwa familia waliopoteza wapendwa wao na tuendelee kuwaweka kwenye maombi majeruhi wote wapate uponyaji wa haraka na waruhusiwe warudi nyumbani kuendelea na majukukumu yao,”amesema Dk Masala
IMG_8742.JPG
IMG_8743.JPG
 
Nina ndugu yangu anafanya mazoezi na rafiki zake nilimshaurigi zaidi ya mara mbili asiwe anakimbia (jogging) kwenye barabara au makazi ya watu angalau upate kiwanja mbona unafanya vizuri tu.

Sababu ya kumshauri kulishatokea tukio maeneo ya G5 mtu alikua anafanya tizi la mbio jioni katoka ufukweni zikapigwa kelele za mwizi mwamba hakupona.
Pili barabarani ndio kama hivyo mtu anaweza poteza uthibiti wa gari na mambo yakawa mengine.

Tujijali kila muda yuthamini kidogo haya maisha tuliopewa.
 
Huyo dereva ukute ni gaidi ameamua kuua watu Makusudi, kama hajafa akamatwe, ashitakiwe naye ahukumiwe kifo
Ajali zinatokea kila siku
Wenye mabasi kila kukicha wanaua na hakuna anaehukumiwa kifo

Sehemu za mazoezi zitengwe na sio barabarani
Sehemu za wazi zote zimeuzwa na washenzi wenye tamaa
Mpaka viwanja vya shule vimeuzwa

Zamani mpaka makahama zilikuwa na maeneno makubwa sana mpaka mpira tulikuwa tunacheza jioni

Police walikuwa na maeneo makubwa
Ila kila mahali wameuza watu wenye tamaa
Hao ndio wa kunyongwa sasa
 
Dah,ila kufanyia mazoezi barabarani ni hatari sana wakati mwingine,nadhani serikali itoe melekezo kwa madereva na wafanya mazoezi,maana hiui sasa imeshakuwa tabu...
Hilo ndio la msingi ukweli hatuna miundombinu itakayo tubeba wote magari, bajaji, pikipiki, baiskeli, watembea kwa miguu na wafanya mazoezi serikali ingeweka katazo marufuku kufanya mazoezi ya aina yoyote barabarani au kando ya barabara kwa umbali fulani ambao hata likatokea la kutokea mtu anaweza kujiokoa nafasi yake
 
Watu wanaangalia walipoangukia na sio walipojikwaa!! Siku zote barabara ni sheria na taratibu, Sasa barabara ni uwanja WA mazoezi!? Yote Hii ni mazoea kupita kiasi, fikiria unaendesha Gari at 60 kph ghafla Gari ya mbele Yako inakubana na kushoto kwako watu wanafanya mazoezi bila tahadhari ya matumizi ya barabara, Sasa wapi itakuwa salama Yako wewe dereva!? Kwenye designs za barabara Kuna kitu inaitwa recovery zone, dereva unaweza kukimbilia sasa ndio ukute wamejazana Wana mazoezi hii ni hatarishi!! Kwa hili bila kumumunya lawama zote ziende Kwa mamlaka Kwa kutozingatia usanifu Bora WA barabara, very poor designs!! Mtu anajenga barabara anatenganisha waenda Kwa miguu na mstari WA njano, like seriously!! Dhahama lote hili walibebe Watu WA manispaa Kwa usanifu WA hovyo, pia sheria ipige marufuku mazoezi barabarani bila uangalizi WA Polisi
 
Hilo ndio la msingi ukweli hatuna miundombinu itakayo tubeba wote magari, bajaji, pikipiki, baiskeli, watembea kwa miguu na wafanya mazoezi serikali ingeweka katazo marufuku kufanya mazoezi ya aina yoyote barabarani au kando ya barabara kwa umbali fulani ambao hata likatokea la kutokea mtu anaweza kujiokoa nafasi yake
Halafu unakuta msululu wa watu kwa kuigana kila mmoja anakimbia tu
Wapige marufuku tu
Mwenye akili timamu hawezi kufanya mazoezi barabarani
 
Halafu unakuta msululu wa watu kwa kuigana kila mmoja anakimbia tu
Wapige marufuku tu
Mwenye akili timamu hawezi kufanya mazoezi barabarani
Kweli kabisa kuiga kunatuponza sana. Tukiona wazungu kwao wanakimbia barabarani na sisi tunajimwaga kumbe wenzetu muda huo miundombinu ipo vizuri wamevaa viakisi mwanga na wana vifaa vya kulinda viungo. Na hata uendeshaji wao unazingatia mambo mengi ajali ni vitu wasivyosikia mara kwa mara japo ajali haina kinga
 
Kweli kabisa kuiga kunatuponza sana. Tukiona wazungu kwao wanakimbia barabarani na sisi tunajimwaga kumbe wenzetu muda huo miundombinu ipo vizuri wamevaa viakisi mwanga na wana vifaa vya kulinda viungo. Na hata uendeshaji wao unazingatia mambo mengi ajali ni vitu wasivyosikia mara kwa mara japo ajali haina kinga
Ajali za ulaya ni nadra sana na barabara zote siku hizi wanaweka njia za baiskeli na wanapewa heshima sana

Uendeshaji wa ulaya ni wa sheria ngumu sana na makosa madogo unapigwa faini na kukatwa point kwenye license ambapo na insurance yako inapanda zaidi kwa kutokuwa muangalifu

Kwa hiyo unakuwa na heshima zote unapoendesha gari
Speed zinabadilika kutokana na barabara na sehemu ulipo na lazima uzifuate

Sasa huko barabara hazina sign za wazi, Alama moja barabara nzima
Na hakuna anaezifuata
Police wa traffic wanakula hongo hata sheria wengine hawajui
 
Back
Top Bottom