WanaCamaraderie na wana Jamvi,
Hizi ndizo Issues.
i) Udini umetoka wapi katika hoja za Dr Slaa?
2) Yaani Chama kituhumiwe kuvunja Amani, mtu yeyote mwenye akili timamu ategemee Katibu Mkuu wa Chama hicho akae kimya tu. Cammon, wana jamvi let us be serious. Ni upuuzi wa aina hii kufumbia mambo ndio kulikotufikisha hapa tulipo kama Taifa.
3) Nimesema mara kadhaa, na ninmeirudia juzi Kigoma, palipo na ukweli na haki au misingi ya ukweli inapofumbiwa macho tutapiga kelele. Hakuna aliye juu ya sheria, haki, ukweli. Hata "Mungu angelikuwa anafanya makosa kama hayo tungelimkemea", kwa bahati nzuri hafanyi makosa. Hiyo ni kuonyesha kuwa hakuna chini ya mbingu ambaye hatakemewa au kusahihishwa kama kwa misingi ya kisheria, ukweli tunaamini amekosea. Ikumbukwe hakuna mwenye "monopoly ya ukweli". Truth is but and is indivisible, hivyo iwe kiongozi wa dini (yeyote), iwe kiongozi wa Serikali wa ngazi yeyote atakemewa au kukosolewa kwa kadiri ya uzito wa kosa au upotoshaji. Wana JF hao wanaojadili personalities badala ya issues mimi hawanisumbui kwa vile tunajua "simple minds discuss people and great minds discuss issues". Tatizo hapa ni issues zilizokuwa raised na kiongozi wa dini je zina ukweli au la, kama sivyo hatuwezi kukaa kimya wakati Taifa linapotoshwa,inaweza kuwa kwa kutokujua kiongozi huyo au kwa malengo yeryote aliyonayo.