Dk Slaa asema Mufti hakufanya utafiti

Dk Slaa asema Mufti hakufanya utafiti

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa amewataka viongozi wa dini nchini kufanya utafiti kabla ya kutoa matamko yao katika vyombo vya habari.Kauli hiyo ya Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Sheikh Mkuu wa Tanzania , Mufti Issa bin Shaaban Simba kukishutumu chama hicho kwamba maandamano yake kinayofanya hivi sasa yana lengo la kuvuruga amani ya nchi.

Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema ameshangazwa na kauli iliyotolewa na Mufti Simba kuwa chama chake kina lengo la kuvuruga amani nchini.“Nimeshangazwa sana na kauli ya Sheikh Mkuu, Mufti Simba aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Kimsingi kama alitaka kujua undani wa maandamano yetu angetuuliza kuliko kutoa tamko bila kujua hata undani wa Chadema,” alisema na kuongeza kuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitoa tamko bila ya kufanyia utafiti jambo ambalo linawafanya watoe maelezo yasiyo na ukweli na yanayolenga kuwapotosha na kuchochea chuki kwa wafuasi wake.Dk Slaa alisema Chadema inajua inachokifanya, hivyo kama mtu anahitaji kujua madhumuni ya maandamano yao ni vyema akawauliza ili

kitoe ufafanuzi kwa kuwa kila jambo liko wazi kwa maslahi ya wananchi wenyewe.“Sioni haja ya kulumbana na kujibizana kila kukicha kupitia vyombo vya habari. Kama wana hoja ya msingi wailete sisi tutaijibu kwa hoja siyo kuongea mambo kwa mtazamo na propaganda za kisiasa. Unapozungumza ni lazima kuwe na utaratibu wa kutafiti unachokizungumza,” alisema Dk Slaa.

Aliwataka viongozi wa dini kuhudhuria mikutano ya chama hicho ili kusikia na kujua kinachozungumzwa na Chadema kuliko kusubiri kusimuliwa na watu na kisha kuyaamini maneno yao.Alisema amelazimika kumjibu Mufti Simba kwa kuwa amesikitishwa na kauli hiyo ambayo alisema badala ya kuwasaidia Watanzania, inachochea chuki na kuruhusu ufisadi kuendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam juzi, Mufti Simba alisema: “Wanasiasa wanataka kuivuruga nchi kwa visingizio kuwa wanataka kuilinda amani, hivyo Waislamu tumeamua kuvunja ukimya uliodumu kwa muda mrefu na kuamua kukekemea vitendo hivyo.”Mjadala wa uhalali wa mikutano na maandamano ya Chadema uliibuliwa na Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia taifa kupitia redio na televisheni mwishoni mwa Februari kwamba chama hicho cha upinzani kina lengo la kuleta machafuko nchini.

Kauli hiyo ilifuatiwa na onyo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira kuwa Chadema kisije kuilaumu Serikali itakapokosa uvumilivu na kuanza kutumia dola kukishughulikia.Wakatihuo huo; Dk Slaa amesema ziara zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika wizara mbalimbali ni matunda ya maandamano ya chama hicho katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Alisema Serikali imeanza kutekeleza madai mengi ambayo Chadema ilitaka iyafanyie kazi ndani ya siku tisa. Hata hivyo, alisema chama hicho kitaendelea kutia shinikizo hadi mambo yote yatakapokamilishwa.“Hayo ni matunda ya maandamano yetu japo utekelezaji wake hauridhishi kwa kiwango tulichotaka.

Lakini imedhihirika kwamba mambo hayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi. Inashangaza kuona wengine wanayaita maandamano kuwa ni ya kuvuruga amani,” alisema.Alisema kuwa matunda mengine ya maandamano ya Chadema yaliyofanyika mkoani Mwanza ni tamko la Rais la kupunguza bei ya sukari kutoka Sh2,200 hadi Sh1,700.Rais Jakaya Kikwete anatembelea wizara mbalimbali kukagua utekelezaji wa maagizo ya yake.

Tunashukuru kwa kuwasilisha maneno ya kadinali Pengo kwa niaba yake, Slaa acha kutumika na wakatoliki
 
we Slaa mpuuzi sana acha kudharau dini za wenzako, Pengo alipotoa maoni yake kuhusu maandamano alifanya utafiti lini? yani nyie mnaposifiwa hakuna comment yoyote ila mkikoselewa tuu,ndo mnakuja na matamko ya kipuuzi! hiyo siasa badilikeni na acheni ulimbukeni coz mnatubero sana

Kwani Pengo alitoa maagizo gani kwa wasaidizi wake na waumini? Si alisema ni mtazamo wake binafsi? Tujaribu kuelewa kabla ya kuleta bifu. Bwana Simba yeye ameagiza wasaidizi wake na waumini kuhusu CHADEMA...ndio kukosa utafiti kewnyewe huko
 
Huyu mzee akili anazo? utafiti afanye saa ngapi, si kudandia gari kwa mbele na hujui liendako?
 
we Slaa mpuuzi sana acha kudharau dini za wenzako, Pengo alipotoa maoni yake kuhusu maandamano alifanya utafiti lini? yani nyie mnaposifiwa hakuna comment yoyote ila mkikoselewa tuu,ndo mnakuja na matamko ya kipuuzi! hiyo siasa badilikeni na acheni ulimbukeni coz mnatubero sana

Wewe hujui kusoma, umeona wapi Dr Slaa akizungumzia juu ya dini bali anaongea juu na Shekhe; wewe ndio mdini sana na tena si msttarabu kwani kutukana ni part of argument. I wonder why mods keep people like you on this forum, you place should be vijiweni ambako unaweza kuwa huru ku gossip na kutukana japo nayo hiyo sio ustaarabu lakini kwa vile huna, such a place will surely suti you. Otherwise mods please ban this creature who insults and insults people we respect????? Abomination
 
Sio Kosa lake

Join Date : 23rd March 2011
Posts : 7
Thanks
1
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power : 0

Wewe hujui kusoma, umeona wapi Dr Slaa akizungumzia juu ya dini bali anaongea juu na Shekhe; wewe ndio mdini sana na tena si msttarabu kwani kutukana ni part of argument. I wonder why mods keep people like you on this forum, you place should be vijiweni ambako unaweza kuwa huru ku gossip na kutukana japo nayo hiyo sio ustaarabu lakini kwa vile huna, such a place will surely suti you. Otherwise mods please ban this creature who insults and insults people we respect????? Abomination
 
HAMAD RASHID-GOGORO, CUF-MASLAHI NA CCM-UFISADI MJUE FIKA USALAMA WA NCHI YETU UNAYUMBISHWA NA 'MUAFAKA WA MASLAHI BINAFSI' YA VYEO NA KUJIUNGA KULE NA NGURUWE KULA MABUA NA UFISADI
ULIOKITHIRI NCHINI

Jamani kuna uwezekano Wa-Tanzania tukawa na tofauti nyingi tu nchini zikiwemo zile za kitamaduni, kiimani, kijinsia na kadhalika lakini matatizo yanayotuhatarishia amani nchini, Wakristo kwa Waislmu na kote Bara na Visiwani ni zile zile!!

Nasema matatizo ya kusisitizwa tu AMANI na kufichwa kule kwa HAKI kwa raia ni chanzo cha matatizo kibao yanayotukaba kila siku nchini kama vile: (1) UFISADI uliokithiri ndani ya serikali ya CCM yatuathiri sote, (2) Muafaka wa CUF kujiunga na CCM kula mabua kwa pamoja na kuwaacha wananchi solemba kwenye umasikini wa kutupwa ni letu sote.

Kama haitoshi, pia (3) Utaratibu wa Serikali ya Muungano usiona tija, na fursa sawa wa moja kwa moja kwa mwananchi wa kawaida, (4) ukosefu wa ajira, (5) elimu duni, (6) Maisha kupanda gharama kila kukicha ni letu sote hivyo kwa hali ya kawaida kabisa Mtanzania hahitaji KAMPENI ZA KUTIANA HOFU pale tunapojiunga kama taifa kujikomboa kwa kudai haki zaidi na Katiba Mpya nchini!!!

... hatuwe kujua vizuri; wenzetu wa CCM na CUF waulizwe vizuri juu ya hilo jambo wanaloliona peke yao tu hapa nchini kuhusu usalama kutetereshwa ambalo sisi wengine hatulion.

Lakini kama kudai HAKI SAWA NA MASLAHI KWA UMMA wa Tanzania ndicho hasa kile kinachowakosesha amani wale MAFISADI walioko serikalini na kuitwa KUHATARISHA USALAMA WA NCHI na basi CHADEMA kazeni mwendo mdundo kwa sana tu.

Wa-Tanzania tunaakili sana kote Bara na Visiwani na pia tunafahamu fika kwamba wale wanaoingia muafakaka na serikali ya CCM gizani kwa maslahi binafsi ya kupata vyeo, mijumba, na mashamba ndio hasa wanaoHATARISHA USALAMA WA NCHI YETU.

Ndugu zetu akina Hamad Rashid, CUF-Maslahi na CCM-Ufisadi, acheni mara moja kuchezea akili za Mtanzania wa leo kote Bara na Visiwani tunasema kwamba Hatudanganyiki wala Hatugawanyiki kwenye Kutafuta Maslahi yetu kama Umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Wewe hujui kusoma, umeona wapi Dr Slaa akizungumzia juu ya dini bali anaongea juu na Shekhe; wewe ndio mdini sana na tena si msttarabu kwani kutukana ni part of argument. I wonder why mods keep people like you on this forum, you place should be vijiweni ambako unaweza kuwa huru ku gossip na kutukana japo nayo hiyo sio ustaarabu lakini kwa vile huna, such a place will surely suti you. Otherwise mods please ban this creature who insults and insults people we respect????? Abomination
read btn lines anawezaje kusema muft hakufanya utafiti?? ana uhakika gani kama sio dharau kwa waislamu wote?? Slaa needs to ask for the apology,ule ulikuwa ni mkutano wa masheikh na maulamaa wa nchi nzima waliokuwa wakijdaili hali ya siasa nchini libya na Tanzania kwahiyo muft Simba alitoa hitimisho ya yaliyoongelewa kwahiyo slaa kwa maana nyingine ameudharau mkutano wote ule! lazima aombe msamaha
 
panic panic panic..... je ni kweli hajafanya utafiti ....? je kuambiwa hujafanya utafiti ni dharau .... all in all hata wewe umekurupuka kwani hujafanya utafiti kama mufti hakufanya utafiti
 
KATIBU

Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema ameshangazwa na kauli iliyotolewa na Mufti Simba kuwa chama chake kina lengo la kuvuruga amani nchini.“Nimeshangazwa sana na kauli ya Sheikh Mkuu, Mufti Simba aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Kimsingi kama alitaka kujua undani wa maandamano yetu angetuuliza kuliko kutoa tamko bila kujua hata undani wa Chadema,” alisema na kuongeza kuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitoa tamko bila ya kufanyia utafiti jambo ambalo linawafanya watoe maelezo yasiyo na ukweli na yanayolenga kuwapotosha na kuchochea chuki kwa wafuasi wake.Dk Slaa alisema Chadema inajua inachokifanya, hivyo kama mtu anahitaji kujua madhumuni ya maandamano yao ni vyema akawauliza
.

SWALI,je Pengo aliwauliza chadema pale alipotoa TAMKO lake kuhusiana na maandamano ya CDM? na je mbona CDM hawakutoa tamko lolote kuhusiana na tamko la pengo au kwavile lilikuwa liko upande wao basi haliitaji kutolewa ufafanuzi? je pengo alifanya utafiti wapi kabla ya kutoa tamko? au wewe bwana slaa ulimpelekea taharifa za maendeleo ya chama kama ilivyo ada? NARUDIA TENA SLAA ACHA UPUUZI NA ACHA KUKURUPUKA UNAPOTOA MATAMKO NYETI
 
you fool,read btn lines anawezaje kusema muft hakufanya utafiti?? ana uhakika gani kama sio dharau kwa waislamu wote?? Slaa needs to ask for the apology,ule ulikuwa ni mkutano wa masheikh na maulamaa wa nchi nzima waliokuwa wakijdaili hali ya siasa nchini libya na Tanzania kwahiyo muft Simba alitoa hitimisho ya yaliyoongelewa kwahiyo slaa kwa maana nyingine ameudharau mkutano wote ule! lazima aombe msamaha

My friend, I am not a fool...and your insults wont do me any harm except they show me that you have no capacity to reason and follow arguments, and for that I truly pity you...to say that someone needs to do research of his utterance does not have any religious connotation...kwamba tu mtu ni mufti does not place such person in a position that all his utterances will be taken at face value...think about it, go to school, get wisdom and understanding...then write arguments na sio matusi...matusi ni dalili ya kukosa values..sijui ulilelewa magangeni?
 
we Slaa mpuuzi sana acha kudharau dini za wenzako, Pengo alipotoa maoni yake kuhusu maandamano alifanya utafiti lini? yani nyie mnaposifiwa hakuna comment yoyote ila mkikoselewa tuu,ndo mnakuja na matamko ya kipuuzi! hiyo siasa badilikeni na acheni ulimbukeni coz mnatubero sana

mpuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuzi ni wewe tena usiyejua maana.nenda zako unaujua uislamu vizuri kweli,Laiti ungejua anachowafanyia simba na kuwauza kinyemela usingesema.

Msiwe watu wa papara tu fanyeni uchunguzi simba ameyafanya hayo kwa msingi gani na anania gani,yapo mambo mengi nyuma ya pazia ambayo watu kama wewe hamyajui njoo nikwambie machache.Mjinga kweli unajifanya unahasira hasira zisizo na umakini.
 
watu wanaona udini tu, Mbona kabala ya uchaguzi Ask Kulola alibainika kutaka ku kampeni dhidi ya chama tawala wan JF walimfombani akama mpira wa kona? wakina Pinda, Membe, Lowassa, Mkapa, Balali etc wote si wakristo hao? jamani focus kwenye mambo ya kuleta haki kwa kila mtanzania, sio ukabila wala udini, mbona watu wana wapongeza wakina Sabodo wanapotoa misaada kwa jamii bila kuuliza dini wala kabila zao?
 
hivi mufti wetu ana elimu dunia kiasi gani?

no offence intended plz.. just wanna know
 
My friend, I am not a fool...and your insults wont do me any harm except they show me that you have no capacity to reason and follow arguments, and for that I truly pity you...to say that someone needs to do research of his utterance does not have any religious connotation...kwamba tu mtu ni mufti does not place such person in a position that all his utterances will be taken at face value...think about it, go to school, get wisdom and understanding...then write arguments na sio matusi...matusi ni dalili ya kukosa values..sijui ulilelewa magangeni?

okey the WISEMAN,am asking you did Pengo make any research? how come his statement was not welcomed with doubts? be fair na sio kuegemea upande fulani
 
you fool,read btn lines anawezaje kusema muft hakufanya utafiti?? ana uhakika gani kama sio dharau kwa waislamu wote?? Slaa needs to ask for the apology,ule ulikuwa ni mkutano wa masheikh na maulamaa wa nchi nzima waliokuwa wakijdaili hali ya siasa nchini libya na Tanzania kwahiyo muft Simba alitoa hitimisho ya yaliyoongelewa kwahiyo slaa kwa maana nyingine ameudharau mkutano wote ule! lazima aombe msamaha
hawa wameanza kuchanganyikiwa,Gadafi kungo'lewa unafikiri watakuwa na amani.kwani jeuri yote wameitoa huko.
waache tu waianzishe ikivuma hapa itakuwa mbaya kuliko.
 
okey the WISEMAN,am asking you did Pengo make any research? how come his statement was not welcomed with doubts? be fair na sio kuegemea upande fulani

Lets say Pengo alifanya (au alifanyiwa) utafiti...now tell us Simba alifanya utafiti?
 
Tunashukuru kwa kuwasilisha maneno ya kadinali Pengo kwa niaba yake, Slaa acha kutumika na wakatoliki

Kwani hujui huyu ni pandikizi la PAPA huyu. Anaitwa Dr Padre Slaa, sasa unashangaa nini?

Slaa hatudanganyikiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom