Dk Slaa asema Mufti hakufanya utafiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa asema Mufti hakufanya utafiti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzambia, Mar 24, 2011.

 1. m

  mzambia JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbroad Slaa amewataka viongozi wa dini nchini kufanya utafiti kabla ya kutoa matamko yao katika vyombo vya habari.Kauli hiyo ya Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Sheikh Mkuu wa Tanzania , Mufti Issa bin Shaaban Simba kukishutumu chama hicho kwamba maandamano yake kinayofanya hivi sasa yana lengo la kuvuruga amani ya nchi.

  Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema ameshangazwa na kauli iliyotolewa na Mufti Simba kuwa chama chake kina lengo la kuvuruga amani nchini.“Nimeshangazwa sana na kauli ya Sheikh Mkuu, Mufti Simba aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
  Kimsingi kama alitaka kujua undani wa maandamano yetu angetuuliza kuliko kutoa tamko bila kujua hata undani wa Chadema,” alisema na kuongeza kuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitoa tamko bila ya kufanyia utafiti jambo ambalo linawafanya watoe maelezo yasiyo na ukweli na yanayolenga kuwapotosha na kuchochea chuki kwa wafuasi wake.Dk Slaa alisema Chadema inajua inachokifanya, hivyo kama mtu anahitaji kujua madhumuni ya maandamano yao ni vyema akawauliza ili


  kitoe ufafanuzi kwa kuwa kila jambo liko wazi kwa maslahi ya wananchi wenyewe.“Sioni haja ya kulumbana na kujibizana kila kukicha kupitia vyombo vya habari. Kama wana hoja ya msingi wailete sisi tutaijibu kwa hoja siyo kuongea mambo kwa mtazamo na propaganda za kisiasa. Unapozungumza ni lazima kuwe na utaratibu wa kutafiti unachokizungumza,” alisema Dk Slaa.

  Aliwataka viongozi wa dini kuhudhuria mikutano ya chama hicho ili kusikia na kujua kinachozungumzwa na Chadema kuliko kusubiri kusimuliwa na watu na kisha kuyaamini maneno yao.Alisema amelazimika kumjibu Mufti Simba kwa kuwa amesikitishwa na kauli hiyo ambayo alisema badala ya kuwasaidia Watanzania, inachochea chuki na kuruhusu ufisadi kuendelea.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam juzi, Mufti Simba alisema: “Wanasiasa wanataka kuivuruga nchi kwa visingizio kuwa wanataka kuilinda amani, hivyo Waislamu tumeamua kuvunja ukimya uliodumu kwa muda mrefu na kuamua kukekemea vitendo hivyo.”Mjadala wa uhalali wa mikutano na maandamano ya Chadema uliibuliwa na Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia taifa kupitia redio na televisheni mwishoni mwa Februari kwamba chama hicho cha upinzani kina lengo la kuleta machafuko nchini.

  Kauli hiyo ilifuatiwa na onyo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Steven Wassira kuwa Chadema kisije kuilaumu Serikali itakapokosa uvumilivu na kuanza kutumia dola kukishughulikia.Wakatihuo huo; Dk Slaa amesema ziara zinazofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika wizara mbalimbali ni matunda ya maandamano ya chama hicho katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

  Alisema Serikali imeanza kutekeleza madai mengi ambayo Chadema ilitaka iyafanyie kazi ndani ya siku tisa. Hata hivyo, alisema chama hicho kitaendelea kutia shinikizo hadi mambo yote yatakapokamilishwa.“Hayo ni matunda ya maandamano yetu japo utekelezaji wake hauridhishi kwa kiwango tulichotaka.

  Lakini imedhihirika kwamba mambo hayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi. Inashangaza kuona wengine wanayaita maandamano kuwa ni ya kuvuruga amani,” alisema.Alisema kuwa matunda mengine ya maandamano ya Chadema yaliyofanyika mkoani Mwanza ni tamko la Rais la kupunguza bei ya sukari kutoka Sh2,200 hadi Sh1,700.Rais Jakaya Kikwete anatembelea wizara mbalimbali kukagua utekelezaji wa maagizo ya yake.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Huyu atafanya utafiti saa ngapi? Anazo hizo akili?
   
 3. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kazi kubwa sana kampa shehe mkuu,"KUFANYA UTAFITI" . Tutasikia jibu la utafiti,ngoja tuone
   
 4. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,076
  Likes Received: 1,112
  Trophy Points: 280
  Taratibu muheshimiwa naona leo umekuwa mkali kweli, salama lakini?
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Haa haa haaa! Nimecheka sana asubuhi hii, na baada ya kutafakari, nikaona kuna ukweli fulani!
   
 6. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,980
  Likes Received: 20,366
  Trophy Points: 280
  Kauli ya sheikh ni ya kuangaliwa kwa umakini mkubwa, tunamheshimu sana kwa wadhifa wake ndani ya dini yetu na jamii kwa ujumla lakini kamwe asijiaminishe kuwa yeye anaipenda sana amani ya nchi hii kuliko umma wa watanzania wote. Amani yetu inakuwepo pale tu HAKI inapokuwa inapatikana na kufikika kwa kila mtanzania, huwezi kunishawishi kwa hali ya tofauti ya kipato miongoni mwa wakazi wa mjni (vijijini utofauti/ kiwango cha umaskini ni kikubwa zaidi) watu hawa wana amani, utulivu wa kundi kubwa la watz usikupofushe na ukadhani wana amani. Mwenye njaa hana amani kiongozi wangu
   
 7. i

  itahwa Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  we Slaa mpuuzi sana acha kudharau dini za wenzako, Pengo alipotoa maoni yake kuhusu maandamano alifanya utafiti lini? yani nyie mnaposifiwa hakuna comment yoyote ila mkikoselewa tuu,ndo mnakuja na matamko ya kipuuzi! hiyo siasa badilikeni na acheni ulimbukeni coz mnatubero sana
   
 8. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mhhh ama kweli viongozi wa dini sasa mnapotoka sana sana
   
 9. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Labda alifanya utafiti.hiyo ni perception yake.wafuasi wake wana uwezo wa kuchuja.na kuamua..tuwape hiyo chansi..changes haiwez kufungamana udini..bali utaifa.
   
 10. F2S

  F2S JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 16, 2008
  Messages: 216
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika maelezo hakuna mahali amedharau dini ( na hawezi kufanya hivyo) ila ameshauri viongozi wetu wa dini zote wafanye utafiti ndipo watoe matamko. Kwa hiyo hoja sasa ni kujua kama Pengo alifanya utafiti ama la. Kulijua hilo ni pale unaposikia tamko ambalo content zake ni nje ya kile ambacho hicho chama kinawakumbusha watawala. Kumbukeni vyama vya upinzani ni watch dog kwa hiyo lazima viikosoe serikali na kuihimiza kurectify mambo yaendayo vibaya.
   
 11. h

  hamidshaban JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Fikiri kwa makini. Huyo shehe hata maana ya utafiti hajui. Alisoma wapi?si kila mtu ana uwezo wa kutafiti! Kwa hapa Slaa nae kakosea. Angempotezea tu.
  F
   
 12. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ameongea pumba sana ndio maana Anamjibu hivyo. Acha Udini kuleta mambo ya dini wewe [Neno Baya] !!!!!!!

   
 13. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ameongea pumba sana ndio maana Anamjibu hivyo. Acha Udini kuleta mambo ya dini wewe [Neno Baya] !!!!!!!

   
 14. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa mtazamo wangu binafsi CDM wako sahihi kwanye maandamano na mikutano wanayofanya,hili ndio la msingi swala la shehe flan au askofu fulani kasema nini sio la msingi kwangu,tusilitazame swala lolote kidini kwani unapofanya hivyo unakua wewe mwenyewe ni mdini kitu ambacho hakistahili kwa dunia ya leo,hakuna anayedharau dini ya mwenzake kwa dunia ya leo na anayehisi kudharauliwa amepitwa na wakati na mawazo yake ni finyu na yeye ndiye mdini na ndiye kiini cha huo udini hivyo kua makini na tafakari,kwanye Jf hatutegemei watu wa mtizamo huu wawepo
   
 15. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Inaonekana jana usiku ulilala njaa na sasa hivi hujapata kahawa na kashata ndio maana una hasira.. pole mjomba... majority ya wa TZ hawapuzii kauli za Dr Slaa hata siku moja... na ni kawaida ya watu kama nyinyi kujiingiza na hoja ya udini na kumtukana Dr bila sababu, tumeshawazoea....
   
 16. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Wakati mwingine uwe unasoma thread kwa umakini ndiyo utoe maelezo.
   
 17. L

  LAT JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mimi ningeshauri taasisi zote za kidini ziendelee kujikita zaidi kuanzisha shule, vyuo, vituo vya afya, zahanati na mahospitali ..... ! hii itawafanya wawe busy zaidi kuliko kukosa shughuli za kufanya
   
 18. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 160
  BAKWATA ni taasisi...ambayo kiongozi wake mkuu ni Mufti. Haina maana BAKWATA haina watu wengine ambao ni wasomi wa kutosha kufanya utafiti wakajua mantiki ya maandamano ya waTanzania (japokuwa wanapropaganda wanayaita maandamano ya Chadema), na kisha wakamshauri Mufti aseme nini. Kama alikurupuka (kumradhi...meant no offense) akatolea tamko kitu ambacho hata hajui mantiki yake lazima 'ashushuliwe', kwani anakuwa hana tofauti na m'mbeya wa uswazi.
   
 19. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wadau,
  Sheikh mkuu alialika waislamu wote na maulamaa wafike msikiti wa Al-farouq kwa ajili ya kujadili hali ya machafuko huko Libya na muenendo wa siasa za Tanzania, Tusimlaumu Mufti kwani hakufanya hayo binafsi. Ni baada ya mkutano huo ndipo akaja na conclusion yake, mkutano huo ulitangazwa saana via Radio kheir kwa kuwaalika wote wafike. Kauli ya mufti isichukuliwe kimzaha, it means something.
  Kiuhalisia wa Tanzania ni kwamba...kumetokea tabaka kubwa na linalosambaa kwa kasi isiyozuilika kirahisi (UDINI). Mufti katoa kauli baada ya Pengo kutoa kauli, HEBU TUYAJADILI MATAMKO YAO KIUJUMLA YALILENGA NINI? Mufti vs Kardinali.
   
 20. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35

  Wewe unaufinyu wa fikira, yaani nakushauri uwe unafikiri na ikiwezekana omba ushauri kwanza kabla ya kuandika, hakuna anayezarau Dini hapa, ila kiongozi wa dini akiongea Pumba ni aibu sio kwa dini ile tu bali hata kwa taifa letu zima, sasa kama Kiongozi mkuu wa dini anaongea vile, haiingii akilini, maana washauri anao tena wasomi wazuri, hapa inamaan hata ushauri wao hasikilizi! balaa hili!
   
Loading...