Dk.Slaa anasa waraka wa siri CCM, afichua wizi wa mabilioni hazina

.
• Anasa waraka wa siri CCM, afichua wizi wa mabilioni Hazina



KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.Willbrod Slaa, sasa ametamka rasmi kwamba nchi haitatawalika, kwani chama chake hakiko tayari kuona Watanzania wakiendelea kuwa katika hali ngumu ya maisha, huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikitekeleza mkakati wa siri wa kuwajaza matumaini hewa badala ya kutatua matatizo yao.
Dk. Slaa ameeleza kuunasa waraka wa siri wa CCM ambao ndani yake chama hicho kimekiri waziwazi kupoteza ladha kwa umma, huku mkakati pekee wa kujinusuru ukielezwa kuwa ni kubadili sura za viongozi wa chama hicho ili kuwajengea matumaini mapya Watanzania.
Kwa mujibu wa Dk.Slaa, waraka huo wenye mhuri mkubwa wa neno “siri” uliandaliwa na baadhi ya wataalam wa CCM waliofanya tathmini ya hali ya chama chao kisiasa na kuuwasilisha kwa viongozi wa juu wa chama hicho ambao tayari wameanza kuufanyia utekelezaji wa “kujivua gamba” kwa lengo la kuwapa matumaini hewa wananchi.
Dk. Slaa alifichua siri za waraka huo wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja wa shule ya sekondari Msakila mjini Sumbawanga ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya chama hicho mkoani Rukwa, baada ya kuutikisa mkoa wa Mbeya kwa maandamano na mikutano ya hadhara kwa siku tatu mfululizo.
Alisema katika waraka huo CCM imekiri kuwa haikubaliki kwa Watanzania na kwamba iliporomoka sana katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, lakini badala ya kurejesha tunu za taifa kama uadilifu, upendo, amani, umoja na uwajibikaji wa kuleta maendeleo yatakayoirejeshea imani toka kwa wananchi, chama hicho kimeamua kubadili tu sura za viongozi wake wa kitaifa.
“CHADEMA tunafanya mambo kwa utafiti. CCM wana waraka wa siri uliowafanya wajivue gamba lakini wanaume tayari tumeshaunasa, tena una mhuri mkubwa wa neno siri lakini tayari tunao. Katika waraka wao CCM wamekiri wenyewe kwamba hawakubaliki tena kwa Watanzania walio wengi, wamekiri wenyewe kwamba wamepoteza ladha kwa wananchi. Wamekiri wenyewe katika waraka huo, kwamba hawakubaliki kwa sababu wameacha siasa ya ujamaa na kujitegemea.
“Na ni kweli wameacha siasa ya ujamaa na kujitegemea. Mabilioni ya Kikwete sio ujamaa na kujitegemea. Mabilioni ya mtoto wake, anayeitwa Ridhawani nayo ni ushahidi tosha kuwa wameacha ujamaa na kujitegemea kama walivyokiri wenyewe kwenye waraka wao.
“Tatizo lao ni kwamba badala ya kuacha ufisadi na kurejesha tunu za taifa kama uadilifu, upendo, amani, umoja na uwajibikaji…badala ya kupunguza kodi kwenye mafuta, sukari, saruji, na bidhaa nyingine, ili wajijengee uhalali kwa umma, wao katika waraka wao wameamua wabadili sura za viongozi kwa kujivua gamba. Hawataji popote kwenye waraka wao jinsi watakavyoboresha maisha yenu,” alisema Dk.Slaa na kuongeza.
“CHADEMA hatuko tayari kuona Watanzania wakiteseka huku CCM yenye serikali badala ya kuchukua hatua za dharura kuwanusuru, inapanga kuendelea kuwadanganya kwa kubadili viongozi kwa kujivua gamba. Arusha nilitoa hotuba moja wakasema Dk. Slaa mchochezi…sasa leo nawatuma usalama wa taifa nendeni mkawaambie CCM kwamba nchi haitatawalika. Wasipochukua hatua CHADEMA itachukua hatua…kama Watanzania hawajui wanakula nini, wanavaa nini, watoto wao wanasoma vipi, wanatibiwa vipi, basi nchi hii haitatawalika.”
Alisisitiza kuwa nchi haitatawalika kwani kila kukicha ufisadi unakithiri badala ya kupungua huku akibainisha kuwa hata ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ya hivi karibuni imeonyesha katika wizara moja pekee, wizara ya fedha na uchumi, jumla ya sh bilioni 365 ziliibiwa wakati zingeweza kutumika kunusuru maisha ya Watanzania.
Mwenyekiti wa chama hicho akihutubia wakazi hao wa Sumbawanga, alisema kupitia maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na chama hicho nchi nzima, CHADEMA imedhamiria kuamsha nguvu ya umma katika kuishinikiza serikali kupunguza kodi kwenye bidhaa na huduma muhimu ili bei zishuke na maisha ya wananchi yawe nafuu.
Alisema kupanda kwa gharama za maisha kumesababishwa na ufisadi na sera mbovu za serikali ya CCM, ambayo inawatoza kodi kubwa wananchi maskini kupitia bidhaa na huduma mbalimbali huku serikali hiyo hiyo ikiwasemehe kodi wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa.
Katika hotuba yake hiyo iliyoonekana dhahiri kuwateka wakazi wa Sumbawanga, Mbowe alisema CHADEMA haipingi watu kulipa kodi, lakini haiko tayari kuona Watanzania maskini wakilipishwa kodi kubwa, huku serikali ikishindwa kuwapa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Akifafanua zaidi historia ya kodi na athari zake kwa wananchi, kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni alisema baada ya serikali ya Rais Benjamin Mkapa kuondoa kodi ya maendeleo, ilileta kodi nyingine ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambayo wananchi wote sasa wanatozwa kila wanaponunua bidhaa dukani na kulipia huduma mbalimbali kama usafiri.
“Nyerere alikuwa akikusanya kodi bilioni saba kwa mwezi, mzee Mwinyi aliondoka akiwa anakusanya kodi ya bilioni 27, akaja Mkapa yeye hadi anaondoka alikuwa anakusanya bilioni 300 na ushei. Baada ya hapo akaja Kikwete, yeye anakusanya bilioni 420 kwa mwezi. Anakusanya fedha nyingi kwa sababu kuna kodi ya VAT iliyoongezwa katika bei za bidhaa na huduma mnazolipia. Mnalipa kodi bila kujua, mnalipa kodi kwenye mafuta, kwenye soda, usafiri, sukari, sanda, pipi...kila kitu kodi kodi kodi,” alisema Mbowe na kuongeza.
“Kwa sababu ya kodi ya VAT, leo katika nchi hii kila mwananchi analipa kodi, mtoto, mjane, kijana, mwanafunzi wote wanalipa kodi …hadi maiti nazo zinalipiwa kodi mnaponunua sanda kwa ajili ya kuzikia. ...lakini kodi hizo zinaishia kustawisha maisha ya vigogo wa serikali, wananchi wa Sumbawanga na Watanzania wengine wanazidi kuwa maskini, mmefikia mahali hamuwezi hata kununua kilo moja ya sukari kwa ajili ya chai au kilo ya mafuta mnaanza kupimiwa kwenye vifuko vya shilingi mia moja...hali ya hatari hii, taifa lina msiba wa umaskini, wananchi wanalia kila mahali sasa, kila kona ya nchi,” alisema.
Akitoa mfano wa jinsi kodi inavyofanya bei za vitu kuwa juu, Mbowe alisema katika kila Sh elfu moja anayotumia Mtanzania kununua bidhaa sokoni au dukani au kulipia huduma, serikali humkata kodi ya wastani wa sh 500 hadi 600, kodi ambayo kama ikiondolewa gharama za maisha zitakuwa nafuu.
“Soda moja inapotoka kiwandani inapaswa kuuzwa kwa Sh 150 lakini kwa sababu ya kodi iliyowekwa na CCM kuanzia viwandani soda moja mnauziwa kwa sh 500 hadi 600. Kila mnaponunua mfuko mmoja wa cement mnakatwa kodi ya Sh 7,500 ambayo kama ikiondolewa au kupunguzwa bei ya saruji itakuwa nafuu na wengi mtaweza kujenga.
“Kila chupa moja ya bia unayonunua unakatwa kodi ya sh 800. Ndiyo maana Kikwete kwa mwezi anakusanya bilioni 420 kutoka kwenu, lakini maendeleo hakuna. CHADEMA tutakomaa na suala la gharama za maisha ndani na nje ya bunge mpaka Watanzania maisha yao yawe nafuu,” alisema Mbowe na kushangiliwa.
Katika mkutano huo pia Mbowe aliwahamasisha wakazi wa Sumbawanga kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata Katiba mpya na kushinikiza katiba hiyo itokane na wananchi na sio itokane kwa utashi na maamuzi ya Rais Kikwete kama ilivyopendekezwa katika Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba.
Naye Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi hao alisema kwa nafasi yake kama Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, ameagizwa na chama chake kuwasilisha bajeti mbadala katika bunge lijalo la bajeti ambayo pamoja na mambo mengine itashinikiza serikali kupunguza kodi kwenye mafuta ya petroli na dizeli kwa asilimia 50 ili yauzwe kwa angalau Shs 1665 kwa lita kutoka kwenye bei ya zaidi ya sh 2000 ya sasa. “Gharama za maisha ziko juu kwa sababu ya mfumuko wa bei za mafuta ambao unasababisha na kodi. Bei ya mafuta ikishuka hadi 1,665 gharama za usafiri na bei za sukari na vyakula nazo zitakuwa angalau. Tutawataka waondoe kodi kwenye mafuta halafu wapunguze misahamaha ya kodi wanayoitoa kwa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa … serikali inasemehe bilioni 635 za kodi zinazopaswa kulipwa na matajiri, sasa hizo zikafidie kwenye mafuta baada ya kupunguza kodi. Wakikataa watakiona cha moto, tutafanya maandamano ndani na nje ya bunge mpaka kieleweke,” alisema Zitto.
 
najua kila anaeipenda nchi yetu anafurahi anapoona au kusikia matukio kama haya lakini kuna wachache wetu hawapendi kabisa kusikia,

mimi nikiwa mmoja wa wale wanaoitakia mema nchi yangu na wananchi wake nashauri cdm iimarishe sana ulinzi wa hawa viongonzi hasa wale wa kitaifa wala isiogope gharama katika kuajiri watu waliobobea katika hii fani ya ulinzi. nasisi tuendelee kuwaombea ulinzi wa mungu.
 
amani&utulivu ingawa viongozi wengi wanahubili amani ni unafiki huwezi ukasema kunaamani watanzania wachache wanaishi maisha yaanasa wengi maisha ya dhiki wanakufa kwamalelya mlo mmoja kwasiku wanakosa elim hukuwachache wanapeleka watoto wawo ulaya tanzania tunautulivu si amani hawa wengi wakitambuwa hakizawo zamsingi amani hi yakinafiki itapotea wote tunataka amani watawara msituibie kwakisingizio cha amani mtuakisema uozo wenu mnakimbilia anatakakuvuluga amani
 
Wakuu Salaam,
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Wilbroad Peter Slaa amerudia kauli yake ya kuwa nchi hii haitatawalika.

Dr. Slaa aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika jana mjini Sumbawanga.

Akihutubia maelfu ya wananchi wa mji huo Dr. Slaa alisema nchi hii haitatawalika kama wananchi wataendelea kuishi katika umasikini uliokithiri huku viongozi walio madarakani wakijineemesha wao wenyewe kupitia rasilimali za taifa na kodi za wananchi ambazo zinatozwa kupitia kila bidhaa anayonunua mwananchi na hivyo kumwongezea mzigo wa gharama za maisha ambazo zinazidi kupanda siku hadi siku.
Dr. Slaa alisema kama serikali imeshindwa kuchukua hatua stahiki kuwapunguzia wananchi makali ya maisha, wao chadema watachukua hatua.
Akinukuliwa na Tanzania Daima Dr. Slaa alisema: "....Nilisema Arusha wakasema Dr. Slaa mchochezi, leo narudia kusema nchi hii haitatawalika kama wananchi wataendelea kuishi katika umaskini uliokithiri, na kama wao ccm wameshindwa kuchukua hatua basi chadema itachukua hatua..."

Habari zaidi:
Tanzania Daima tarehe 10.05.2011

Ukisikia kuzeeka vibaya ndiko huku, nchi haitawaliki wakati serikali inaendelea na kazi zake kama kawaida, kwa njia ya kufanya maandamano tu km cdm wafanyavyo huwezi sema nchi haitawaliki kwa hakuna mgomo sehemu yoyote ambao utaathiri uchumi wa nchi
 
amani&utulivu ingawa viongozi wengi wanahubili amani ni unafiki huwezi ukasema kunaamani watanzania wachache wanaishi maisha yaanasa wengi maisha ya dhiki wanakufa kwamalelya mlo mmoja kwasiku wanakosa elim hukuwachache wanapeleka watoto wawo ulaya tanzania tunautulivu si amani hawa wengi wakitambuwa hakizawo zamsingi amani hi yakinafiki itapotea wote tunataka amani watawara msituibie kwakisingizio cha amani mtuakisema uozo wenu mnakimbilia anatakakuvuluga amani

Hiki kiswahili cha wapi mkuu ? na uhakika kabisa ww si mtanzania
 
Ukisikia kuzeeka vibaya ndiko huku, nchi haitawaliki wakati serikali inaendelea na kazi zake kama kawaida, kwa njia ya kufanya maandamano tu km cdm wafanyavyo huwezi sema nchi haitawaliki kwa hakuna mgomo sehemu yoyote ambao utaathiri uchumi wa nchi

Lakini ameahidi kuwa wao cdm watachukua hatua japo hakusema ni lini.
 
Nchi haitawaliki maana maisha ya mtanzania wa chini inaendelea kuwa mbaya siku hadi siku na hamna jitahada za serikali iliyoko madarakani za kumwondolea huu mzigo mtanzania wa kawaida bali imebaki kuwakumbatia mafisadi tu kwa hiyo itafika siku usemi huu wa Dr utatimia
 
Ni kweli nchi haiwezi kutawalika kwa staili hii ya utawala mbovu wananchi mafukara,serikali haiwezi kujiamulia mambo kienyeji kama vile wananchi hawapo,kama mambo yataendelea hivi kuna mambo yataendelea kutokea kwenye nchi hii na kusababisha mpasuko ambao serikali itakuwa haina ubavu wa kutuliza kelele za wananchi,is a matter of time!!
 
Walipokuwa wanachakachua hawakuzingatia implications za uovu wao katika kuongoza nchi.Watakoma!
 
Nchi haitawaliki maana maisha ya mtanzania wa chini inaendelea kuwa mbaya siku hadi siku na hamna jitahada za serikali iliyoko madarakani za kumwondolea huu mzigo mtanzania wa kawaida bali imebaki kuwakumbatia mafisadi tu kwa hiyo itafika siku usemi huu wa Dr utatimia

Slaa hana lolote bana kwani kauli zake nyingi ni za kisiasa zaidi kuliko kiutendaji, na hapo ndipo uthamani wake unapo pungua siku hadi siku
 
Maisha ya Mtanzania(mwananchi masikini)yanategemea sana huruma ya Mungu sbb tumaini lao lilishazimika siku nyingi Kama mshumaa.
 
Ukisikia kuzeeka vibaya ndiko huku, nchi haitawaliki wakati serikali inaendelea na kazi zake kama kawaida, kwa njia ya kufanya maandamano tu km cdm wafanyavyo huwezi sema nchi haitawaliki kwa hakuna mgomo sehemu yoyote ambao utaathiri uchumi wa nchi

Brainless
 
kuendelea kutawala 'kama kawaida' sio assurance kuwa nchi itaendelea kuwa hivyo kila siku. kwa hakika hali inavyozidi kuwa ngumu un-proportionally inaleta hisia na hamasa kwa wasiofaidika kuanza kuchukua hatua dhidi ya watawala (wafaida) wao. ikifikia hapo nchi haiwezi kutawalika. sidhani kama unahitaji kuwa 'beyond genius brain' kuliona hilo. ukitaka kuendelea kutawala 'kwa amani' tatua kero za wengi
 
Slaa hana lolote bana kwani kauli zake nyingi ni za kisiasa zaidi kuliko kiutendaji, na hapo ndipo uthamani wake unapo pungua siku hadi siku

Lakini kauli aliyotoa ni nzito mkuu, na hii mi naisikia kwake kwa mara ya tatu sasa. Wassira aliahidi kuwa akirudia tena anampeleka jela. Sasa mbona anairudiarudia lakini Wassira na Serikali kwa ujumla hakuna hatua zozote wanazochukua? Au wanamwogopa Slaa na cdm?
 
Ni kweli nchi haiwezi kutawalika kwa staili hii ya utawala mbovu wananchi mafukara,serikali haiwezi kujiamulia mambo kienyeji kama vile wananchi hawapo,kama mambo yataendelea hivi kuna mambo yataendelea kutokea kwenye nchi hii na kusababisha mpasuko ambao serikali itakuwa haina ubavu wa kutuliza kelele za wananchi,is a matter of time!!


Watanzania wamebweteka miaka mingi, na watawala wamejua kwamba wanatawala watu mabwege kwa hiyo wakawa wanafanya wanavyotaka ikiwa ni pamoja na kufanya ufisadi katika hazina ya nchi, katika mbuga za wanyama, katika madini nakadhalika nakadhalika. Watanzania wachache sasa wamegundua janja ya watawala ya kuwaibia rasilmali za nchi. Nasema wachache kwa kuwa bado watanzania walio wengi hasa kule vijijini bado hawajaelewa kinachoendelea na wanaiona ccm kama ndiyo mama yao na baba yao na bila hiyo mambo hayatakwenda. Amani na utulivu ambao ndiyo umekuwa ngao ya watawala kila wanapoona wamezidiwa sio amani na utulivu kwa hakika bali ni ujinga tu wa watanzania uliojikita katika woga wa kudai haki zao. Hata hivyo jinsi hali ya maisha inavyozidi kuwa ngumu kwa watanzania wa kawaida mpaka kukosa hata ule mlo mmoja wa siku hiyo inayoitwa amani na utulivu itatumbukia tumboni maana pale watu watakapoona hawana hata faida ya kuishi watakuwa tayari kufanya lolote kwa sababu wataona kwao kuishi ni mateso na hakuna faida na kufa pengine ndiyo itakuwa heri yao. Huko ndiko tunakoelekea kwa sababu watawala wetu wameshapofuka masikio kwa raha ya ufisadi. Na hali hiyo ndiyo anayosemea Dr. kuwa nchi haitatawalika. Asalam aleikum
A%20S%20cry.gif
 
Slaa hana lolote bana kwani kauli zake nyingi ni za kisiasa zaidi kuliko kiutendaji, na hapo ndipo uthamani wake unapo pungua siku hadi siku


pole sana,mda si mrefu mtawashuhudia watanzania mnaowadharau kila kukicha.umaharufu wenu ndio unapotea watanzania ndio tunaofanya maamuzi sasa na tuko tayari kwa lolote kwa mmetunyanyasa vyakutosha na chama kilichojaa majambazi.kazi kuwakamata vibaka mnaita majambazi wakati majambazi wa kweli ni ninyi mnaovaa suti.
saa na wakati umewadia.
 
CCM wenyewe wenyewe walishajua chama chao kimeshakufa, sasa hizo semina elekezi za nini? watu wanafikia level kama hiyo hawajui wajibu wao kuwatumikia wananchi? inasikitisha sana.

Haya yote anayosema DR. ni ya ukweli ila wao watawaambia wananchi eti mzushi wakifikiri wananchi ni wale wa enzi zile za "Zidumu fikra sahi hi za mwenyekiti", time will tell lakini CCM is no more guys.
 
the plain truth is Tanzania will be a better place if ccm is removed from power. no matter which party comes after it, it will do better than ccm. and the precedent that will be set by tanzanians will be accountability. you are given ridhaa ya kutawala because we want you to work for us. you dont work for us, we remove you from there and find another party. we are not voting you because we love you, we have our spouses and families to love. we are giving you assignments to accomplish i.e. deliver for the people
 
Back
Top Bottom