Waziri Nchemba: Utoaji risiti za kielektroniki imekuwa kama punguzo la bei, mteja asipopewa risiti anapunguziwa bei

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
754
3,097
"Matumizi ya mashine za kielekroniki kwa ajili ya kodi na kutoa risiti bado imekuwa ni changamoto kwa wananchi, kwasasa utoaji wa risiti umekuwa kama punguzo la bei manake mtu asipopewa risiti anapunguziwa bei tofauti na akidai risiti jambo ambalo linasababisha bidhaa nyingi kuuzwa nje na bei inayofahamika na TRA na hapa nataka niwakumbushe watanzania kuwa suala la kodi sio la TRA peke yake ni jambo la watanzania wote"

kwepa kodi uwezavyo

index.jpg
 
Hakuna mtanzania asietamani kulipa kodi na sio kodi tu hata ingekuwa kuchangia bajeti yetu kwa hela za mfukoni tungechangia, shida ni matumizi mabovu ya pesa za kodi, ufujaji na wizi wa viongozi wetu, ndio hapo unapoona kulipa kodi ni ujinga, kitu cha laki 3, akikwambia na risiti 350000 bila risiti 300000, unaona hii 50000 bora niwanunulie kuku na basmati nyumbani watoto wafurahie.

Serikali inapaswa ibadilike(japo najua haiwezi badilika)
 
"Matumizi ya mashine za kielekroniki kwa ajili ya kodi na kutoa risiti bado imekuwa ni changamoto kwa wananchi, kwasasa utoaji wa risiti umekuwa kama punguzo la bei manake mtu asipopewa risiti anapunguziwa bei tofauti na akidai risiti jambo ambalo linasababisha bidhaa nyingi kuuzwa nje na bei inayofahamika na TRA na hapa nataka niwakumbushe watanzania kuwa suala la kodi sio la TRA peke yake ni jambo la watanzania wote"

View attachment 2918088
Matumizi ya kodi zetu yanatuvunja sana moyo kuendelea kuwajibika kuzilipa. Sasa hivi wananchi wakipata upenyo wa kukwepa watakwepa tu. Viongozi wapunguze matumizi ya anasa na ubadhilifu.
 
Serikalini hakuna usiriaz kwenye matumizi.

Matumizi makubwa kwenye magari ya anasa ni sababu pekee miongoni mwa nyingi zinazonichochea kukwepa Kodi.

Watumishi wa wilayani akiwemo DC watumie magari chini ya cc2000, isipokuwa polisi wao waendelee na mashine zenye kifua kipana!

Ni big 6 pekee ndo wapewe vxr
 
Mmehamasisha matumizi ya cash kwa kuweka tozo za kipumbavu kwenye miamala ya kieletronic, vuneni matunda ya upumbavu wenu na huyo waziri weny wa fedha asiye na maono.
mpumbavu mamako, kuna tozo gani sahivi, ulitaka usichangie maendeleo ya nchi. Ukiona vyaelea vimeundwa we bwege
 
Mmehamasisha matumizi ya cash kwa kuweka tozo za kipumbavu kwenye miamala ya kieletronic, vuneni matunda ya upumbavu wenu na huyo waziri weny wa fedha asiye na maono.
Wakitaka cashless systems waondoe kodi na tozo zao.
Wameshtuka kwa sasa bank kwenda bank ni 2000 kwa malipo chini ya 10mil

Kwenye hizi Mpesa waondoe kodi haswa VAT na makato mengine ili tupambane kati ya benki na hizo mobile
 
Ukiingia dukani kununua bidhaa, tegemea yafuatayo:
1. Majadiliano ya bei ya bidhaa unayoitaka
2. Aina ya risiti unayoitaka
3. Ukitaka risiti ya Nchi utapata bidhaa hiyo kwa bei ya moto
4. Ukitaka risiti ya kawaida utapata bidhaa hiyo kwa bei iliyopoa.
 
Tukwepe kodi kadri tuwezavyo
Mtazame jinsi anavyosoma karatasi...hakuna element yoyote kwamba yupo serious.
Hayo mambo anayosoma hivi kweli kabisa kwa mtu mwenye PHD anahitaji kukodolea macho mstari kwa mstari?...vitu obvious ambavyo vinajulikana...
 
"Matumizi ya mashine za kielekroniki kwa ajili ya kodi na kutoa risiti bado imekuwa ni changamoto kwa wananchi, kwasasa utoaji wa risiti umekuwa kama punguzo la bei manake mtu asipopewa risiti anapunguziwa bei tofauti na akidai risiti jambo ambalo linasababisha bidhaa nyingi kuuzwa nje na bei inayofahamika na TRA na hapa nataka niwakumbushe watanzania kuwa suala la kodi sio la TRA peke yake ni jambo la watanzania wote"

View attachment 2918088
Serikali nzima inatumia vibaya kodi zetu, mkikusanya mnapanga safari za nje zisizokuwa na manufaa kwa taifa tena mnakwenda kwa mamia na machawa. Bora anayeweza kukwepa kodi afanye hivyo kwa ari mpya na kasi mpya.
 
Wakati wa Magu tulianza kabisa kuridhia kuomba risti na kuwa na furaha kulipia kodi sababu tulikuwa tunaona matumizi ya kodi zetu, tunapewa mipango ya nchi, mikakati ya nchi, tunapewa update za hatua za kila mradi ulipofikia.

Kwa sasa ukiuliza unaambiwa hamia burundi, sasa anaehamia unatakaje kodi yake tena
 
Back
Top Bottom