Dk Manyaunyau ajisalimisha kwa Yesu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Manyaunyau ajisalimisha kwa Yesu

Discussion in 'Celebrities Forum' started by eRRy, Dec 10, 2009.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Aliyekuwa mganga wa kienyeji, Jongo Salum, maarufu kwa jina la Dokta Manyaunyau amesababisha watu kupigwa na butwaa, baada ya kujitokeza hadharani na kutangaza azma yake ya kumpa Bwana Yesu maisha yake Jumapili iliyopita.

  Azma yake hiyo aliitangaza kwenye mkutano mkubwa wa Injili ulioandaliwa na Soul Winners Ministry International (SWMI), uliofanyika kwenye viwanja vya Yombo Matankini jijini Dar es salaam, muda mchache baada ya mganga huyo kukwama katika jaribu lake la kuharibu mkutano huo kwa njia za kishirikina

  …..akishuhudia umati wa watu, uliowachukua muda mrefu kuamini kama kweli aliyekuwa anazungumza na kukabidhi maisha yake kwa Yesu alikuwa Manyaunyau, mwenyewe alisema amekuwa akifanya uharibifu mkubwa katika kuzalisha migogoro katika ndoa za wakristo, ikiwa ni pamoja na kuvunja uchumba kabla ya ndoa.

  Alisema kwa siku hiyo alikuwa anakusudia kuharibu nguvu ya mkutano huo, lakini alijikuta akikwama na hivyo kujikuta akishawishika kuacha kazi hiyo na kuamini kwamba Yesu ni kiboko.

  …….Baada ya shuhuda zake na kuutangazia umma kuwa sasa ameamua kuokoka, aliruhusu watumishi wa Mungu wafike nyumbani kwake kwa ajili ya kuchoma moto zana (tunguli) zote ambazo alikuwa akijivunia katika biashara yake ya kuzimu.

  Kwa jijini Dar es salaam, dokta Manyaunyau amekuwa akifanya kazi ya uganga wa kienyeji kwa uaminifu mkubwa kutoka kwa wateja wake, kwani hadi alipokuwa anatangaza kuokoka, tayari amefika kiwango cha utajiri wa kumiliki mali mbalimbali, yakiwemo magari ya daladala, ambapo haijafahamika mara moja kama atayafanya nini baada ya kuanzisha maisha hayo mapya ndani ya Kristo.

  Miongoni mwa mambo aliyokuwa akiyafanya kwa wateja wake ni kuchangisha fedha katika mitaa mbalimbali, ili kutoa wachawi mitaani, jambo lililompatia umaarufu mkubwa kutoka kwa wateja wake, maana wanadai aliimudu vilivyo kazi hiyo. Mojawapo ya mambo ya kipekee aliyokuwa akifanya mganga huyo wa kienyeji ni kuwakata shingo paka kwa meno na kunywa damu zao hadharani.​

  Source: http://strictlygospel.wordpress.com/2009/10/19/mganga-wa-kienyeji-ajisalimisha-kwa-yesu-dk-manyaunyau/
  All Glory To God Jehovah!
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Stunt 101
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,997
  Trophy Points: 280
  HAKUNA MtU ATAYEWEZA KUNIFUATABILA KUVUTWA NA BABA ALIYENITUMA
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Jina la YESU lihimidiwe! Na kila goti lita pigwa kwa JINA LA YESU. Amen
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Dec 10, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Kweli kila goti litapigwa kwa jina lake yeye pekee...jina lake lihimidiwe na sifa na shukrani zinarudishwa kwake pekee anaestahili kuabudiwa.........
   
 6. D

  Dear Member

  #6
  Dec 10, 2009
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Asante yesu,asante yesu,asante yesu
   
 7. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #7
  Dec 10, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Kwake yeye kila GOTI litapigwa!!!
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Dec 10, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,999
  Trophy Points: 280
  sifa na utukufu ni kwako mwokozi
   
 9. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #9
  Dec 10, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii khabari ni njema saaana,
  Jamaa ametoka kwa shetwani amemfuata Mungu wa kweli,
   
 10. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #10
  Dec 10, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mungu ni mwema sana, anataka watu wote wairudie toba ya kweli kupitia Jina lipitalo majina yote, Yesu Kristo!
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  To God be the glory for the things He has done.
   
 12. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Huyu alikuwa tapeli, na amesha kusanya ngawira za kutosha! Sasa anmeamua kuzuga watu kwamba ameokoka.
  Lakini si watu wote walitajao jina la bwana wata fika Mbinguni..!
   
 13. Mkanya

  Mkanya JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 600
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wengi tu watajisalimisha..... bado maana wengine wanadai kuwa hawawezi kuelewa
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  6Yesu akawaambia, ``Mimi ndiye Njia na Kweli na Uzima; mtu hawezi kufika kwa Baba bila kupitia kwangu. 7Kama mngekuwa mnajua mimi ni nani, mngemfahamu na Baba yangu. Tangu sasa mnamfahamu Baba yangu na mmemwona.''
   
 15. P

  Preacher JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakika yesu ni bwana, mwokozi, muweza wa yote.

  Kwake "hakuna jambo lililo gumu"
   
 16. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  There is none like God!
   
 17. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,937
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Kwa jina la YESU kila goti litapigwa na kila ulimi kukiri ya kuwa YESU NI BWANA.Amen
   
 18. Ngorunde

  Ngorunde JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 17, 2006
  Messages: 1,122
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Na yote hayo yamefanyika ili wote waliokuwa wanamfuata huyo mganga waelewe hakuna msaada kwa mwanadamu awaye yote bali kwa Mungu. ...ili litimie neno lililoandikwa, " Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu kuwa kinga yake"
   
 19. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo. tuendelee kueneza injili kwa maneno na matendo yetu. ina la Bwana lihimidiwe!
   
 20. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwa yesu kila goti litapigwa na kila ulimi utakiri kwamba yesu ni bwana
  asante yesu
   
Loading...