Dk Manyaunyau ajisalimisha kwa Yesu

PYTHEME122309.jpg
 
Manyaunyau anatengeneza movie nyingine,,ili aendelee kupiga pesa zaidi mtaani,,siku hizi waganga wanamtumia mola baadala ya shetani
 
Watanzania tatizo letu tunapenda kuonewa huruma, huyu mtu hajawahi kuwa mganga zaidi ya kutapeli watu kazi yake kubwa ilikuwa fundi uhashi aliiacha baada ya kugundua kuwa kuna pesa kuwa mganga na akawa anatumia watu kwa lugha yao wanawaita mavise, hapo amesema uongo mwingine ili kutengeneza pesa let's wait tuone mwisho wa movie hiyo itakuwaje maana hata wakati anaanza uganga niliwambia watu tusubiri tuone itakuwaje
 
Wakristo kwa kuamini porojo kiboko,

Naona wengi hapa jf wanasherehekea bila kujiuliza kilichomfanya Manyaunyau kuacha ugang, ni kwa sababu ameuelewa ukristol au nimazuazua aliyo yaona kwa kipindi kile?

Sitoshangaa baadae akaukana na huo ukristo kwa sababu kaingia sio kwa kuujua, kujifunza bali kwa mauzauza aliyo yaona, mauzauza hayo yanaweza kuwa yamesababishwa na uchawi/uganga umemrudia, matatizo ya akili au utapeli aliouandaa ili kujichotea mapesa kwa wafuasi mbumbumbu wasio hoji, kwa sababu kwao ukihoji unaonekana unamapepo.
 
Jina lako litukuzwe yeye aliye juu ambaye kwaye Yesu alizaliwa kwetu na utukufu wake unazidi kudhihirika kizazi hadi kizazi.
 
Bwana Yesu asifiwe sana...Ama kweli Bwana kama wewe ungehesabu maovu yetu, nani angesimama mbele zako...

Lakini kwako Bwana kuna msamaha Mungu wa Israeli!..
Nguvu za Mungu ziko hapa jioni ya leo...! Ameeen!
 
damu ya yesu ni uhai-walawi 11:15
wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo yesu kristo- ufunuo 12:11
Hakuna jina lipitalo majina yote zaidi ya jina ka YESU ALIE HAI
 
Back
Top Bottom