Dk. Kitila Mkumbo ajitambulisha rasmi ACT

Dk. Kitila Mkumbo ajitambulisha rasmi ACT

HUU ndio uungwana kama unataka kuanzisha chama hata cha mashoga, siasa au hata footboli anzisha tu. Lakini tabia ya kutumiwa na TISS kutaka kuhujumu vyama vya ukombozi wa watanzania huku uko ndani tena kiongozi haivumiliki. Lakini mjue cdm ndio iliwafanya muonekane mna maana!
 
Wakati akihojiwa na radio clouse fm asubuhi kada huyo wa chadema zamani,amesema anamtaka zitto ajiunge na act ili akagombee uwenyekiti katika chama chao kwakua ana akili nyingi sana;je wanachama wengine hawana akili? Je kwanini asiwakaribishe kugombea wanachama wote,je kwanini zitto wakati anajua yupo chadema?je hiyo ndio demokrasia waliyo isema haipo chadema?kwanini uwe na timu utegemee wachezaji wa timu pinzani?wana jamvi kumbukeni wapo wasomi wengi walijifanya wajuaji waka anzisha vyama mwisho wakafulia wao na vyama vyao wakapotea katika ramani ya siasa tz,karibuni act tz ila acheni majungu chadema ni mwalimu wenu mtake msitake,kuche kuchwe

Hapo ndipo wanapotudanganya.....

Zito ajiunge vipi wakati yeye ndie muhasisi wa ACT?
Na ukiongea offline na yeye mwenyewe anakili hilo, na hata kitila nae anakili hilo mkikutana, hawa jamaa wanamfichaficha kuna kitu wakiogopa
 
Dk. Kitila Mkumbo amejitambulisha rasmi kuwa ni mwanachama wa ACT kupitia Clouds fm leo asubuhi amesema atamshauri Zitto aje kugombea uwenyekiti.

==============

JamiiForums imefanikiwa kumtafuta Dr. Kilila Mkumbo kuthibitisha habari hii. Amekiri kuongena na Clouds FM na kwamba yeye ni Mwanachama wa Alliance for Change and Transparency (ACT).
Dr Kitila na Zitto Kabwe sio tu ni wanachama wa ACT bali wao ndio Waasisi na Financier wa ACT toka waliposhtukiwa Chadema. Wapo pia akina Mchange, na huenda hata Dr Bashiru wa UDSM naye yumo. Ndio maana unasikia hata Wasomi wanaiunga mkono ACT. Nawatakia kila la heri iwapo kuwapo kwao kutasaidia kuwaondoa CCM madarakani, lakini kama kuja kwao ni kujaribu kuwavuruga CHADEMA kwa manufaa ya CCM hawatafanikiwa.
 
At last kelele zitaisha CDM,na makala zake pia zitaacha kuiponda CDM. Na ndoto zake za kugombea ubunge kwa Mwigulu zimerejea,ingawa kupitia ACT atashindwa kirahisi

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Maskini weee kwa hiyo demokrasia ya Kitila ni ya kutaka mtu amtakaye awe mwenyekiti mwenyekiti wa muda LImbu Malaya wa kisiasa ADC amemuachia nani tangu CCM,UDP,TLP,CUF a mwisho ACT LImbu anasema ana demokrasia ipi

yule TAPELI WA KARIAKOO sijui atafanya kazi gani aisee ?
 
Salama ya Chadema ni kuimarisha UKAWA,na ngazi ya ACT kuwa chama kikuu cha upinzani ni kufa kwa UKAWA. Kwa hali ilivyo sasa Chadema bila UKAWA ni kifo kwake.Naamini Chadema itaiendeleza UKAWA ata ikibidi kwa kuviua vyama wanachama na kutoka na UKAWA rasmi kama kundi lisilotengashika.
 
Adc act sijui ccm jumlisha na vyama vingine unavyovijua ukiwaunganisha bado mziki wa cdm hawauwezi
 
Sheria haimruhusu kabisa Kittlya kuwa mwanasiasa na wakat anatumikia umma kama mwalim, lakin kwakuwa wao waliomtuma ndio serikar utasikia hili!!

Inategemea unadefine vip uanasiasa...ila sharia inaruhusu mfanyakazi wa serikali kuwa mwanachama wa chama cha siasa.Na Kitila sio kiongozi bali mwanachama wa kawaida.
 
Lakini Zitto kwa maneno yake alisema atakuwa wa mwisho kuondoka CHADEMA.

Umeona eeh! Sasa hiyo ni kuonyesha huyu kijana sio mkweli. Maana kusema atakuwa wa mwisho kuondoka it means ni mpaka chama kife au kufutwa. Sasa mbona ameshiriki uanzishwaji wa chama kingine wakati issue yake ya uanachama aliyopeleka mahakamani haijaisha?


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom