Dk. Kitila Mkumbo ajitambulisha rasmi ACT

Dk. Kitila Mkumbo ajitambulisha rasmi ACT

Kwa sababu bado hatujapata chama mbadala KARIBUNI nawatakia kila la heri. Msiwe wasanii kama jina la chama chenu lilivyo. ACT. pigeni kazi huenda mkawa chama mbadala siku za usoni.
 
Lakini Zitto kwa maneno yake alisema atakuwa wa mwisho kuondoka CHADEMA.

Hata Juliana Shonza alitamka kuwa yeye bado makamu Mwenyekiti BAVICHA na mwisho wa siku tukamuona kakumbatiwa na Mwenyekiti wa CCM taifa akitambulishwa kuwa amejiunga CCM kwa hiyo tambua hizo huwa ni kauli za kutapatapa.
 
Akiongea leo kwenye redio ya mawingu fm, Dr kitila amesema Mh Zitto Kabwe ni mmwanasiasa maarufu na mwenye akili nyingi na ni watu wajinga tu ndiyo watamuacha kwenye vyama vyao. Amesema atafanya kila njia ili ajiunge nao kwenye chama kipya kitakacholeta upinzani wa kweli kilichopata usajili wa kudumu hivi karibuni. :A S 39:

ni kweli kabisa zito ni maarufu kwa sababu ya uzandiki na unafiki mkuu alo nao.Ni mtu hatari kuliko intarahamwe
 
waasisi wa ACT ni watatu tu - Zitto, Mkumbo na Mwigamba!!

Hiki ni chama kilichoasisiwa mahsusi kupunguza kura za CDM 2015 ili CCM ipate ahueni - nyie mtaona kama kitapigwa hata bomu moja kwenye mikutano yake!!

Waache wapunguze kura za CDM; ni swala la muda tu; lakini wajue ni lazima kuna siku kura hizo zitatosha na mabadiliko kuelekea Tanzania tuipendayo yatakuwa sio hadithi tena wala ndoto. A reality.
 
Mwajiri wa Kitila Mkumbo anasemaje juu ya hili?

Sheria haimruhusu kabisa Kittlya kuwa mwanasiasa na wakat anatumikia umma kama mwalim, lakin kwakuwa wao waliomtuma ndio serikar utasikia hili!!
 
Kwani lazima Zitto awe mwenyekiti!? Ina maana kitila anawaona wanachama wengine hawana akili ya kuongoza hicho chama lazima awe zitto!? Msomi wa ajabu kabisa huyu na amewatukana sana wanachama wa hiki chama!
 
Akiongea leo kwenye redio ya mawingu fm, Dr kitila amesema Mh Zitto Kabwe ni mmwanasiasa maarufu na mwenye akili nyingi na ni watu wajinga tu ndiyo watamuacha kwenye vyama vyao. Amesema atafanya kila njia ili ajiunge nao kwenye chama kipya kitakacholeta upinzani wa kweli kilichopata usajili wa kudumu hivi karibuni. :A S 39:

Yes nilimsikia pia,ila cha kushangaza sijui kwa nini aliogopa kufunguka kwamba Zitto ni mwananchama wa A.C.T kwasababu kwa kila alichokuwa anasema ilikuwa wazi kabisa Zitto ni mwanachama,anyway that is non of our business we hope they will come and fight to remove CCM,but not to weakerning the oppossition as that will not help the common mwananchi
 
Chadema walikurupuka bila kupima upepo. Sasa kuna wabunge 24 wa chadema wanaomuunga mkono Zitto watafuata nyayo ikiwa jamaa ataondoka CDM.

Una maana hao wabunge 24 walipewa ubunge na Zito kwa hiyo hata wakiondoka Chadema atawarudisha bungeni?
 
Mwajiri wa Kitila Mkumbo anasemaje juu ya hili?

Tatizo kwa waajiriwa Serikalini ni kuwa Viongozi au wananchama wa CHADEMA hapo ndio sheria uchukua mkondo wake lakini unapokuwa mwanachama wa vyama vingine hakuna tatizo lolote.
 
Huyu anatafuta gia ya kuinadi ACT. Sijui kwanini wanajiita Alliance for Change and Transparency wakati wenyewe wanajifichaficha. Dr. Kitila, mh. Zitto siyo dini inayohitaji kuabudiwa, Tanzania tunahitaji kiongozi muadilifu na wenye matendo yaliyonyooka ili watanzania tumwamini na kumpa dhamana.

Kwa hiyo muadilifu ni Mbowe na dr. Slaa
 
Kutengeneza combination ya Mbowe & Slaa (katika mazingira ya chama (CCM) kushika hatamu) inaweza kugharimu miaka mingine 20......
 
Chadema walikurupuka bila kupima upepo. Sasa kuna wabunge 24 wa chadema wanaomuunga mkono Zitto watafuata nyayo ikiwa jamaa ataondoka CDM.

Hao wabunge walipata ubunge kwa watu kuwapigia kura kwa kuchagua CHAMA (CHADEMA) na sio mtu kwa hiyo wakiondoka hawana nafasi ya Kushinda tena Ubunge kwani ZITTO hana uwezo wa kunadi wagombea na hana hizo sifa na ndio maana katika Jimbo lake madiwani wa CHADEMA wamepungua kila msimu baada ya yeye kuwa Mbunge tofauti na kabla ajaingia kuchukua nafasi hiyo.
 
Wakuu frema120 na kibogo nimewaelewa vyema sasa ya kuwa; CCM na ACT ni kama JUMA na ROZA vile, ya kwamba Kitila Mkumbo hatochukuliwa hatua kwa kujiingiza katika siasa akiwa ni mtumishi wa umma!
 
ACT tunapambana na changamoto zinazoikabili taifa. Hatuna mapambano na chama chochote

Hangaika na dunia wewe. Sisi lengo ni moja tu. Kipunguza kura za CDM na hii kazi tumetumwa.
Kwa idhini ya Serikali ya CCM tunafanya kazi hii kwa lengo moja TU.
Tunalipwa hela ndefu siyo bure wewe. Hatuna shughuli yoyote ile na mwananchi wala nchi hii ya Tanzania. Tukimaliza shughuli yetu baasi tunazugazuga tu huku tukiendelea kuvuta fungu(matunda yenu ya nchi) na kutafuna tartiiiiibu

Tuko makini
 
Back
Top Bottom