Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 137
- 179
Mantiki ya kisiasa inaonyesha Dkt. Hussein Mwinyi ana weledi, busara na nidhamu za kuulinda muungano bila nongwa yoyote, aidha ni mwaminifu na myenyekevu anayeshauriwa na kusikiliza, kwa sifa hizo anastahili kupewa nchi kupitia sanduku la kura hapo Oktoba 28, Wanazanzibari kwa umoja wenu mchagueni Dk. Mwinyi aendeleze na kudumisha misingi ya Mwl. Nyerere na Karume ya kuona Muungano unastawi na kuwa bora zaidi, Aidha Dkt. Mwinyi anauchungu na Muungano na anajua dhamani yake, kuliko viongozi wengineo wanao omba ridhaa ya kupewa kiti cha urais.
Muungano upo salama mikononi mwa Dkt. Mwinyi endapo mtampa ridhaa ya kuwatumikia, lakini Muungano upo mashakani endapo kura atapewa kiongozi yoyote yule zaidi ya Mwinyi, ni rai ya andiko hili kuwaombeni wana wapendwa wa Zanzibar kumchagueni Dkt. Mwinyi hili Muungano, Amani, Maendeleo na uchumi wa watu na vitu viboreshwe zaidi, aidha tumuamini, tumtume na kumuombea kwa maslahi ya taifa la Zanzibar.
Dkt. Hussein Mwinyi anao uwezo, nia, upeo na utayari wa kuwatumikia wanazanzibari kuliko mgombea yoyote yule kwa sasa ndani ya visiwa vya Zanzibar, hivyo imani ya kuiona Zanzibar mpya itawale vichwani mwetu na tutambue ipo njiani, ni imani ya andika hilo kuwa ubora wa Dkt. Hussein Mwinyi utamfanya ashinde kiti cha urais dhidi ya Bwana Maalim Seif Shariff Hamad, Bila shaka hata bwana Maalim analitambua hilo kutokana na upekee wa sifa alizo nazo Dkt. Hussein Mwinyi, Myonge myongeni lakini haki yake mpeni.