mbona jamaa mwenyewe ameshakwisha hivyo.......nikijumlisha 3years naona atakuwa anakimbilia kwenye mkongojo...sidhani kama ataweza hata kufikiri kwa umakini vitu sensitive atakuwa kama shati lililopo sasa hivi, ni kukenua tuuuuuuuuuuu.
Unawakumbuka Wade na Mwai Kibaki? Wade bado anapiga jalamba pamoja na umri wake.mbona jamaa mwenyewe ameshakwisha hivyo.......nikijumlisha 3years naona atakuwa anakimbilia kwenye mkongojo...sidhani kama ataweza hata kufikiri kwa umakini vitu sensitive atakuwa kama shati lililopo sasa hivi, ni kukenua tuuuuuuuuuuu.
Wanajamii;
Kwa wafuatiliaji wa habari bila ya shaka watakua wamegundua kuwa Makamu Wa Rais Mh. Dk Bilali kwa kipindi kirefu sasa amekuwa katika ziara za kikazi mikoani na wilayani na kupewa kipau mbele katika media za Tanzania. Ziara hizi kwa mtazamo wa haraka japokuwa ni za kikazi lakini zimekuwa ni nyingi sana zaidi ya kiongozi mwingine yoyote wa Kisiasa.
Ikumbukwe kuwa Dr. Bilali ni Makamu wa Rais na anafanya zile kazi ambazo Rais amemwagiza au yuko aware nazo.
Yawezekana kabisa kuwa Rais Kikwete ameamua kuchukua uamuzi huo wa kumuandaa na kumtangaza Bilali awe mgombea Urais wa CCM 2015 ili kukinusuru chama chake CCM kutokana na makundi ambayo itake isitake 2015 yatakimega CCM kabisa kwa asilia 100%. Huenda akawa na sababu nyingi lakini chache ni zifuatazo:
- Safari hii ni zamu ya Wazanzibar kutoa Rais. Kumbuka hii ni hoja rahisi kama walivyoamua kuwa safari hii Spika ni Mwanamke na hivyo kumweka Sita pembeni. K
- Dk. Bilali hana Makundi na amekuwepo katika siasa za Bara na Visiwani na anakubalika (Of course ziara za sasa zimam-promote)
- Dk. Bilali amekuwa Makamu wa Rais na anakubalika kama Presidential Material
- Ili kuzima chokochoko za Wazanzibari kuua Muungano dawa ni kumweka Mzanzibar. JK hawezi kuruhusu Zanzibar iwe Nchi au Dola (Historically na Kikatiba).
- JK hataki aonekane kaivuruga Nchi ndo maana kwa mambo yote makubwa nchi hii kaamua bora tu akae kimya kuliko kusema. La kuhusu katiba ameona bora atofautiane na Chama chake ili kuacha Lergacy na kuleta utengamao katika Nchi.
Ni nini maoni yako binafsi kuhusu Dk. Bilali na harakati zake za kuzunguka mikoani na wilayani in connection na mbio za Urais 2015? Je yawezekana akawa ni Chaguo la JK?
Nawasilisha.
usiwe na fikra finyu namna hii angalia uwezo wa mtu usiangalie anakotoka, kwani huyu wa sasa hivi si anatoka kwenye population kubwa ya watu milion 40+ amefanyia taifa nini zaidi ya kuwa baba mlezi wa mafisadi?? Bilal kama hafai( na mimi naamini hivo) mtafutie sababu nyingine za kum disqualify lakini kabila dini au sehemu atokako mtu its not an issue here!!
Watu wa Ng'wanakitolyo watapewa kanga na kofia wakati ukifika na usisahau wakipewa wali nyama mambo saaaaafiiiiiiiiii!!!!!Hiyo point ya tatu: kwamba anakubalika kama presidential material ni very questionable. Anakubalika kwa nani? Nani kafanya utafiti na kuthibitisha kuwa hata kule Ng'wanakitolyo Bilal anakubalika?
Huyo mshikaji ni zombi kinyama, ziara zake zote huongozana na wake zake wawili. Nadhani anajifunza ziara bt sidhani kama atamrith jk.
Nilisikia TBC jana wanasema Makamu wa Rais alikuwa Rukwa huko ziarani akafika mahali barabara zikawa mbovu sana ikabidi wamletee helkopta ya polisi asafiri nayo. kwa kuwa yeye ni kiongozi na wao serikali yao ndio imetufikisha hapa angepaswa kusafiri kwa barabara kama walivyokuwa wamepanga aone shida za watu. Kukwepa na kuagiza helkopta iletwe ni usaliti na sii uongozi bora
Nilikuwa nataka nami nimwambie lakini basi. Mbona hoja imekaa vizuri. Mtoa mada umetoa changamoto nzuri tu, mtu badala ya kuchangia anaanza matusi. Hawa watu ndio wanaichafua JF. Kama mtu hana hoja si anyamaze tu. Kuna watu nadhani hawawezi hoja za kufikirisha wakiona tu kuna kugikiria kidogo tu basi anakimbilia matusi!
Hakuna tusi pale mkuu, ukiona hakuna ban jua hapo hakuna matusi. Ok, tuyaache hayo tuendelee na mada. Mi nadhani si kama JK anampa promo Bilal isipokuwa babu anatimiza tu majukumu ya umakamu wa rais. Ana nafasi kubwa nyuma ya rais hata hivyo hafai kuwa rais wa jamhuri. Kama ikiwa ni lazima rais atoke upande wa pili wa nchi. Nadhani Shein anayo nafasi kubwa zaidi kuliko Bilal.
Watachimbiwa visima na wawekezaji kwenye madini!Watu wa Ng'wanakitolyo watapewa kanga na kofia wakati ukifika na usisahau wakipewa wali nyama mambo saaaaafiiiiiiiiii!!!!!
Hakuna tusi pale mkuu, ukiona hakuna ban jua hapo hakuna matusi. Ok, tuyaache hayo tuendelee na mada. Mi nadhani si kama JK anampa promo Bilal isipokuwa babu anatimiza tu majukumu ya umakamu wa rais. Ana nafasi kubwa nyuma ya rais hata hivyo hafai kuwa rais wa jamhuri. Kama ikiwa ni lazima rais atoke upande wa pili wa nchi. Nadhani Shein anayo nafasi kubwa zaidi kuliko Bilal.