Makamu wa Rais Kupanda Helkopta Kutokana na Barabara mbovu ni Usaliti

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,543
550
Nilisikia TBC jana wanasema Makamu wa Rais alikuwa Rukwa huko ziarani akafika mahali barabara zikawa mbovu sana ikabidi wamletee helkopta ya polisi asafiri nayo. kwa kuwa yeye ni kiongozi na wao serikali yao ndio imetufikisha hapa angepaswa kusafiri kwa barabara kama walivyokuwa wamepanga aone shida za watu. Kukwepa na kuagiza helkopta iletwe ni usaliti na sii uongozi bora
 
Usaliti mkubwa sana, kwa kiongozi madhubuti angekataa kupanda chopper,angetaka apite nae ajionee maana nae ni binadamu kama wengine wanaoitumia kila siku-watoto,kina mama wajawazito,vikongwe nk
 
Helikopta hiyo iliagizwa toka wapi? Je! Ni kutoka Dar, Mbeya ama Dodoma?

Wanashindama kuifilisi nchi?
 
Angekuwa ana tumia helkopta kila siku yeye na boss wake,inge punguza gharama
na foleni barabarani.
 
Labda ana shida na afya!
Na kama helcopter itakuwa imetoka dsm sasa ilo wese mpaka kule!
No wonder serikali inahaha haina ela
 
To be honest huwa ninakasirika kila ninapomwona huyu mzee na hizi zaira zake. Hivi haswa zina tija kwa taifa? Juzi nimeona anatembelea shamba la waziri mkuu Pinda. hivi kweli of all the problems we have leo hii kiongozi wa nafas yake na msafara wake ndio kazi wanazofanya?????? Wananchi tunalalamika maisha yamekuwa magumu ila wao wanashindana kuitafuna nchi. Hizo kazi za kukata utepe hata mkuu wa wilaya si anaweza kuzifanya tukapunguza gharama. No wonder it is said siku hizi huenda huwa anatembea na mkasi na ribbon kabisa just in case akikutana na jengo la kukatia utepe asipate tabu!!!!!!!!!!!!!!
 
Amepangiwa kazi na mkweree kuwa atakuwa anafanya safari za ndani ya nchi tu na yeye mkweree atafanya safari za majuu basi; kwahiyo msimshangae ndio majukumu aliyopangiwa!!
 
ni usaliti ulio wazi maana kwa kuwa wao ni viongozi hawastahili kupata shida tunazopata wananchi we unafiliri ni kwa vp watapata uthubutu wa kutatua shida zetu wakati wao hawaonji chungu ya shida zetu?
 
na atalipwa mafao eti alikuwa kazini na sherehe ya kustaafu muda ukifika ,,,,lakini namuona kama mgonjwa au muda umeenda sana kama ana 85 years......vile
 
Mzee wa mkasi na utepe,
hana lolote babu,huwa nauzika sana hawa wazee wanvyofanya anasa kuzunguka kwa mambo yasiyo na tija,
siku mkipata ajali ndio mtajifunza
 
Back
Top Bottom