Mshume Kiyate
JF-Expert Member
- Feb 27, 2011
- 6,766
- 894
Diwani wa kata ya Mabogini. Moshi Vijijini, Albert Msando (Chadema) jana alikuwa kivutio mahakamani baada ya kujitokeza na kumtetea Diwani wa Kata ya Machame wilayani Hai, Rajab Nkya (CCM) anayeshitakiwa kwa uhujumu uchumi.
Katika baadhi ya maeneo mkoani Kilimanjaro, ni nadra kwa mfuasi wa Chadema kumtetea mwenzake wa CCM, kufuatia uhasama wa kisiasa uliopo. Msando ni wakili wa kujitegemea na miongoni mwa mawakili wanaoitetea Chadema na wafuasi wake katika kesi mbalimbali.
Diwani huyo ndiye ambaye CCM inamnyooshea kidole kuwa aliihujumu katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai na kuiwezesha Chadema kuchukuwa nafasi hiyo, Hata hivyo yeye binafsi, mara kadhaa amekanusha madai hayo.
Msando ndiye anayemtetea Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe katika kesi kuhusu tuhuma za kumpiga makofi, Nassir Othman wakati wa kupiga na kuhesabu kura.
Source: Mwananchi Aprili 30, 2011