Diwani wa Chadema Albert Msando amtetea wa CCM Rajab Nkya kortini

Dude!.........Kwa hiyo Msando aligombea Udiwani kupitia CDM ili apate ulaji mbali na fani yake ya Uwakili!...........halafu ukiwa Diwani wa CDM hivyo wewe unawakilisha CDM tu..............hizo societies za huko Marekani (especially Tea Parties za GoP) zimekuathiri mazee...........

Mangi, hebu nambie nani kwenye Congress ya Marekani ambaye ni ana practice law wakati huo huo akiwa congressman au congresswoman?
 
NyaniNgabu,

Siasa unayofanya wewe mimi sifanyi. Kwanza perception hazinilazimishi kufanya au kutokufanya uamuzi fulani. Endapo nitaruhusu 'wanachofikiri' watu kufanya maamuzi nitakuwa najikosea pamoja na jamii inayonizunguka.

Tuna tatizo. Wengi wanaangalia zaidi jamii inaona nini badala ya kufanya kile ambacho ni HAKI. Huo ni unafiki.

Rostam ana HAKI ya kutetewa. Msingi mmoja wa Katiba ni 'innocent until proven guilty'. Huwezi kuupinga msingi huo hata kama ni Rostam au Lowassa. Ingekuwa inawezekana basi wangekuwa jela.

Tusiwe na siasa za unafiki. Tusiogope kusimamia maamuzi ya HAKI kisa watu wataonaje.

Kuhusu uwakili na udiwani, vinaenda pamoja. Ukisema eti niache moja nibaki na moja unakosea. Kama itabidi tufanye hivyo basi wengi tutakuwa nje ya siasa....kuna msemo sikumbuki ni MwanaJF gani anautumia...'siasa isiachwe kwa watu fulani pekee...'

dah! kumbe watu hawamtendei haki kiongozi wanapomshambulia alivyowanadi kina mramba!
 
Mfuatiliaji, am humbled. Kilichotokea kwa nionavyo mimi ni uonevu kwa Rajab Nkya kisa eti anatuhumiwa alimpigia kura Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai ambaye ni wa CDM. Hata kama alipiga ni haki yake na lazima iheshimiwe. Kuja kumuundia kesi sio sawa. Ni uonevu! Mambo kama haya tuyapinge bila kujali itikadi. Wapo watu wengi wanabambikiziwa kesi kwa sababu za kisiasa.
 
Husninyo,

Niseme hivi, Rajab Nkya sio fisadi. Naamini hivyo. Tuhuma dhidi yake ni za kisiasa kama zilivyo za Mh. Mbowe, Dr. Slaa, Lema na wengineo.

Sio kwamba sielewi mkanganyiko unaoweza kuwepo. Nililaumiwa sana kumfungulia kesi Mh. Grace na Lucy Owenya kutaka tafsiri ya mahakama kuhusu uhalali wa Mbune wa Viti Maalumu kuingia kwenye Halmashauri kisa tu anafanya kazi kwenye Halmashauri hiyo.

Atakayenihukumu kwa hilo anakosea. Jukumu langu kama wakili na diwani ni kutetea HAKI. Sio HAKI ya Chadema pekee, ni HAKI ya mtu yeyote anayestahili kutendewa HAKI. Maoni ya jumla yasituzuie kusimamia yale tunayoaamini.

Being a CHADEMA councilor/ activist and at the same time being a full time legal practitioner who represents a broad range of clients does undercut your credibility.

Kama unataka kuwa mtetezi wa haki pasipo kuonekana mnafiki basi achana na huo udiwani. Fanya uwakili wako kwenye hivyo vimahakama vyenu na hakuna atakayekuhoji motives zako.
 
Chadema kama kweli wapo makini wasiwape hawo mawakili nafasi za uongozi katika chama chao, wabakie kama wanachama wa kawaida, mimi naona kama mchezo wa kuigiza wanafanya Chadema wanazunguka nchi nzima wanafanya maandamano huku wanataja orodha ya MAFISADI, cha kuchekesha MAFISADI wakifishwa mahakamani hao hao viongozi wa Chadema mawakili wanachukuwa pesa za MAFISADI wanawatetea mahakamani kuwa hawa sio MAFISADI, hizi ndio siasa za Tanzania utapeli mtupu

cdm wachunge sana wananchi wasijesema hii kutaji orodha ya mafisadi ni
njia ya kuwatafutia wanasheria wao ulaji (tenda)
 
cdm wachunge sana wananchi wasijesema hii kutaji orodha ya mafisadi ni
njia ya kuwatafutia wanasheria wao ulaji (tenda)

These CHADEMA lawyers are driven by mercenary motives. They will do anything for money and say anything to get elected.

Imekula kwetu hiyo. Msitegemee miujiza toka kwa hao watu. They could very well be worse than CCM.
 
Busara hii ingeingia ndani ya bunge letu, hasa kwa wabunge wa ccm, ingeleta mvuto na heshima kwa wananchi.
Kutetea Haki bila kujali ni Chama gani kimeleta hoja husika.
 
Husninyo,

Niseme hivi, Rajab Nkya sio fisadi. Naamini hivyo. Tuhuma dhidi yake ni za kisiasa kama zilivyo za Mh. Mbowe, Dr. Slaa, Lema na wengineo.

Sio kwamba sielewi mkanganyiko unaoweza kuwepo. Nililaumiwa sana kumfungulia kesi Mh. Grace na Lucy Owenya kutaka tafsiri ya mahakama kuhusu uhalali wa Mbune wa Viti Maalumu kuingia kwenye Halmashauri kisa tu anafanya kazi kwenye Halmashauri hiyo.

Atakayenihukumu kwa hilo anakosea. Jukumu langu kama wakili na diwani ni kutetea HAKI. Sio HAKI ya Chadema pekee, ni HAKI ya mtu yeyote anayestahili kutendewa HAKI. Maoni ya jumla yasituzuie kusimamia yale tunayoaamini.

umeeleweka msando.
Kama unaamini hana kosa una haki ya kutetea.
 
Sifanyi chcochote kwa ajili ya fedha. Ingekuwa rahisi kufanya chochote kama ningegombea kupitia CCM! Kuwa diwani kwa tiketi ya CDM na bado kuendelea kuwa wakili ni vizuri ukajiuliza!

Kusema niache uwakili na kubaki diwani inaonyesha hujui unachoongelea. Sifa mojawapo ya Diwani kwa mujibu wa sheria ni kuwa na kipato halali. Sasa nikiacha kuwa wakili kipato halali napata wapi? Hilo hulioni!
 
Heheheheheheeeee sasa nimekuelewa Bw. Msando. Mke na wana lazima wale. Asante kwa kuwa mkweli.
 
Ni kweli Nyani Ngabu lazima wale. Lakini watakula halali. Njaa ni kitu kibaya sana. Viongozi wengi wanageuza siasa kazi. Njia ya kupata kipato. Leo hii kwa posho ya 120,000 kwa mwezi unategemea mtu akiwekewa ofa mezani ili atoe tenda ataacha? Hizi 10% unafikiri ni nini? Njaa na tamaa!
 
Kwa hiyo mie kama ni mhandisi rostam akinipa kazi ya kihandisi nisifanye? Mie nitafanya sana
je kama mimi ni daktari na hao mafisadi wamekuja kwangu kwa ajili ya matibabu nifanyaje, nisiwatibu? is it not unethical,immoral and unproffesional
 
mkuu msando usitudanganye hawa hata sisi law tunaijua na tunaifanyia kaz..eti unatetea haki?..naomba nikukumbushe the concept of techinicalities of law b4 the court of law haki inanunuliwa the more you hire a good advocate possibility ya ushindi wa kesi inakuwa kubwa sasa nenda kawadanganye ma laymen ktk kata yako na sio hapa
 
Back
Top Bottom