Diwani wa Chadema Albert Msando amtetea wa CCM Rajab Nkya kortini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani wa Chadema Albert Msando amtetea wa CCM Rajab Nkya kortini

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mshume Kiyate, Apr 30, 2011.

 1. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Diwani wa kata ya Mabogini. Moshi Vijijini, Albert Msando (Chadema) jana alikuwa kivutio mahakamani baada ya kujitokeza na kumtetea Diwani wa Kata ya Machame wilayani Hai, Rajab Nkya (CCM) anayeshitakiwa kwa uhujumu uchumi.

  Katika baadhi ya maeneo mkoani Kilimanjaro, ni nadra kwa mfuasi wa Chadema kumtetea mwenzake wa CCM, kufuatia uhasama wa kisiasa uliopo. Msando ni wakili wa kujitegemea na miongoni mwa mawakili wanaoitetea Chadema na wafuasi wake katika kesi mbalimbali.

  Diwani huyo ndiye ambaye CCM inamnyooshea kidole kuwa aliihujumu katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai na kuiwezesha Chadema kuchukuwa nafasi hiyo, Hata hivyo yeye binafsi, mara kadhaa amekanusha madai hayo.

  Msando ndiye anayemtetea Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe katika kesi kuhusu tuhuma za kumpiga makofi, Nassir Othman wakati wa kupiga na kuhesabu kura.

  Source: Mwananchi Aprili 30, 2011
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Albert Msando. Unatekeleza kazi/wito wako wako wa kitaaluma ipasavyo
   
 3. h

  hoyce JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Si ajabu. Hata Marando yuko chadema akipambana na ufisadi, lakini kama wakili anawatetea watuhumiwa wa ufisadi wa EPA
   
 4. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 483
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  gud siasa ni kupingana kwa hoja si uhasama tunawzhitaji sana wenye uelewa kama msando..keep going mh
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kweli Tanzania shamba la wajinga, Watu wanafanya ufisadi mkubwa kwenye idara za serikali, Halmashauri, wanaingia mikataba mibovu Taifa linapata hasara ya mabilioni ya pesa, wanafikishwa mahakamani kwa makosa yao cha kushangaza watokea Mawakili ambao ni viongozi wa chama kikuu cha upinzani Chadema ambao wameapa kupambana na mafisadi wa nchi hii, wanawatetea bila aibu hawo mafisadi wakiulizwa wanasema eti uwakili ni taaluma wapo kazini hakuna kosa lolote kuwatetea mafisadi mahakamani, sito shangaa siku mmoja kumuona Rostam Azizi akitetewa na Msando, au Marando na Prof Safari
   
 6. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Kwenye maisha kuna uhasama na chochote kinaweza kufanyika.Maoni yangu binafsi ni kwamba,kama ningekuwa mwanasheria ningefanya hivyo hivyo lakini nikigundua kwamba ni kweli mtuhumiwa kafanya kosa hilo la ufisadi nitajitoa kwa kuwa hata dhamira njema itanibana.Hayo ndiyo mawazo yangu
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Huju jamaa kama sikosei jana alikuwa Arusha..kwenye ile kesi ya viongozi na wanachama wa CDM...
   
 8. S

  Sio Mwanasiasa Senior Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kaka usiite watu wajinga wakati wewe huonyeshi uerevu wako..katiba ya nchi hii inataka mahakama ndio imtie mtu
  Hatian na c hisia au maneno ya magazeti yamfanye mtu ana makosa..sasa ikitokea wakili amepata mteja ambaye kwa mujibu wa maelezo ya huyo mteja wakili anaona wazi kua huyu c mkosaji kwann asimtetee?..me nadhan tunapaswa kufaham kua kila mtu anapaswa kupata haki yake ikiwemo hiyo ya kutetewa na kusikilizwa..kwan hujawah kusikia watu wansingiziwa kesi,so kwak wewe inatosha sana kama flan akisemwa mwizi afthn akamatwe na kutiwa ndan
   
 9. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, angalia vizuri bandiko langu sijamuita mtu mjinga nimetumia lugha ya kawaida kutokana nchi yetu ilivyo, naona unaleta porojo kama za JK, kwa hiyo Dk Slaa alivyotaja orodha ya mafisidi kafanya makosa kwa mtazamo wako wewe, kuna ushahidi wa kimazingira unatosha kujua mtu kama fisadi, waziri ana dola milioni moja benki kaweka ulaya unasubiri mahakama ikuambie, unataka kutuambia mpaka sasa Tanzania hakuna mafisadi
   
 10. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo mie kama ni mhandisi rostam akinipa kazi ya kihandisi nisifanye? Mie nitafanya sana
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Saturday, 30 April 2011 09:44

  Daniel Mjema, Hai

  DIWANI wa Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini, Albert Msando (Chadema) jana alikuwa kivutio mahakamani baada ya kujitokeza na kumtetea Diwani wa Kata ya Machame wilayani Hai, Rajab Nkya (CCM) anayeshitakiwa kwa uhujumu uchumi.

  Katika baadhi ya maeneo mkoani Kilimanjaro, ni nadra kwa mfuasi wa Chadema kumtetea mwenzake wa CCM, kufuatia uhasama wa kisiasa uliopo. Msando ni wakili wa kujitegemea na miongoni mwa mawakili wanaoitetea Chadema na wafuasi wake katika kesi mbalimbali.

  Diwani huyo ndiye ambaye CCM inamnyooshea kidole kuwa aliihujumu katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai na kuiwezesha Chadema kuchukua nafasi hiyo.

  Hata hivyo yeye binafsi, mara kadhaa amekanusha madai hayo.Wakili huyo ndiye anayemtetea pia Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Justine Salakana ambaye amekwama kulipa Sh10 milioni za dhamana.

  Msando ndiye anayemtetea Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe katika kesi kuhusu tuhuma za kumpiga makofi, Nassir Othman wakati wa kupiga na kuhesabu kura wilayani Hai, katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

  Kesi hiyo nayo ilitajwa jana katika mahakama ya Wilaya ya Hai, lakini iliahirishwa kwa kuwa Mbowe hakwenda mahakamani kwa sababu alikuwa na udhuru.

  Jana Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai (Chadema) alikuwa asomewe maelezo ya awali katika kesi hiyo.Kesi ya diwani huyo wa CCM anayeshtakiwa pamoja na wenzake wawili ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Denis Mpelembwa.

  Hata hivyo iliahirishwa hadi Mei 5 mwaka huu.
  Mapema, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Anneth Mavika, aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba ipange siku ya kuwasomea watuhumiwa maelezo ya awali.

  Diwani Nkya ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Nkuu, anashtakiwa pamoja na Katibu wa chama hicho, Esther Shoo na mfanyabiashara Awadhi Lema.

  Mfanyabiashara huyo anakabiliwa na tuhuma za kukiuuzia chama hicho, trekta lililochakaa.
  Inadaiwa kuwa kati ya Machi na Oktoba mwaka 2007, washtakiwa walikisababishia chama hicho hasara ya Sh38 milioni kwa kununua trekta hilo.

  Takukuru ilidai kuwa kitendo kilichofanywa na washitakiwa hao ni matumizi mabaya ya ofisi.
   
 12. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kwa suala la haki hatuangalii chama wala dini bali kuona haki inatendekea, huyu wakili ni mwanaJF mwenzetu na kajiandika majina yake hayo hayo na huwa anapost makala nyingi tu humu na pia ni classmet wangu tukiwa chuoni na mpiganaji wa siku nyingi ktk masualaya siasa tangu chuoni.
   
 13. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  bila kusahau ni mwanaJF mwenzetu,
  anatekeleza dhana ya haki kuona inatendeka,
  haki haina dini wala siasa bali ionekanake wazi inatendeka.
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Apr 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Katika uwanja wa maoni ya watu ni vigumu kuwaelewa hao mawakili ambao ni wanachama wa CHADEMA (ambao inasadikika kuwa ni anti-ufisadi) kuwatetea watuhumiwa wa ufisadi mahakamani. Hata kama kitaaluma wako ndani ya maadili na miiko yao, lakini bado kisiasa wataonekana kama ni wazushi zushi na wanafiki flani hivi. Hiyo tupende tusipende, ndivyo ilivyo na ndivyo itakavyokuwa.

  Chukulia huu mfano, mimi ni civil rights lawyer halafu nakubali kumwakilisha a self-avowed white supremacists katika kesi yake ya kumdunda binti wa kiafrika ambapo jamaa anatuhumiwa kumpiga huyo binti huku akitoa matusi na kejeli kuhusiana na rangi yake ya ngozi.

  Kikazi na kitaaluma nitakuwa niko sawa kabisa. Lakini mbele ya macho ya wengi nitaonekana kama mtu wa ajabu. Civil rights lawyer anaenda kusimama kizimbani kumtetea mbaguzi wa rangi tena yule ambaye haufichi ubaguzi wake? Hahahahahaaaa.....ni ngumu sana kueleweka hapo.
   
 15. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakuna tatizo lolote kwa Mbunge wa CHADEMA kumtetea mbunge wa CCM kama kuna haki na hata mbunge wa CCM anaweza kumtetea mbunge wa CHADEMA kama kuna haki.
   
 16. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  nashangaa kwa nini watu wanashindwa kuelewa mambo madogo kama haya!
  CDM inatetea haki na usawa pamoja na kupinga ufisadi!! kama mtu amesingiziwa ufisadi ni haki mfuasi wa CDM kumtetea mtu huyo.
  kwa habari zilizopo zinaonyesha prof MAHALU ameshitakiwa kwa visa vingine nje ya ufisadi ila ufisadi umetumika kama kigezo tu,je Marando au Msando akimtetea ni kosa????Mengi na akina Manji mi naona ni walewale tu ndo maana Mengi anaiogopa sana serikali kwa kuwa anaijua na serikali inamjua vilivyo pa kumbana. ugomvi walionao na Manji ni wa kibiashara zaidi na sio siasa na uadilifu,sioni shida kwa Marando kumtetea mmoja wao especially kwenye mahakama hizi za kwetu ambazo maamuzi ya kesi yanafanyika kwingine ila hukumu ndo inasomewa kwenye kichumba cha mahakama.....
  kwa sasa kuna watu wengi wamesingiziwa ufujaji wa mali kwa kuwa tu walikuwa wanaunga mkono mabadiliko wakati wa uchaguzi....wilayani makete nimeambiwa makatibu kata wapatao wa5 wamesimamishwa kazi kazi kwa maelekezo ya vikao vya chama cha magamba...Msando akiwatetea atakuwa anakoosea???jibu ni HAPANA..
  keep it up Msando ila tetea haki na haki itakulinda.
   
 17. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hayo ni mambo ya taaluma hivyo siasa ni lazima iwekwe pembeni
   
 18. Jagermaster

  Jagermaster JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 656
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa CCM inamtuhumu huyo diwani kuwa aliihuju na kupoteza nafasi ya Uenyekiti Hai, na Msando kama diwani wa CDM yuko right, kwani The enemy of my enemy is my friend
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Apr 30, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Whether we like it or not, the court of public opinion has different standards than the court(s) of law. And that's the conundrum that some lawyers face.

  For these CHADEMA lawyers to defend/represent CCM members who are accused of UFISADI and at the same time sing anti-ufisadi songs, that simply doesn't cut it with some people. And in a way it undercuts their credibility and sincerity. It makes them look two-faced.
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  na niya mtu binafsi...
   
Loading...