Diwani wa CHADEMA Muheza atimkia CCM. Akoshwa na kasi ya Maendeleo ya Rais Samia

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727
Wakati Chadema ikiendelea kujifariji Kwa kusema inaenda kuiondoa CCM madarakani 2025,Diwani wa kata ya Kata ya Mkuzi huko Muheza bwana George Chamabai amekihama chama hicho na kutimkia CCM.

CCM wao wamemkaribisha na kusema mtoto mkaidi amerudia nyumbani Kwazazi wake.

My Take
Chadema Maigizo ya Kusema Wanaccm Wamerudisha kadi sijui Wameandika Mabango Hayatawasaidia.

Mnajidanganya na kucheka wenyewe,ona Sasa mnavyoumbuka.

---
Diwani.png

Diwani wa Kata ya Mkuzi Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, George Chambai kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amejiunga rasmi na Chama cha Mapinduzi CCM leo Jumapili Septemba 10, 2023.

Ametangaza kuachana na chama chake cha zamani wakati wa Mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika viwanja vya Sokoni Mkuzi nakuhudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abrahaman na Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma maarufu ‘Mwana FA’ na viongozi wengine wa chama na Serikali.

Chambai amesema kuwa hakushawishiwa na mtu yeyote katika uwamuzi wake, bali amefanya hivyo baada ya kuridhishwa na kasi ya maendeleo inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan.

"Nimehama kwa mapenzi yangu, siasa siyo chuki wala ugomvi, tunataka watu wapate maendeleo ya haraka hivyo sikuwa na sababu ya kubaki upinzani,"amesema.

Akizungumza katika mkutano huo, mwenyekiti wa CCM Rajab Abrahaman amempongeza Diwani huyo kuamua kujiunga na chama cha mapinduzi na kwamba ameahidi watampa ushirikiano wa kutosha .

Mwenyekiti huyo ameongeza ifikapo mwakani wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, CCM mkoani Tanga haitafanya mzaha na kwamba watahakikisha inashinda nafasi zote za uongozi.

Ameongeza mkoa huo umejipanga kuhakikisha unaongoza kitaifa katika kumpa kura nyingi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati wa uchaguzi mkuu ujao, pia wanashinda kata zote 245, vijiji, vitongoji na Mitaa yote mkoani Tanga.

Chanzo: Mwananchiu
 
Back
Top Bottom