Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,226
- 113,575
Hayo ni mambo ya taaluma hivyo siasa ni lazima iwekwe pembeni
Basi wachague moja. Siasa full time au uwakili full time. Zaidi ya hapo utaonekana mtu usiyeeleweka.
Hayo ni mambo ya taaluma hivyo siasa ni lazima iwekwe pembeni
Kwa hiyo mie kama ni mhandisi rostam akinipa kazi ya kihandisi nisifanye? Mie nitafanya sana
Msando and the like are hypocrites..Kwenye majukwaa unapinga ufisadi kwa nguvu zote halafu unaingia mahakani kuutetea.
Saturday, 30 April 2011 09:44
Daniel Mjema, Hai
DIWANI wa Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini, Albert Msando (Chadema) jana alikuwa kivutio mahakamani baada ya kujitokeza na kumtetea Diwani wa Kata ya Machame wilayani Hai, Rajab Nkya (CCM) anayeshitakiwa kwa uhujumu uchumi.
Katika baadhi ya maeneo mkoani Kilimanjaro, ni nadra kwa mfuasi wa Chadema kumtetea mwenzake wa CCM, kufuatia uhasama wa kisiasa uliopo. Msando ni wakili wa kujitegemea na miongoni mwa mawakili wanaoitetea Chadema na wafuasi wake katika kesi mbalimbali.
Diwani huyo ndiye ambaye CCM inamnyooshea kidole kuwa aliihujumu katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai na kuiwezesha Chadema kuchukua nafasi hiyo.
Hata hivyo yeye binafsi, mara kadhaa amekanusha madai hayo.Wakili huyo ndiye anayemtetea pia Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Justine Salakana ambaye amekwama kulipa Sh10 milioni za dhamana.
Msando ndiye anayemtetea Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe katika kesi kuhusu tuhuma za kumpiga makofi, Nassir Othman wakati wa kupiga na kuhesabu kura wilayani Hai, katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.
Kesi hiyo nayo ilitajwa jana katika mahakama ya Wilaya ya Hai, lakini iliahirishwa kwa kuwa Mbowe hakwenda mahakamani kwa sababu alikuwa na udhuru.
Jana Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai (Chadema) alikuwa asomewe maelezo ya awali katika kesi hiyo.Kesi ya diwani huyo wa CCM anayeshtakiwa pamoja na wenzake wawili ilitajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Denis Mpelembwa.
Hata hivyo iliahirishwa hadi Mei 5 mwaka huu.
Mapema, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Anneth Mavika, aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba ipange siku ya kuwasomea watuhumiwa maelezo ya awali.
Diwani Nkya ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Nkuu, anashtakiwa pamoja na Katibu wa chama hicho, Esther Shoo na mfanyabiashara Awadhi Lema.
Mfanyabiashara huyo anakabiliwa na tuhuma za kukiuuzia chama hicho, trekta lililochakaa.
Inadaiwa kuwa kati ya Machi na Oktoba mwaka 2007, washtakiwa walikisababishia chama hicho hasara ya Sh38 milioni kwa kununua trekta hilo.
Takukuru ilidai kuwa kitendo kilichofanywa na washitakiwa hao ni matumizi mabaya ya ofisi.
mkuu, angalia vizuri bandiko langu sijamuita mtu mjinga nimetumia lugha ya kawaida kutokana nchi yetu ilivyo, naona unaleta porojo kama za jk, kwa hiyo dk slaa alivyotaja orodha ya mafisidi kafanya makosa kwa mtazamo wako wewe, kuna ushahidi wa kimazingira unatosha kujua mtu kama fisadi, waziri ana dola milioni moja benki kaweka ulaya unasubiri mahakama ikuambie, unataka kutuambia mpaka sasa tanzania hakuna mafisadi
jamvin kunaitaj maandaliz ya fikra na si kukurupuka
Kwenye maisha kuna uhasama na chochote kinaweza kufanyika.Maoni yangu binafsi ni kwamba,kama ningekuwa mwanasheria ningefanya hivyo hivyo lakini nikigundua kwamba ni kweli mtuhumiwa kafanya kosa hilo la ufisadi nitajitoa kwa kuwa hata dhamira njema itanibana.Hayo ndiyo mawazo yangu
WanaJF,
Ni kweli namtetea Rajab Nkya ambaye anashtakiwa kwa makosa mawili. Kuhujumu uchumi na kutumia madaraka vibaya. Mazingira ya kesi hiyo (bila kuathiri mwenendo wa kesi) yana utata.
Kwa muda mrefu diwani huyo amekuwa anashutumiwa kwamba aliuza kura yake Chadema na kwamba anashirikiana na viongozi wa chadema Hai kudhoofisha CCM. Kuna chuki na fitna nyingi zinaendelea dhidi yake. Hana msaada wowote kutoka kwenye chama chake.
Kwa kumtetea mtu anayetuhumiwa ni fisadi sio kwamba natetea ufisadi. Nikimtetea muuaji sio kwamba natetea watu kuua! Nikitetea kampuni isilipe kodi iliyokuwa assessed na TRA sio kwamba natetea watu wasilipe kodi.
Inawezekana mwungine asielewe kwanini namtetea Rajab Nkya, lakini kuna kila uwezekano anaonewa. Kama kweli amehujumu uchumi mahakama itaamua. Ninachotakiwa kutetea ni HAKI itendeke. Ni jukumu langu kama ilivyo jukumu langu kupinga ufisadi. Kama viongozi wa chadema wanaotuhumiwa kuandamana bila kibali na uchochozi wanaonewa kuna uwezekano pia Rajab Nkya anaonewa. Nitatenda HAKI bila kujali itikadi, dini, kabila wala kanda. Ni wajibu wangu kama kiongozi na wakali wa kujitegemea.

Ndiyo matatizo ya kuchanganya siasa na kazi. Kwani huwezi tu ukawa wakili wa kujitegemea bila kuwa mwanaharakati unayejihusisha na chama fulani cha kisiasa? Au huo udiwani wa CHADEMA hauna ulaji wa kutosha hivyo inabidi kuwa na side gig? Na hapo sasa sijui side gig ni ipi, udiwani au uwakili.....utajaza mwenyewe. Lakini habari ndo hiyo, kwenye siasa perception is reality. Watu wakishakuona wewe mzushi na mganga njaa hata kama si kweli, itaonekana ni kweli. It's just the nature of the beast. Na ndiyo maana kwenye litigious societies kama Marekani mawakili ni moja ya watu wanaochukiwa sana.
Rostam Aziz akija kununua huduma zako za uwakili kuhusiana na kutuhumiwa kwake na ufisadi utakubali kumwakilisha?
.................Tuna tatizo. Wengi wanaangalia zaidi jamii inaona nini badala ya kufanya kile ambacho ni HAKI. Huo ni unafiki.
...................Tusiwe na siasa za unafiki. Tusiogope kusimamia maamuzi ya HAKI kisa watu wataonaje...'
NyaniNgabu,
Siasa unayofanya wewe mimi sifanyi. Kwanza perception hazinilazimishi kufanya au kutokufanya uamuzi fulani. Endapo nitaruhusu 'wanachofikiri' watu kufanya maamuzi nitakuwa najikosea pamoja na jamii inayonizunguka.
Haki ni subjective kama ilivyo unafiki. Unachoona wewe ni haki mwingine anaona dhuluma. Tunachoona sisi kuwa ni unafiki wewe unaona ni ukweli. Such is life. Deal with it.Tuna tatizo. Wengi wanaangalia zaidi jamii inaona nini badala ya kufanya kile ambacho ni HAKI. Huo ni unafiki.
Hilo nalielewa vyema sana. Ila wewe kama huelewi concept ya court of public opinion nakushauri ukajinadi kwake ili upate kuwa wakili wake halafu 2015 ugombee ubunge kwa tiketi ya CHADEMA.Rostam ana HAKI ya kutetewa. Msingi mmoja wa Katiba ni 'innocent until proven guilty'. Huwezi kuupinga msingi huo hata kama ni Rostam au Lowassa. Ingekuwa inawezekana basi wangekuwa jela.
Then choose one; CHADEMA affiliated activist or an independent attorney. Being what you are now makes you look bad, makes you lose credibility in the fight your party is waging, and worst of it all it makes you look like a sleazeball attorney who will do anything for money unless you tell me you are representing that CCM guy pro bono.Tusiwe na siasa za unafiki. Tusiogope kusimamia maamuzi ya HAKI kisa watu wataonaje.
Kuhusu uwakili na udiwani, vinaenda pamoja. Ukisema eti niache moja nibaki na moja unakosea. Kama itabidi tufanye hivyo basi wengi tutakuwa nje ya siasa....kuna msemo sikumbuki ni MwanaJF gani anautumia...'siasa isiachwe kwa watu fulani pekee...'