Najisi ni kila kitu kinachofanya usiruhusiwe kusali mpaka uitoe hiyo najisi. Najisi ni uchafu kwa kifupi. Na uchafu upo wa aina nyingi. Kuna aina ya uchafu haulazimiki kuuondoa ili usali yaani uanweza kusali na uchafu wako hivyo hivyo na swala yako ikawa sawa. Kwa mfano wewe ni fundi makenika umechafuka oil kila mahali, lakini hiyo oil na nguo zako chafu za oil haikuzuii wewe kusali. Ukitaka kusali hivyo hivyo unaweza tu.
Lakini kuna aina ya uchafu ukiwa nao ni lazima uutoe kwanza ndio usali, huu ni mfano umeenda chooni ni lazima ujioshe na maji, hairuhusiwi kusali na mavi/mikojo hata ikiwa kwenye nguo utalazimika uoshe hiyo sehemu kwanza ndio usali.
Ndio hivyo hivyo upande wa wanyama kuna wanyama wengi ambao ukigusana nao hawana najisi mfano ngombe, mbuzi, paka, simba n.k ila kuna specific wametajwa kuna wana najisi ambao ni mbwa na nguruwe. Na hata hizo bacteria unazosema sio zote ni najisi
I hope nimekujibu swali langu na Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi zaidi