Maslahi yangu kiroho: mimi ni mshika dini kwa imani na dhehebu langu na nina hofu na Mungu
Dini ni njia buniwa ya mwanadamu ya kumtafuta Mungu iliyoshindwa vibaya kabisa; chochote afanyacho mwanadamu chini ya jua hakina ukamilifu wa kimungu kwakuwa mwanadamu mwenyewe si mkamilifu.
Ni katika kutengeneza huo mfumo uitwao dini binadamu anajikuta anajichanganya mwenyewe ama kutofautiana na mwenzake, ama kabila na kabila, imani na imani. Kufikia hapo ndio zikaanza kufumuka dini na imani za kila aina.
Wanaomtaja na kumwamini Mungu wakawa na dini zao nyingi tu lakini ndani yao wakipingana wenyewe kwa wenyewe. Walioona kwa Mungu hakuwatoshi nao wakaanzisha dini zao lakini nao hawakuishia pema, ni mitufuano tu. Kila dini sasa bila kujali ni ya kumtaja Mungu mmoja ama miungu wakawa na mitume na manabii wao. Na kila dini inawaheshimu na kuwatii sana sana.
Ni kupitia michakato hiyo ya kidini kujitangaza na kutaka kukubalika zaidi ndani ya jamii mbalimbali duniania. Dini imejikuta kwenye mtanziko mkubwa wa mambo mabaya kabisa duniani.
Ni kwa kupitia dini hizo mamilioni wamepoteza maisha yao kwa vita ya kidini ama kuuawa kwenye mabishano ya kidini.
Ni kupitia dini hizo watu kwa maelfu wamepotea na kupotezwa na wasionekane tena.
Ni kupitia dini hizo mamilioni ya watu duniani wamepitia madhila na mateso makubwa sana.
Ni kupitia dini hizo mamilioni ya watu duniani, wameteswa, wamenyanyaswa na kudhalilishwa kwa kiwango kisichomithilika
Dini badala ya kuwa suluhisho imegeuka kuwa jinamizi litishalo ndani ya jamii mbalimbali
Ushirikina haujawahi kufanya mambo mabaya hivyo kama yaliyofanya kwa kutumia dini, lakini ushirikina unatumiwa vibaya na wanadini kama pitio na kimbilio la kutupia lawama na mabaya yote kuficha madhaifu yao kwenye dini.
Inachekesha mno kiongozi wa dini anaposimama kwenye madhabahu na kuanza kukemea ushirikina kumbe jana yake tu alikuwa huko ama naye ni agent na muumini mwaminifu wa ushikirikina.. Viongozi wa dini zote hizi zinazoamini katika Mungu mmoja ndio kundi linaloongoza kwa kwenda kwa waganga wa kienyeji na ni waumini wakubwa wa ushirikina!
Kila nikipima haya mawili katika mizania ya haki bado USHIRIKINA una nafuu kubwa katika uhalisia wake kuliko hiki kitu kizuri kiitwacho dini!
Mkuu ungekuwa umefunga ningesema swaumu imekukalia vibaya 🤣 🤣 ila sasa najua wewe ni kobe mwenzangu.
kwenye mkanganyiko wa dini ya kikristo/kiislam hilo halina ubishi. Kwa waislam kuna madhehebu na pia kwa wakristo yapo ya kutosha
Wanahistoria wanatuambia kuna miaka wakatolik walijaribu kuthibiti walichoita uasi , walitumia nguvu zote kuzuia watu wasitoke kwao.
Katika nguvu hizo kuna watu waliuawa, wengi tu.
Tunapaswa kujua binadamu ni kiumbe huru na naamini Mungu aliacha tuwe huru. Kumfuata au kutokumfuata. lakini akatuonyesha na kitakachotupata tusipomfuata
Tangia vitoto vya kwanza vya Adam na Hawa vilikinzana, hadi kuuana. Hapa zilitengenezwa tawala mbili. Moja inatii maagizo ya Mungu na Nyingine inaona haina haja ya kutii maagizo ya Mungu
Hata hivyo pamoja na mkanganyiko bado njia ya kumuendea Mungu ni dhahiri na ya hakika
Mathayo 7:13-27 BHN
“Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba. Kwa maana njia inayoongoza kwenye maangamizi ni pana, na mlango wa kuingilia humo ni mpana; waendao njia hiyo ni wengi. Lakini njia inayoongoza kwenye uhai ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo. “Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili? La! Basi, mti mzuri huzaa matunda mazuri, na mti mbaya huzaa matunda mabaya. Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni. Kwa hiyo, mtawatambua kwa matendo yao. “Si kila aniambiaye, ‘Bwana, Bwana’, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza matakwa ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile ya hukumu: ‘Bwana, Bwana! Kwa jina lako tulitangaza ujumbe wako, na kwa jina lako tuliwatoa pepo na kufanya miujiza mingi’. Hapo nitawaambia: ‘Sikuwajua nyinyi kamwe; ondokeni mbele yangu, enyi watenda maovu.’ “Kwa hiyo, kila mtu anayeyasikia maneno yangu na kuyazingatia, anafanana na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo. Lakini haikuanguka kwa sababu ilikuwa imejengwa juu ya mwamba. “Lakini yeyote anayesikia maneno yangu haya bila kuyazingatia, anafanana na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. Mvua ikanyesha, mito ikafurika, pepo kali zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, nayo ikaanguka; tena anguko hilo lilikuwa kubwa.”
Kuhusu uchawi kusema kwamba ni afadhali kuliko dini, hapo hapana.
Watu wanaotoka sehemu zinazosifika kwa uchawi wanaelewa zaid madhara yake