Dini vs Ushirikina: Kwanini ningechagua ushirikina

Maslahi yangu kiroho: mimi ni mshika dini kwa imani na dhehebu langu na nina hofu na Mungu

Dini ni njia buniwa ya mwanadamu ya kumtafuta Mungu iliyoshindwa vibaya kabisa; chochote afanyacho mwanadamu chini ya jua hakina ukamilifu wa kimungu kwakuwa mwanadamu mwenyewe si mkamilifu.

Ni katika kutengeneza huo mfumo uitwao dini binadamu anajikuta anajichanganya mwenyewe ama kutofautiana na mwenzake, ama kabila na kabila, imani na imani. Kufikia hapo ndio zikaanza kufumuka dini na imani za kila aina.

Wanaomtaja na kumwamini Mungu wakawa na dini zao nyingi tu lakini ndani yao wakipingana wenyewe kwa wenyewe. Walioona kwa Mungu hakuwatoshi nao wakaanzisha dini zao lakini nao hawakuishia pema, ni mitufuano tu. Kila dini sasa bila kujali ni ya kumtaja Mungu mmoja ama miungu wakawa na mitume na manabii wao. Na kila dini inawaheshimu na kuwatii sana sana.

Ni kupitia michakato hiyo ya kidini kujitangaza na kutaka kukubalika zaidi ndani ya jamii mbalimbali duniania. Dini imejikuta kwenye mtanziko mkubwa wa mambo mabaya kabisa duniani.

Ni kwa kupitia dini hizo mamilioni wamepoteza maisha yao kwa vita ya kidini ama kuuawa kwenye mabishano ya kidini.

Ni kupitia dini hizo watu kwa maelfu wamepotea na kupotezwa na wasionekane tena.

Ni kupitia dini hizo mamilioni ya watu duniani wamepitia madhila na mateso makubwa sana.

Ni kupitia dini hizo mamilioni ya watu duniani, wameteswa, wamenyanyaswa na kudhalilishwa kwa kiwango kisichomithilika
Dini badala ya kuwa suluhisho imegeuka kuwa jinamizi litishalo ndani ya jamii mbalimbali

Ushirikina haujawahi kufanya mambo mabaya hivyo kama yaliyofanya kwa kutumia dini, lakini ushirikina unatumiwa vibaya na wanadini kama pitio na kimbilio la kutupia lawama na mabaya yote kuficha madhaifu yao kwenye dini.

Inachekesha mno kiongozi wa dini anaposimama kwenye madhabahu na kuanza kukemea ushirikina kumbe jana yake tu alikuwa huko ama naye ni agent na muumini mwaminifu wa ushikirikina.. Viongozi wa dini zote hizi zinazoamini katika Mungu mmoja ndio kundi linaloongoza kwa kwenda kwa waganga wa kienyeji na ni waumini wakubwa wa ushirikina!

Kila nikipima haya mawili katika mizania ya haki bado USHIRIKINA una nafuu kubwa katika uhalisia wake kuliko hiki kitu kizuri kiitwacho dini!
Mie bhana kinachonishangaza kwenye dini kuwa unaambiwa usiende kwa waganga wkt dini yenyewe ni imani kama ilivyo kumuamini mganga na kwa bahati nzuri unakuta mganga pia anakwambia mtegemee mungu utafanikiwa hicho kitu au una kuta mtu unateseka na gonjwa la kupewa mda mrefu alf mwisho wa siku wew utumie njia ya kifizikia kulitibu hlo gonjwa wkt daktari anakwambia haoni tatzo.
 
Pengine kuna kitu unahitaji kusikia kutoka kwangu na hukipati au nakuwa mfinyu wa kukuelewa ndio maana
Si kweli ila maswali ninayo kuuliza ni mepesi sana na yako wazi mno,hili unataka mpaka ubanwe sana ndiyo uje kujibu,kama ulivyokuja kujibu maana ya Uchawi na hukuweza kuitetea ipasavyo.

Nimekuuliza swali nini Ushirikina na historia yake ilianza vipi,kadhalika dini ni nini na utupe ushahidi wa kile ulichodai kwamba dini zimetungwa na watu nw nikakutaka utoe mifano hili hujalifanya.

Sasa ombi langu ni ujibu maswali niliyo kuuliza.
 
Sioni logic yako hapa; kama viongozi wa dini ndio wanaoongoza kwenda kwenye ushirikina na unawalaumu kwa hilo unafikiri kipi kibaya zaidi dini au ushirikina?

Pia usisahau kuwa ushirikina ni dini ya watu.

Tenganisha dini kama institution na dini kama imani.

Binafsi najua ubaya wa kuwa mwanadini bila kuwa na imani nzuri au ucha Mungu lakini kamwe ushirikina sio afadhali ukilinganisha na dini.

Jua kwamba kwenye ushirikina ndio matendo makuu ya shetani hufanywa kama kuua n.k.

Usiwaaminishe watu eti ushirikina ni jambo jema labda kama wewe ni agent wa mfumo huu wa shetani.
 
In terms of mambo mabaya kwa wakati mmoja na yaliyoangamiza watu wengi kwa mara moja uchawi unasubiri mbele ya dini
Tumeshuhudia si mara moja au mbili vita vya kidini vilivyoondoka na roho za malaki wasio na hatia... Je ni wapi umewahi kusikia ushirikina ukiuwa kwa halaiki?
Huenda uchawi unafanya mauaji zaidi ya dini. Tatizo hakuna ushahidi, mambo yao hayaonekani kwa macho ya kawaida.
 
Ila ni bora uamini kile unachokiamini kuliko kukaa bila kuamini chocote maana umeona hata mwamba mmoja amesema Korea Kusini hawana Dini lakini wanaishi freshi tu, hata Japan wengi wao hawana dini wengine ni Budha lakini maisha yao wako freshi tu, kimsingi imani ni suala binafsi sana na inahitaji kuelewa sana unachokiamini otherwise unaweza kuwa tisted sana na kuishia kuhangaika tu huku na huko bila kujielewa. Ukiamua kuwa na dini kuwa na dini yako ambayo ni personal wala haina maana kuishadidia na kuwafanya wengine wasioamini kuwa hawana maana. Ukiamua pia kuwa traditionalist ruksa ili mradi tu ni personal haiathiri wengine.
 
Si kweli ila maswali ninayo kuuliza ni mepesi sana na yako wazi mno,hili unataka mpaka ubanwe sana ndiyo uje kujibu,kama ulivyokuja kujibu maana ya Uchawi na hukuweza kuitetea ipasavyo.

Nimekuuliza swali nini Ushirikina na historia yake ilianza vipi,kadhalika dini ni nini na utupe ushahidi wa kile ulichodai kwamba dini zimetungwa na watu nw nikakutaka utoe mifano hili hujalifanya.

Sasa ombi langu ni ujibu maswali niliyo kuuliza.
Naomba nifanye hivyo alfajiri akili ikiwa fresh kwasasa nitapiga danadana tuu
 
Sioni logic yako hapa; kama viongozi wa dini ndio wanaoongoza kwenda kwenye ushirikina na unawalaumu kwa hilo unafikiri kipi kibaya zaidi dini au ushirikina?

Pia usisahau kuwa ushirikina ni dini ya watu.

Tenganisha dini kama institution na dini kama imani.

Binafsi najua ubaya wa kuwa mwanadini bila kuwa na imani nzuri au ucha Mungu lakini kamwe ushirikina sio afadhali ukilinganisha na dini.

Jua kwamba kwenye ushirikina ndio matendo makuu ya shetani hufanywa kama kuua n.k.

Usiwaaminishe watu eti ushirikina ni jambo jema labda kama wewe ni agent wa mfumo huu wa shetani.
Hapana fazili sijamwaminisha mtu wala kumlazimisha mtu kuamini nimeweka mada kwa mtazamo wangu ili tujadili kwa pamoja
 
Kuamini ushirikina kuwa una faida zaidi kuliko dini ni
Mshananistic ideology...we need to rethink beyond our cognitive
Ushirikina ni jina lililopewa imani zetu ili kuzitweza tu

Huwa inaniuma kwanini nachofikiri mimi kuna mtu hafikiri? Halafu unakuta ni msomi kabisa, inawezekana hivi elimu walileta ni ili kutupumbaza zaidi

Maana haiingii akilini jinsi jamii zinavyoelimika ndivyo ujinga unavyozidi
 
Huenda uchawi unafanya mauaji zaidi ya dini. Tatizo hakuna ushahidi, mambo yao hayaonekani kwa macho ya kawaida.
Wakati wa maalbino kuuliwa na kukatwa viungo sauti zilipazwa sana..hivyo ushahidi hauwezi kukosekana
 
Mie bhana kinachonishangaza kwenye dini kuwa unaambiwa usiende kwa waganga wkt dini yenyewe ni imani kama ilivyo kumuamini mganga na kwa bahati nzuri unakuta mganga pia anakwambia mtegemee mungu utafanikiwa hicho kitu au una kuta mtu unateseka na gonjwa la kupewa mda mrefu alf mwisho wa siku wew utumie njia ya kifizikia kulitibu hlo gonjwa wkt daktari anakwambia haoni tatzo.
Ukweli ambao hata Mshana ataukubali ni kwamba mambo yako hivi:

1.Viumbe wote wameumbwa kutoka kwenye SUPREME POWER AMBAYE NDIYE wengi wetu TUNAMUITA MUNGU.

2.MWANADAMU anayeishi sehemu yake muhimu na kubwa Zaidi INAITWA ROHO.

3.ROHO ZOTE hizo ni derivative ya ROHO MOJA KUU-Roho wa Mungu.

4.ROHO ZOTE zina GODLY INTELLIGENCE.
Zina ELIMU yote ya mambo yaliyoko na yaliyopita.

5.Ndani ya ubinadamu kuna uwezo wa kutafsiri mambo kutoka JUMBE ZA KIROHO.

Tafsiri nyingi zinapelekwa kwenye desk top ambayo ni UBONGO.

Ubongo hauna uwezo wa kutafsiri taarifa za Roho hata kwa nafasi ya moja ya million.

6.kutokana na uwezo mdogo wa akili(Brain),ndiposa kunatokea mchanganyiko wa habari.

Witchery is one of the poorest interpretations.

Deepest meditation through which the soul gets communicated so well,we call it PRECISE PRAYERS.

DINI nyingine especially CHRISTIAN WANA ROHO MTAKATIFU.

Actually Huyu yuko kwa kila mtu.

Tatizo ni KUJITAMBUA.

na

KUMTAMBUA na

KUWASILIANA NAYE.

Organized religions zimeharibu ukweli huu kwa kuwa wamamgeuza MUNGU kuwa BABA MKALI.
BABA MWENYE HASIRA.
BABA MWENYE GHADHABU...

Wameumba sura ya Mungu asiyekwepo.
Mungu wa kuchonga.

Kwa ab

Mungu ni UPENDO NA UPENDO NI MUNGU.

Kila kilicho kinyume na hilo ni uwongo......

Etc
Etc
Etc
 
Wakati wa maalbino kuuliwa na kukatwa viungo sauti zilipazwa sana..hivyo ushahidi hauwezi kukosekana
Sawa,ni sehemu ya unyama unaofanywa na wachawi. Je unaweza kujua usiku wa leo wachawi wamewaua watoto na watu wazima wangapi? Kuna mimba elfu kadhaa zimeharibika kwa sababu ya uchawi,kuna watoto,watu wazima na wazee kibao wameuliwa na wachawi kupitia magonjwa ya kutengenezwa.

Kuna ajali za barabarani,majini na angani. Kote huko mamia kwa maelfu ya watu wamechukuliwa kichawi kwa ajali za kutengeneza. Tatizo ya wachawi mambo yao ni ya gizani sana ndio maana tunaona km wana unafuu.
 
Ninacho amini Mimi dini ni utamaduni,,na kila jamii ya watu Ina utamaduni wao na namna yao ya kumuabudu Mungu...Bible ni habari za wayahudi na dini yao,mwokozi na kila Wanachoamini,,uislam waarabu,uhindi, Buddha and so...wazungu na waarabu wametufanya tuone dini zetu,tamaduni zetu,,si lolote si chochote,Ila vyao wao ndio vya maana tuvishike,,sio utumwa huu???dini zililetwa kwao ndio zikaja kwetu??kabla ya wao hatukua na dini???..wazee wetu waliambiwa na Nani kua kuna Muumba??
 
Back
Top Bottom