Mkuu ngoja nipate nafasi nzuuri Kisha nieleze tofauti ya vitu hivi VITATU.FAIDA NA HASARA ZAKEKaribu mkuu, shusha vitu
Mkuu kuna utofautiHapana ushirikina ndio mkusanyiko wa hivyo vyote
AhsanteKaribu...!
Una maswali mengi.Kuna wale wanaoji-protect dhidi ya uizi especially wa pesa, chuma ulete, position ofisini na vitu kama hivyo. Hawa wanaangukia wapi?
Sawa mkuu nitafanya hivyo.Una maswali mengi.
Hebu nifollow.
huwa natoa darasa la mambo ya kiroho siku moja moja.
Inshort mimi binafsi hizi ndio sabàbu kuu zinazonifanya niishikirie haswa imani yangu katika Yesu kristo.
1. Kufika mbinguni sio point ya kwanza hiyo ni faida ambayo nitaipata pindi maisha ya duniani yaki katika. Yani baadae kabisa muda bado.
2. Hekima za kimungu, nazihitaji sanaaa yani ili kufanya maamuzi mbalimbali, kutenda haki, kulinda mwili wangu, kupata mke atakae nifaa na vingine vingi
3. Nguvu za kiroho: yani hakuna mshirikina ninao muogopa wala kunitisha kwa lolote.
4. Sijui kama nitakua tajiri sana au la lakini huakika ni napata chakula kilicho kiasi changu, mavazi, nakula na bata ndogo ndogo vizuri tu naburudisha mwili kidogo kwa minyo.
5. Roho yangu ina amani sana, (amani rohoni ).
Awayajui maandiko Mungu ujipigania mwenyewe haitaji msaada wa mwanadamuKwa wakiristo Mungu hapiganiwi dini sababu biblia inatamka vita ni ya Bwana sio mwanadamu Istael walimshinda farao na jeshi lake bila kurusha hata jiwe au kofi.Wasio na Mungu ndio utasikia napigania mwenyezi Mungu
Ni madhara ya uchawi? Kudumaa kiakili? Recently kuna familia moja huko Morogoro wametembea uchi sababu ya haya mambo ya ushirikina. Is that what you support?Kuhusu uchawi kusema kwamba ni afadhali kuliko dini, hapo hapana.
Watu wanaotoka sehemu zinazosifika kwa uchawi wanaelewa zaid madhara yake![]()
I never said so!Ni madhara ya uchawi? Kudumaa kiakili? Recently kuna familia moja huko Morogoro wametembea uchi sababu ya haya mambo ya ushirikina. Is that what you support?
Kweli usemacho si fununu tu,Sawa mkuu nitafanya hivyo.
Nakubaliana na wewe ukiishi katika Kristo unapata amani ya kweli kwani utaridhika na kila ulichonacho na upatacho kwa kutumia nguvu zako kwa michakato halali
Tamaa, hofu, matatizo na shida humshawishi mtu kuacha njia. Uvumilivu katika Kristo unawashinda wengi
Lakini jambo hili ni kubwa zaidi, kuna fununu kuwa hata nchi inaongozwa kishirikina mfano mbio za mwenge ( http://https://jamii.app/JFUserGuide/archive/index.php/t-8986.html) na mambo mengine
Ushirikina pia ni dini, ni namna ya kuabudu. Watu wengi wameuwa kwa imani za kishirikina. Albino wasio na hatia, watoto wadogo, wazee. Kwa kifupi hakuna afadhali. Ushirikina unasababisha uishi kama umekufa vile, yaani maisha ya tabu na mateso. Kwa kifupi imani ni udhaifu mkubwa wa binadamu.Maslahi yangu kiroho: mimi ni mshika dini kwa imani na dhehebu langu na nina hofu na Mungu
Dini ni njia buniwa ya mwanadamu ya kumtafuta Mungu iliyoshindwa vibaya kabisa; chochote afanyacho mwanadamu chini ya jua hakina ukamilifu wa kimungu kwakuwa mwanadamu mwenyewe si mkamilifu.
Ni katika kutengeneza huo mfumo uitwao dini binadamu anajikuta anajichanganya mwenyewe ama kutofautiana na mwenzake, ama kabila na kabila, imani na imani. Kufikia hapo ndio zikaanza kufumuka dini na imani za kila aina.
Wanaomtaja na kumwamini Mungu wakawa na dini zao nyingi tu lakini ndani yao wakipingana wenyewe kwa wenyewe. Walioona kwa Mungu hakuwatoshi nao wakaanzisha dini zao lakini nao hawakuishia pema, ni mitufuano tu. Kila dini sasa bila kujali ni ya kumtaja Mungu mmoja ama miungu wakawa na mitume na manabii wao. Na kila dini inawaheshimu na kuwatii sana sana.
Ni kupitia michakato hiyo ya kidini kujitangaza na kutaka kukubalika zaidi ndani ya jamii mbalimbali duniania. Dini imejikuta kwenye mtanziko mkubwa wa mambo mabaya kabisa duniani.
Ni kwa kupitia dini hizo mamilioni wamepoteza maisha yao kwa vita ya kidini ama kuuawa kwenye mabishano ya kidini.
Ni kupitia dini hizo watu kwa maelfu wamepotea na kupotezwa na wasionekane tena.
Ni kupitia dini hizo mamilioni ya watu duniani wamepitia madhila na mateso makubwa sana.
Ni kupitia dini hizo mamilioni ya watu duniani, wameteswa, wamenyanyaswa na kudhalilishwa kwa kiwango kisichomithilika
Dini badala ya kuwa suluhisho imegeuka kuwa jinamizi litishalo ndani ya jamii mbalimbali
Ushirikina haujawahi kufanya mambo mabaya hivyo kama yaliyofanya kwa kutumia dini, lakini ushirikina unatumiwa vibaya na wanadini kama pitio na kimbilio la kutupia lawama na mabaya yote kuficha madhaifu yao kwenye dini.
Inachekesha mno kiongozi wa dini anaposimama kwenye madhabahu na kuanza kukemea ushirikina kumbe jana yake tu alikuwa huko ama naye ni agent na muumini mwaminifu wa ushikirikina.. Viongozi wa dini zote hizi zinazoamini katika Mungu mmoja ndio kundi linaloongoza kwa kwenda kwa waganga wa kienyeji na ni waumini wakubwa wa ushirikina!
Kila nikipima haya mawili katika mizania ya haki bado USHIRIKINA una nafuu kubwa katika uhalisia wake kuliko hiki kitu kizuri kiitwacho dini!