Unapo ambiwa ahlul fitrah ni watu ambao hawakufikiwa na ujumbe wala mtume, kisha ukasoma aya inayosema ya kuwa kila umma ulifikiwa na ujumbe unajifunza nini hapo ?
Hapo najifunza kuwa ahlul fitra ni kikundi kidogo cha watu ambacho kipo ndani ya kundi kubwa la watu (ummah)kundi ambalo lilifikiwa na Mtume na ujumbe pia.
Tukisema mtume tunakusudia na ule ujumbe.
Aya haikusema kuwa kila mtu alipewa ujumbe ama alifikishiwa utume,aya haiakuainisha kuwa kila mtu bali aya imeainisha kuwa kila ummah.
Sasa ukidai kuwa ahlul fitrah hawakupewa utume kwani hapo tafsiri yake si ni watu wa fitrah tafsiri ambayo ni ndogo ambayo inatoa idadi ndogo kuzidi ile ya ummah.
Aya haikusema kila mtu alipewa mtumr aya imesema kila ummah ulipewa Mtume .
Na katika huo ummah wenye mtume sasa kuna baadhi ya watu wachache ambao hawakupata huo ujumbe wa Mtume sasa.
Ni sawa na kuwa waseme tanzania walileta chakula lakini haina maana kuwa kila mtanzania alipata chakula.
Ama tanzania walileta vyandarua haina maana kuwa kila mtanzania mmoja mmoja alipata,ila kwa tanzania walileta.
Au china wamepata corona,haina amaana kila mchina mmoja mmoja kaipata corona.
Na ndivyo ilivyo katika ahlul fitrah sasa.hao ni baadhi ya watu wachache katika ummah wa watu fulani waliopewa mtume,ila hao sasa hawakufikiwa na ujumbe huo na wala hawakufikiwa na mtume.
Wangefikiwa na mtume basi na huo ujumbe wa Mtume ungewafikia pia.
Kwa hiyo hapo changanua ubongo vizuri uone urahisi wa mambo.
Unasoma na kufikiri kaka ama unasoma tu kilichoandikwa.
Huku watu hao wakiingia katika umma na ni umma, nilikuuliza historia iliandika kuna watu waliitwa Wamagharibi ya kale bali kulipita kitambo hapakuwa na mtume wala nabii, hawa watu ni umma au ni nini ? Mathalani jamii ile ya Wagiriki na Wanafalsafa wa kale wa Magharibi huu ni mfano tosha, na waliishi kitambo kirefu sana. Kina Thales, Homeri, Demokritus wa Abdera, Plato wengine, hizi zilikuwa ni jamii kubwa.
Hao watu unaowasema wewe kama kweli hawalufikiwa na ujumbe siweI kukataa.lakini kutokufikiwa kwao haina maana ya kuwa ati hakukuwepo na ujumbe wa Mtume fulani ambae alitumwa kwa zama za watu ambao hao wanafalsafa wakiwemo.
Mfano baba yake mtume katika hadithi mtume anasema baba yake Mtume yuko motoni.
Ssasa kama yuko motoni na kafa mtume hata hajapeawa utume wala ujumbe unadhani kwa nini aende motoni na wakati yeye anakufa hapakuwa na mtume wala ujumbe wowote kwa wakati ule ?
Ukisema kuwa ilitakiwa wafuate mila ya nabii ibraahimu hapo maanaa ayake utakubali kuwa tokea aondoke nabii ibraahaimu ujumbe wake umefanya kazi na uliwajibikia zama zote za hapo kati mpaka kufikia wakati wa mtume muhammad,unakubali hilo ?