Sasa wewe unajenga hoja alafu unanipa marejeo.
Lazima nikupe marejeo sababu Elimu ni amana, na kila amana hurudishwa kwa watu wake, na mimi nakurudisha kwa watu wa Elu, kasome, na ninayo kuandikia hapa ndiyo utayakuta humo humo, ili ujihukumu mwenyewe.
Pili, naweka marejeo kwa mtindo huo ili kuokoa muda.
Wewe unatakiwa uweke hapa hayo marejeo na hizo hadithi.
Mpaka sasa hivi nimeshakumulia ile hadithi, aliyo isimulia al Imaam Ahmad, sasa kama hujaisoma hilo ni tatizo lako la kutokuwa makini, na nikakupa marejeo mengine ili ukasome na upate faida zaidi.
Nafanya hivi, sababu hapa tunajadili jambo la kielimu, na hakuna kipya zaidi ya kunukuu toka kwa wakubwa zetu, walio tuzidi kwa ubora,elimu na maarifa bali mpaka umri.
Sioni kama ni sahihi unajadiliana na mtu alafu unajenga hoja kwa ushahidi ambao upo kwako.
Ushahidi upo kwangu kivipi wakati nimekuwekea marejeo, unakumbuka ile nukuu uliyo niwekea kuhusu maneno aliyo yasema al Imaam Muqbil na unajua kwanini sikuendelea na lile jambo, sababu nilienda kusoma zaidi, na mimi nakuwekea marejeo kwa uwazi na si wewe peke yako usome bali yeyote atakae pita hapa aone na akosome kwa faida zaidi.
Wewe ndo utoe hayo marejeo na sio unaniambia mimi nikapitie,wewe kwa nini usilete hapa.
Sasa nitoe marejeo mara ngapi wakati kila hoja nakupa marejeo ukasome ? Au unataka nini zaidi ya hivyo ?
Hivi kuna jambo bora kuliko ninalo lifanya mimi, la kukutajia kitabu na nina la muandishi wa kitabu hicho, ili ukasome mwenyewe kama hukuelewa ukaulize upate ufafanuzi zaidi. Sasa naona unataka kunipotezea muda mzee.
Kama mjumbe unakubali kuwa ni mtume kwa nini unakataa kuwa kila umma walipata mjumbe ?
Hakuna aliye kataa ya kila umma uliletewa mjumbe, bali nakataa ya kuwa si sawa ya kusema ya kuwa hakuna watu ambao hawakufikishiwa mtume, sasa sababu Qur'aan na Hadithi thi hazipingani, ulitakiwa ukawaulize wakubwa zako ni vipi wanao anisha nususi hizi mbili na kupata jibu moja.
Kwa maana hiyo kabisa iko wazi ni kuwa wewe hujaelewa maana ya aya.