Sahihi kabisa, ni wakati gani unatumia dalili ya ujumla ? Je kwa kuangalia dalili au kwa njia gani ?
Unatumia dalili ya ujumla ikiwa hakuna dalili ya umaalumu.kama kuna dalili ya umaalumu basi dalili ya ujumla haifanyi kazi katika jambo hilo.
Kama hakuna dalili maalumu basi tunatumia dalili ya ujumla.
Mfano..
Mama aisha alipata siku za mwezi akiwa ameenda hijja,akamuuliza mtume kuwa amepata siku itakuwaje ?
Mama aisha akaambiwa kuwa afanye kila wanachofanya mahujaji isipokuwa twawafu.
Ukiangalia hapo utaona kuwa hata kuswali mahujaji wanasali pia kwa hiyo mama aisha hakukatazwa kusali alikatazwa kufanya tawafu.kwa maana kwa ujumla huo mpaka kusali ilikuwa asali.
Lakini kuna dalili khaaswa ambazo zimekuja nje ya hadithi hiyo kuvua kuwa mwenye hedhi hatakiwi kusali.
Kwa hiyo ujumla wa hadithi ya mama aisha utamruhusu kufanya kila anachofanya hujaji isipokuwa yale ambayo yamevuliwa kuwa hayafai kufanywa na mtu aliyeko katika siku zake.
Kwa hiyo dalili ya ujumla tunaitumia ikowa hakuna dalili maaluumu.
Lakini pia mtume hakufunga masiku haya kama alivyosimulia mama Aisha hadithi ipo katika Sahihi Muslimu. Sasa tutawauliza watu hao ambao unasema wamefunga na ushahidi umetujia ya kuwa mtume hakufunga masiku haya. Vipi wao wafunge masiku haya ?
Kwa matendo yake hakufunga.
Ila kwa maneno yake ameruhusu kwa ile dalili ya ujumla kwa kusema matendo mema.
Kama ambavyo mtume kwa matendo yake sala za usiku hakuzidisha zaidi ya raka 11.
Ila kwa maneno yake ameruhusu rakaa zaidi ya hizo 11 pale aliposema kuwa "sala za usiku ni rakaa mbili mbili...."
Kwa maana sali rakaa mbili,toa salamu,sali rakaa mbili toa salamu....pakikaribia alfajiri unamalizia witri.
Huwezi kusema kuwa ati haifai kusali zaidi ya rakaa kumi na moja ati kwa kuwa Mtume hakuzidisha,kwenye kauli yake karuhusu.
Kilicho ivua ipo hadithi ya mama Aisha kama nilivyo kugusia huko juu, hadithi ipo katika sahihi Muslim
Haijaivua kwa sababu hadithi ya mama aisha haikukanusha kuwa mtume hakusema maneno yale ya "masiku haya 10 matendo mema yanapendwa zaidi na Allah .."
Bali hadithi ya mama aisha inasema kuwa mtume hakufunga,na wala hadithi haijasema kuwa mtume hakufunga.
Hadithi moja inaeleza alichosema Mtume wa Allah.
Hadithi nyingine inaeleza alichofanya Mtume wa Allah.
Kuwepo kwa mpingano wa maneno ya Mtume na matendo yake sio hoja ya kuharamisha kitu kingine kwamba hakifai.
Mfano Mtume alisema kuwa sala za usiku ni rakaa mbili mbili....yaani mbili toa salamu,mbili toa salamu.
Ila mama aisha huyo huyo akasema kuwa Mtume hakuzidisha rakaa zaidi ya 11.
Sasa hapo kuna matendo ya mtume ambayo alionekana akifanya,na kuna kauli ya Mtume mwenyewe kama kule kwenye masiku 10 ya dhulhijja,kuna maneno na vitendo vyake.
Sasa huwezi kusema haifai kuzidisha zaidi ya rakaa 11 kwa kufuata ufahamu wako huo.