Mkuu, Copenhagen piga mzigo zichange tu wakti ndio huu.
Kuna wakati heshima itarudi kwa madiaspora wakianza kutia timu Tanzania kijumla.
Unafahamu sasa hivi kuna madiaspora kama sisi bado tunalea watoto, na wakiishakua tu basi tunawaachia walipe mortgage ya huku na sisi turudi tukafaidi hizo Euro huko Bongo.
Ni lazima kutesa iwe kwa zamu.
Na kuna watu watashangaa sana kuanzia mwaka huu.
Halafu mkuu Copenhagen kama hujaanza kutafuta mwenza uwaangalie sana hao vidosho wa hapo kwako, maana kuna wengine ukianza nao wanabana mno kuhusu Euro, unatakiwa uwe "smart".
Kama unapenda kuchanganya, ukitaka wadada wa ku-settle nae tafuta pande ya East kama shemeji yako hasa wa Latvia na Estonia.
Wao nao kiingereza chao ni kama wanajifunza na akikukuta unatema ung'eng'e mzuri anakukubali, maana utamsaidia mambo mengi kama shule.