Diaspora na deni la Taifa

KAYGREKO

Member
Jan 18, 2013
37
32
DIASPORA NA DENI LA TAIFA

Hakuna takwimu kamili, lakini inaaminika watanzania tuliopo ughaibuni tunafika milioni mbili.
Aidha wengi tunaoishi ughaibuni, tunajua nchi yetu ina deni la nje na la ndani japo wengi hawajui kiuhakika ni kiasi gani.

Leo ningependa kuja na ushauri ambao kwa wale wataouona ni ndoto za Abunuwasi ni vyema wakakaa kimya. Ama wale wataoona unafaa ila una makosa yatayohitaji kurekebishwa ni vyema warekebishe huenda tukapata pa kuanzia.

Hapa Ugiriki wakati ule wa Crisis iliyotufikisha kwenye Capital control,tukawa tunakadiriwa kiwango kidogo cha kutoa pesa kwenye ATM,na wengine walipoteza ajira wakashindwa hata kumudu mahitaji muhimu, ulibuniwa mfumo wa kusaidiana (HAUKUANZISHWA NA SERIKALI WALA VYAMA VYA KISIASA) Wagiriki waliopo nje ya nchi nao walishiriki ipasavyo.

Hapa sitopenda kufafanua nini walifanya bali nitapenda kujikita katika mazingira yetu sisi watanzania milioni mbili tuishio ughaibuni.

Nimejiuliza swali lifuatalo: Badala ya kutumia usd 50 kwenda angalia mechi moja, au kutumia euro 50 kunywa bia na nyama choma, au(,….) hivi kweli tutashindwa kujitolea japo usd MOJA TU? (au 2,5,10 au zozote atazoweza kila mmoja wetu kulingana na uwezo wake? Of course siyo wote watakaotoa lakini idadi yoyote itayopatikana itakuwa imesaidia. Hili linawezekana kama tutakuwa tumeelewa na kuuona umuhimu wa kupunguza deni.

Najua kuna wataohoji ni bora hiyo dola moja wakawatumia wazazi wao na wengine wataohoji kuwa hizo zitaibwa,zitatumika vibaya nk. Lakini inabidi tufike mahala kama taifa tuanze kujijengea utamaduni wa kupenda kusaidia taifa hadi tunaowapa majukumu nao wafike mahala wahisi uzito wa majukumu yao.

Huku ughaibuni kuna waTZ wana ujuzi na utaalam wa hali ya juu mno wakikaa wanaweza kutupatia mfumo mzuri wa kuhakikisha hizo pesa tutazochangia zinaonekana wapi zilipofika.
Je unaliboreshaje wazo hili ili tupate pa kuanzia ?

KAYU LIGOPORA
ATHENS – GREECE
28/10/2021
 
Nakuunga mkono Mkuu kwa kuja na wazo zuri kabisa LA kizalendo,kwa mtazamo wangu naona ikiwa wazo hili litaungwa mkono na kupitishwa,hizo fedha zitakazopatikana zisipelekwe kwenda kulipa deni lolote la taifa iwe la ndani or nje..Bali hizo fedha ziletwe huku nyumbani ziboreshe Vituo vya afya kwa kununua vifaa tiba kuongeza idadi yake.

Huku Nyumbani tatizo la Afya bado ni kubwa kuna vijiji kupima malaria na typhod mpaka usafiri kilometa karibu hamsini na kuendelea ilihali miundombinu ya barabara ikiwa sio rafiki.

Mama mzito akitaka kujifungua kinachotegemewa ni kudra za MwenyeziMungu ili ajifungue salama mana likitokea la kutokea inakuwa mtafutano.

Kama huko tunaona hakufai pia basi ni kheri hizo fedha zikatumika kujenga viwanda ili kutoa ajira kwa sisi watanzania wenzenu,huku hali sio hali ajira hakuna na tukijiajiri mijini machinga tunaondolewa.

Na nyie mlioko huko ughaibuni mkiona kuna michongo mnatushika mkono ndugu zenu kuongeza idadi ya Diaspora wengi hii itasaidia kuongeza fedha nyingi za kigeni na kukuza pato la taifa.

Nigeria nafikiri ndio wanaoongoza Afrika kwa kuwa na Diaspora wengi duniani,hili linasaidia kuchangia maendeleo ya Nchi.Cha msingi nyie kubalianeni tu kuchangishana hizo fedha zipatikane zikija huku mambo ya kufanya na muhimu ni mengi.

Wasalaam
 
sijaelewa pesa kufika hapa Tz.

za corona zinaliwa za misaada ya elimu zina nunuliwa ndege.

hizo pesa zenu tengenezeni maisha yenu au msubiri mpaka utawala utakao kuwa unaheshimu maisha ya wananchi wake
 
sijaelewa pesa kufika hapa Tz.

za corona zinaliwa za misaada ya elimu zina nunuliwa ndege.

hizo pesa zenu tengenezeni maisha yenu au msubiri mpaka utawala utakao kuwa unaheshimu maisha ya wananchi wake
Mkuu wamesema watakuwa wanaziControl wenyewe hivyo kuondoa shaka yoyote ya ubadhirifu na matumizi yasiyo sahihi na makusudio.

Tusiwavunje moyo watu kama hawa Mkuu,mbegu ya Uzalendo ikiota inatakiwa kupaliliwa na kumwagiwa maji ili iendelee kumea.
 
Hizo pesa endeleeni kunywa bia na nyama, maana sisiyemu zikifika watesema ni zao na wamezipata kupitia fedha zao za ndani.
 
Wazo zuri sana ili. Kwa ushauri wangu Diaspora wafungue NGO yao nchini na pesa zote zipitie hapo ili kufikia walengwa.

Ninapata shida sana kuona watoto wanakaa chini na waalimu wanakaa kwenye nyumba za majani wakati huo huo kuna watu wako huko nje wanaweza kusaidia.

Uchangiaji ukiwa mzuri, zingine zinakwenda kulipia deni la serikali. Ila kwa hii nchi yetu sijui maana kila kitu ni siasa na vikwazo ni vingi. Ninawatakia kila la heri wachangiaji wa huu uzi.
 
Hujamalizia ila umeeleweka... anyways, hela yangu nimeitafuta kwa mbinde (kwa kupoteza muda akili nguvu na kadhalika) halafu leo niipeleke tena serikalini kulipia deni la taifa. Soma tena hapo mwisho LA TAIFA maana yake siyo la watu fulani

Hiyo hela mpaka unaipata umeshakatwa kodi na malipo kadha wa kadha kwajili ya serikali sasa iweje tena uipeleke huko!? Siyo kwamba napinga uzalendo au mimi siyo mzalendo bali hapa ninachomaanisha mngejikita kwenye maswala mengine yanayogusa kijamii mojakwamoja zaidi kwamfano

1.Kujenga na kuwezesha miundombinu ya afya na elimu
2.Kujenga miundombinu ya Huduma za maji umeme na barabara
3.Kuwezesha miundombinu ya... na kadhalika na kadhalika

Hiyo itafanya serikali iweze kujikita kwenye mambo mengine zaidi ikiwemo hayo madeni (kwakuwa itakuwa imekasimisha/imepokewa/imepunguziwa baadhi ya majukumu


Hatahivyo sijawahi kuona mtu anapewa hela ili akalipe madeni makubwa! Bali nimeona anawezeshwa tu mifumo ya namna ya kuweza kulipa deni.Hata serikali sidhani kama ikipewa hela hiyo itafanya hivyo zaidi ya kuielekeza kwenye mambo mengine ya msingi sana sana itAjiongezea sifa ya kuweza kuwa na kigezo cha kukopa zaidi

MASWALA YA MADENI YA TAIFA MWACHENI TAIFA MWENYEWE ALIPE.
 
Watanzania waishio nje hata laki tatu wanaweza wasifike.
Usichokijua usikiongelee utawapoteza wanaotaka kujua. Na kama ulikuwa umeongea kiutani basi naona kadhia hii si ya utani.Try to be serious. Je wewe ushawahi kuja nje? Kama bado waulize rafiki zako watakujulisha kuwa hiyo idadi ya laki tatu unayoitaja ni ndogo mno
 
Kabla ya yote tuanze kuiomba serikali iwe transparent na matumizi pia takwimu zipatikane wazi ili tujue hela zinazochngwa zinatumikaje.

Mpaka sasa hivi hat ufahamu manunuzi ya ndege yalikwendaje.
 
Usichokijua usikiongelee utawapoteza wanaotaka kujua. Na kama ulikuwa umeongea kiutani basi naona kadhia hii si ya utani.Try to be serious. Je wewe ushawahi kuja nje? Kama bado waulize rafiki zako watakujulisha kuwa hiyo idadi ya laki tatu unayoitaja ni ndogo mno
Hata laki tatu wengi, sidhani hata kama wanafika laki na nusu.
 
Back
Top Bottom