Diamond Platnumz anavuna alichopanda. Wasanii wenzie wasilazimishwe kumuunga mkono. Mmesahau ya Fiesta kipindi cha Makonda?

Diamond asijione yuko salama kupostiwa na wasanii ambao hua hapendi kazi zao kufanya vizuri, in short wanajua kwamba diamond hua anawabania, huu unaweza ukawa ni mtego mkubwa sana kwa diamond. Asipokua makini ndio itakua mwisho wake!

Hua anawabaniaje?
 
Bila support ya hao wasanii na tena media kibao zikimbania na bado kapata nomination (na si mara ya kwanza), most viewed and paid artist kwenye platforms zote unazozijua wewe.

Hao wanaosapotiana mbona hatua hawapigi wakafika alipo? Let us learn to appreciate.

Get hate or motivated
Wajina,baadhi ya mibongo ina roho nyeusi sana,yaani hawapendi kabisa mafanikio ya wengine
 
Kama yeye asivopenda mafanikio ya wanamuziki wengine
Sidhani,asingewainua kina harmonize,rayvann,zuchu na wengineo

Amin wabongo hatupendi wenye mafanikio ila Diamond sijaona kosa lake,ni chuki binafsi tu.Ukiangalia wengi wanaomsema vibaya wana wivu na mafanikio yake.Mfano hao wanaosema kuwa ooh aliipigia chapuo CCM kwenye uchaguzi mkuu uliopita,hata wewe ungekuwa msanii unayejielewa huwezi kwenda tofauti na chama chenye Serikali,Afrika demokrasia bado sana kukubali mawazo tofauti
 
Sasa mtu unamsifia makonda alafu niwe na mapenz na wewe ya nini
 
Wanajamvi Habari.

Hivi karibuni baada ya msanii Diamond Platnumz kuchaguliwa kuwania tuzo za BET kumeibuka makundi mbalimbali hasa baadhi ya wasanii na wanasiasa kulazimisha wasanii na wadau wote wa muziki na wasio wadau wa muziki kumuunga mkono Diamond.

Lazima tuseme ukweli kuwa hata Diamond mwenyewe huwa haungi mkono wasanii wote kwenye kazi zao na wadau wote kwenye kazi zao hivyo tusiwalaumu au kuwalazimisha watanzania wote kumuunga mkono Diamond.

Lazima tukubali Diamond ana makundi na yanajulikana na ndiyo yanayo mgharimu sasa kwa hiyo watu waache nature/asili ichukue nafasi.

Nakumbuka kipindi kile cha Paul Makonda alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam alizuia kufanyika kwa tamasha la Fiesta na Diamond na kundi lake ndio waliongoza kuchekelea na kuwabeza Clouds....

Diamond alikuwa anajua fika kipindi kile wasanii wenzie wengi walikuwa wanapata kula kupitia lile tamasha lakini alichekelea kufungiwa kwa hilo tamasha hadi kukwaruzana na wakina Fid Q ... Kwa hiyo watu waache wachague cha kufanya wasilazimishwe uzalendo maana Diamond sio mzalendo.

Wasanii wanampost tu kwakuwa wasionekane wabaya na wengine wanafanya hivyo kwakuwa ni mmiliki wa radio lakini si kwamba wanapenda maana ukweli ni kwamba Diamond huwa hatoi support kwa wasanii wenzie....

Watu waache wawe huru kabisa maana Diamond atavuna alichopanda watu wasilazimishwe kumuunga mkono.
Hivi toka 2011 unamuombea jamaa ashuke haujakoma tu??
 
tanzania wajinga wengi sana sikuwahi kujua tundu lissu ana akili ndogo kiasi hiki, yaani mtu kua mpenzi wa chama anachokitaka imekua shida?? Hata mm sikipendi chama cha mapinduzi ila tusilazimishane mapenzi kila mtu afuate chenye manufaa kwake tusilazimishane
Kuwq muelewa Lissu na wanaharakati wengine hawajamushambulia Mond kuhusu mambo ya uchama. Wanachokidai ni Mondi kutokemea uovu wa uvunjifu wa haki za binadamu uliokuwa ukifanywa na ile serikali, badala yake akawa anawaunga mkono waziwazi.
 
Huo uvunjifu wa haki kama upi ambao alikuwa anauunga mkono?
 
Kwani diamond akichukua tuzo nyie mnafaidika nini!???..na hasipochukua nyie mnapata hasara gani!!?..kila mtu na apambane na Hali yake bwana..
 
Watu wanakufa awamu ya Magufuli, yeye kama mtu mwenye ushawishi ndani ya Taifa anaimba nyimbo eti akae kimya.

Hovyo kabisa, ameshindwa kujua mioyo ya Watanzia wengi imechoshwa na siasa, vijana wengi walianza kumkataa kutokana na unafki wake.
 
Mbona mange kimambi alikua na ushawishi akawashawishi mkaandamane na hamkwenda watanzania ni wanafiki tuu, watanzania mngetoka wengi kwenda kuandamana naamini hata hao wasanii wengeunga mkono
 
Back
Top Bottom