Diamond awe mfano na darasa kwa wahusika wote

Diamond awe mfano na darasa kwa wahusika wote

Nauliza sijibiwi humu..
Kwanini huwa haudhurii vikao vinavyoitishwa na Wizara kukadili majamboz.. kama alivyosema Waziri mwenyewe?
Wawakilishi wa diamond babutale na fella wahudhuriaji wakubwa wa vikao vya BASATA na kwa watu wanaongoza kuhudhuria vikao ni Babutale,Fella na Nikki wa pili .
 
Mkuu uko right kiukweli Shonza kachemka! Mond naye amekataa haki zake kukanyagwa, mara ngapi vikundi vya ngoma vya Tzee vya makabila mbalimbali vinacheza nusu uchi na basata kimyaaaa, yaleyale ya kumfungia shilole kwa kosa alilolifanya belgium. Msanii anafungiwa miezi 6 asijihusishe na muziki khaaa ustaarabu wa wapi huu?? Tatizo kila waziri anatafuta kumfurahisha Magu matokeo yake ndiyo hayo. Kweli hii Tanzagiza. Mwakyembe naya maskini kawa teja la madaraka ila hajioni anamuona Mond kalewa umaarufu!!
Tena mkuu utadhani Diamond platnumz ameanza kuwa Star mwaka jana pia Amesahau wamempa Bendera kwenda GABON Africon hata CCM-2015 walimchukua kwa sababu ya Umaarufu na Ushawishi #Chuki#Hujengwa# na huku naona wanamuharibia Rais maana wengi watazingisha chuki dhidi ya Serikali.
 
Pamoja na kupanic kwa Diamond (jamaa anapoint ila tatizo uwasilishaji wake ,lkn yupo sahii 100%) lkn inabidi wajitafakari kwanza BASATA ,TCRA na WIZARA .Hii tasnia ya burudani inaenda kimungumungu (wasanii walivyo kama wale mbuzi wakafara) na maamuzi yao yanawaumiza wasanii baada ya kuwasaidia.Kuna watu wanasema Diamond ana mdomo kwani kafungiwa peke yake,ukiona hivyo mond haki yake anaijua,ila hao wengine waoga wameamua kuwa kondoo,kama huamini unaweza ukakuta sasa hivi wanatuma sms kumpongeza diamond,lkn wanataka sana kuongea.
 
*Adhibitiwe na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kwa 'kumtweza' Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo kupitia mitandao (kama itathibitika hivyo). Umaarufu haujawahi kuizidi nguvu serikali popote pale ulimwenguni.

*Mawaziri, Manaibu Mawaziri na viongozi wengine wa kiserikali wajiepushe kutenda na kusema kinyume na taratibu za kiserikali. Mitandao ya kijamii si njia sahihi ya kutoa kauli ya kiserikali. Pia, viongozi wetu wajiepushe kujibu mambo yasiyo na msingi.

* Tuheshimu viongozi wetu hata kama hatuwakubali au kuwapenda. Na viongozi wetu watuheshimu hata kama wana uwezo na nguvu za kufanya na kusema popote na lolote. Tuheshimiane.
Hii ni siasa mzee msioelewa hilo vichwa ndio vinawauma
Hawa watu wanawapigia ngoma na nyie mnacheza hapo wanawacheka kweli kwa kuona kwamba wanafaulu
Mpango wao
 
Petro tatizo langu ni tabia inayojengeka ya hawa wanasiasa. Wanafikiria kudhalilisha watu ndiyo utendaji kazi. Hata kama hao wasanii wana makosa kwani taratibu za kiserikali zikifuatwa unapungukiwa nini. Kwa nini sasa baada ya Diamond kusema ndiyo wakumbuke kuwa kuna kuandika barua.

Wanashindwa kujua kuwa kauli zao hasi kwenye vyombo vya habari na mitandao inawaumiza zaidi hao wasanii na hasa hawa ambao wameshajijrngea soko la nje ya nchi.

Halafu ni kinyume cha haki za binadamu kumfungia mtu kufanya kazi yake inayompa kipato. Adhabu kama hii ni za kisoshalisti na hazifai. Unamfungia mtu kufanya kazi maana yake unamuua.

Na hawa ni Wakristo; kwa nini hawatendi kama Kristo alivyowafundusha?
Kweli mkuu maana upande wa majirani zetu kwenye pro wako vizuri ukiangalia kwenye Media zao umeanza kuweka [HASHTAG]#Teamaftetban[/HASHTAG] hii inaharibu taswira ya nchi kiukweli.
 
naww ni dikteta mavi? unaweza ukasema kitu gani mond kakosea hadi achukuliwe hatua zakuwekwa ndani ao umekurupuka tu ??
 
Shonza ajifunze kuziachia taasisi za wizara yake zifanye kazi zake. Hawezi kuwa kila kitu.
Ilitakiwa kazi ifanywe na BASATA ili wasanii wa appeal kwake.
Diamond asiponzwe na jeuri anayopewa na Bashite. Kuna leo na kesho.
unatapika
 
maadili ni suala pana sana na kama watu walimsikiliza diamond vizuri alitolea mfano ngoma za jadi kama baikoko na nyingine nyingi zinazofanana na hizo alisema vitu vinavyofanyika huko ni zaidi ya hivi ambavyo serikali inahangaika navyo kwenye nyimbo za wasanii. Swali je mbona serikali haipigi marufuku ngoma za namna hiyo.
 
Kama tunaka taka kusamamia maadili tusiangalie muziki tu au sanaa tu. Mfano mimi ningependa kumuuliza huyu naibu waziri kwa mfano yeye siku ile kwenye xxl alionekana akiwa amevaa suruali nyeusi, swali JE MTOTO WA KIKE KUVAA SURUALI HAYO NI MAADILI YETU? siongopi wakuu ukifika katika baadhi ya jamii hapa Tanzania ukiwa umevaa suruali alfu wewe ni mwanamke wanakuona kama mtu wa tofauti ni zaidi wazee watakuona wewe ni mhuni. Okay that's not a case, je maadili ni
1. Kuteka watu
2. Kuikubali rushwa
3. Kuvaa vimini au transparent clothes
4. .........

kama mmeamua kusimamia maadili katika jamii yetu lazima tuangalie swala hili katika mtizamo mpana sana Lazivyo mama ulikurupuka
Kwa mfano picha za ngono ni miongoni mwa vitu ambavyo vimeharibu maisha ya vijana wengi katika jamii yetu, mbona hamuifungii hii mitandao inayosambaza picha za ngono isifanye kazi hapa Tanzania, kama kweli mmefungia nyimbo za diamond eti kuna wanawake wapo naked, je hiyo mitandao inasambaza picha za wanawake ambao wamevaa kanzu ???
 
Wawakilishi wa diamond babutale na fella wahudhuriaji wakubwa wa vikao vya BASATA na kwa watu wanaongoza kuhudhuria vikao ni Babutale,Fella na Nikki wa pili .

Msaniiiiii
Msaniiiiiii hajataja mameneja au?
 
BASHITE NDIO REMOTE YA A BOY FROM TANDALE,KWAHIYO DIRECTOR WA HIYO MOVIE NI DAB,USIINGIE KICHWA KICHWA MWANANGU.(IN MABOYA'S VOICE).

 
Back
Top Bottom