Diamond anauliza ampende nani??

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
[h=3]DIAMOND ADONDOSHA PINI JIPYA 'NIMPENDE NANI'[/h]

WAKATI sakata la msigano wa kimapenzi baina ya msanii nyota wa muziki wa bongo fleva Nassib Abdul ‘Diamond’ dhidi aliyekuwa mpenzi wake Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu na anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa sasa, Jokate Mwegelo likiendelea kushika kasi, msanii huyo ameachia singo mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nimpende Nani’.
Diamond ametoa singo hiyo kama swali kutokana na hali halisi ya sakata hilo inavyoendelea kwa sasa kwani wiki chache zilizopita aliachia singo nyingine mpya inayokwenda kwa jina la ‘Mawazo’ ambao ndo kwanza umeanza kushika kasi katika vituo mbalimbali vya redio.
Wimbo huo ambao Diamond anaonekana kuujiuliza ampende nani kati ya wapenzi wake hao huku akiwataja kwa majina Wema na Jokate, huku singo hiyo ikiwemo ndani ya albamu yake aliyoingiza sokani mwezi Novemba iitwayo ‘Lala Salama’ ambapo sehemu ya mashairi ya wimbo huo inasema ““Yasiwe kama Wema sepetu kila siku kwenye magazeti, simtaki kama Uwoya ni mtemi anahasira,awe mpole kama Jokate…nimpende nani, nimpendeee”.
Mbali na wimbo huo mpya, albamu hiyo inanyimbo kama Moyo Wangu ambao ulipata kushika chati mbalimbali za muziki, pia kuna Lala salama uliobeba jina la albamu, Chanda chema, Nimpende nani, Najua,Mawazo,Kwanini,Gongolamboto,Natamani na Kizaizai.
Awali Diamond ambaye alipata kutwaa tuzo tatu za muziki za Kilimanjaro, awali alitoa albamu ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘Mbagala’ ikiwa na nyimbo kadhaa ambazo zilipata kufanya vema kwqenye medani za muziki zikiwemo Nalia na Mengi, Kamwambie, Nitarejea, Binadamu Wabaya na nyinginezo
 
NIlihisi "the romantic" ni promoter wa Diamond since alipoanza kuleta yale masredi yenye takataka za wema na diamond.... Ok
 
NIlihisi "the romantic" ni promoter wa Diamond since alipoanza kuleta yale masredi yenye takataka za wema na diamond.... Ok

Ni wazi utakua umekurupuka mzee,mi ndio mara ya kwanza kuleta mambo ya huyu mtoto humu,na hii nimeifanya kutokana na ushamba wake,maana dogo kalishwa perege anatangaza mji mzima eti kala samaki sasa akilishwa pweza si matangazo yafika mpaka cnn naona!huyu kweli anatoka mbagala!
 
sorry kwa kurupuka... but you continue kumpa promo as we post

samahani sana mkuu, sirudii tena kukuita wewe promota wa diamond, ntakuita mshabiki wake mkuu kwa kuleta lyrics za wimbo wake na kuendelea kumpa promo:nerd:
 
Mafua yananisumbua,nataka nipyenge kamas,
fyeeee,
aaah,tone limeingia kwenye Chai
 
Apende kazi yake ya muziki cos ndio iliyomtoa tandale mpaka sinza,mboga moja mpaka msosi wa draft,kutoka kupata watoto poli mpaka masuperstar,pamba moja mpaka kuwa duka,pair moja ya viatu mpaka kumatchisha so apende muziki wake kwani ndio kila kitu na akumbuke kuweka akiba kidogo cos bado mdogo na anasafari ndefu sana ktk maisha na ya mafanikio,wazuri wanazaliwa kila cku tena na adabu zao
 
Thats true dogo inabidi azingatie muzik na maisha yake ya badae maana ngoma ikivum
 
Ni wazi utakua umekurupuka mzee,mi ndio mara ya kwanza kuleta mambo ya huyu mtoto humu,na hii nimeifanya kutokana na ushamba wake,maana dogo kalishwa perege anatangaza mji mzima eti kala samaki sasa akilishwa pweza si matangazo yafika mpaka cnn naona!huyu kweli anatoka mbagala!

TANDALE. Take Note Son
 
Mbona lips zake zimefanana sana na za Wema? I mean, ah ngoja niache.

Najua ntaitwa hater. Lakini mwanaume unafikie hatua ya kujiremba hivi? Thats not man enough. Piga scrub sawa ila mpaka malip bum sijui lip shine. Khaa inatia kinyaa!!
 
Najua ntaitwa hater. Lakini mwanaume unafikie hatua ya kujiremba hivi? Thats not man enough. Piga scrub sawa ila mpaka malip bum sijui lip shine. Khaa inatia kinyaa!!

mkuu nimecheka sana kwa hii post yako ila huwezi kuitwa hater kwa kuongea ukweli hii ya leo ni real kabisa.
 
Back
Top Bottom