Diamond anashindwa kufanya Timing nzuri katika biashara zake

Oct 26, 2021
75
150
Kwanza nimpongeze kwa jitihada anazofanya kwani zimekuwa motisha kwa vijana wengi ambao wanapenda sana umaarufu wake kuliko jitihada alizoonesha na harakati ngumu alizopitia.

Niwakumbushe vijana mpaka anafika pale bwana Almasi haikuwa kazi nyepesi, na kama mlivyo sikia kwa mahojiano yaliyofanyika na msanii ambaye alikuwa chini ya lebel yake akisema nakuu "... uniwezi kiselikali, wala kiuchawi..." Pengine kwa jitihada pekee za kawaida hisingewezekana na hapo ndo nakumbuka msemo wa rafiki yangu mmoja alipokuwa akinambia ili kuwa tajiri na kufanikiwa ndani ya jiji la Dsm lazima uwe na roho mbaya.

Tuachane na hayo twende kwenye suala zima la Timing ambalo limekuwa mada kuu na msukumo mkubwa katika ili. Sidhani kama ni wakati sahihi kwa bwana Almasi kuleta betting App nadhani angewekeza zaidi nguvu kwanza kupush Wasafi TV/radio kwanza ili kufika mbali, Mpaka sasa redio hii haijafika nchi nzima ya Tanzania na sehemu ambayo imefika ni sehemu chache imekuwa redio pendwa kwa wakazi wa maeneo haya.

Hapa anapata changamoto kutoka redio kongwe ikiwemo Clouds, East Africa redio, Radio one etc.. kwa upande wa TV kuna mafanikio yake kwani hapa ni vituo vingi vimepwaya na vimekuwa vikijitafta aswaaaa ndipo katikati ya tundu ili alipenyea walau na kupata nafuu. Kwa upande wa redio ukitoa SPORTS ARENA kdg na Kipindi cha Diva LAVIDAVI basi zinabaki frequency tu vingine ni wanaruka ruka tu.

Naendelea huu ulikuwa ni wakati wa kupush redio na TV kuliko iki kilicholetwa kulingana na changamoto iliyopo katika sekta ya habari asa baada ya kuwapoteza wakongwe na makontawa katika sekta hii (R.I.P RUGEMALILA MTAHABA, DR. REGNALD MENGI na watangazi maarafu ikiwemo BABA T alietutoka siku sio nyingi, KIBS etc).

Katika kufanya Timing hii bwana Almasi ingependeza zaidi kama angekuja na Album ambayo ingemuimarisha zaidi kimziki na kumrdisha daraja la juu kama ilivyo kwa kina Wizkid, Burna Boy, Tems na ingewapoza walau mashabiki zake ambao kawaachia nyimbo ambazo upepo wake unawahi kukata sana sio kama zile za awali ambazo zilikaa kwa trend kwa zaidi ya miezi hadi mwaka... ubaikumbuka onanaa aloimba na Mr. Flavour ww?!!! 2016 nzima ipo trending.

Changamoto zilizopo kwenye betting app ni nying, uendeshwaji wa hii kitu ni inahitaji mzigo /Uwekezaji wa kutosha ili kutoa odds zilizoshiba na maana. Vijana wengi wanaofanya michezo hii wanataka pesa iliyokubwa ili wapte kuneemeka mapema sio mchezo mchezo.

Pia masuala ya kudukuliwa; hapa ni imani yangu amrjipanga naaIT wake kukamilish ili zoezi.... itaendelea
 
simon2016

JF-Expert Member
Oct 19, 2020
422
1,000
Ana watu nyuma Wana pesa wapo tayari kufanya partnership yeye atoe jina la label yake na kusimamia, inatosha kufungua miradi yake hata kama ataweka kiasi cha pesa.

Hawezi kaa anawakatilia watu Nina radio na tv subirini kwanza nizipush.

Kila jambo Lina mkakati huwezi fungua radio leo halafu miaka 2,3 iwe kila mahali rafiki
Radio zinaenda kutokana na uhitaji ndio maana kahakikisha kwa kiasi frequency zipo kwenye majiji na mikoa yenye uhitaji.

Mwisho radio/Tv pekee hapa Tanzania inayoshika popote utakapo kuwa ni tbc radio/tv zingine ukiwa vijijini huko hupati mawimbi yao.
 
nG'aMBu

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
1,854
2,000
Kwanza nimpongeze kwa jitihada anazofanya kwani zimekuwa motisha kwa vijana wengi ambao wanapenda sana umaarufu wake kuliko jitihada alizoonesha na harakati ngumu alizopitia...
Hata kama yake, iyo kamapuni ina options nying za kubet, kama corner, card, cross bar, shoot on target etc, vinginevyo itapata upinzan sana kwa makampuni mengine
 
steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
8,051
2,000
Mkuu, hakuna asiyejua kwamba betting ndio habari ya mjini kwa sasa hasa kwa kizazi cha sasa, na makampuni ya industry hiyo yanapiga sana hela ingawaje nayo yanaliwa pia, naona ni bora mno kudiversify uchumi kuliko kung'ang'ania vitu vile vile, kwa mtazamo wangu hiyo haimzuwii kutofanya hizo biashara nyingine alizonazo
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
25,878
2,000
Kwanza si sahihi kusema Mond amekaza sana kufika alipo,yaani ni kumpa sifa ambayo si sahihi,wasanii wengi sana wanakaza ila bahati ni jambo jingine.

Kwe kwa shari ama kwa karata mezani, Mond ana nyota kali sana ambayo imembeba maeneo yote anayogusa.kama hutaki jaribu kupita alipopita, ndio utanielewa.

Kuhusu uwekezaji kwanza hilo kampuni yeye ni bland tu, sijui anakunja ngapi huko, halafu hata kama anafeli yeye sio malaika kwamba atapatia kila sehemu.
 
sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
1,316
2,000
Hii sio kampuni ya Diamond.

Wakenya wametumia jina la Wasafi kupush biashara yao na Diamond anavuta mkwanja wake saaaafi
Diamond hawezi kuipa jina Wasafi kampuni isiyo yake.

Wasafi bets ni kampuni inayomilikiwa kwa pamoja kati ya Diamond na mtoto wa Mwai Kibaki.

Diamond hana huo ufala wa kupush biashara ya mtu.
 
Tempus Fugit

JF-Expert Member
Jun 22, 2016
607
1,000
Hii sio kampuni ya Diamond.

Wakenya wametumia jina la Wasafi kupush biashara yao na Diamond anavuta mkwanja wake saaaafi
Huwezi jua huenda ana hisa kwenye kampuni hiyo kwa hapa Tanzania. Yaani hiyo kampuni kwa kushirikiana na Either Wasafi limited wameanzisha a subsidiary company in Tanzania ambayo Wasafi ni minority shareholder whereas hiyo kampuni nyingine ni major shareholder.
 
Oct 26, 2021
75
150
Mkuu, hakuna asiyejua kwamba betting ndio habari ya mjini kwa sasa hasa kwa kizazi cha sasa, na makampuni ya industry hiyo yanapiga sana hela ingawaje nayo yanaliwa pia, naona ni bora mno kudiversify uchumi kuliko kung'ang'ania vitu vile vile, kwa mtazamo wangu hiyo haimzuwii kutofanya hizo biashara nyingine alizonazo
Habari ya mjini ni what is future of money and banking system?!!! There we speak about #Cryptocurrency sio kubet mshua
 
Mayu

JF-Expert Member
May 11, 2010
4,797
2,000
Huwezi jua huenda ana hisa kwenye kampuni hiyo kwa hapa Tanzania. Yaani hiyo kampuni kwa kushirikiana na Either Wasafi limited wameanzisha a subsidiary company in Tanzania ambayo Wasafi ni minority shareholder whereas hiyo kampuni nyingine ni major shareholder.
Inawezekana pia
Maana yangu ilikua kwamba huwezi kukataa deals mpya ambazo haziingiliani kimaslahi kwasababu kuna moja bado haijatanuka kwa mtazamo wa mtoa hoja

Leo hii likija shirika la ndege la Australia na kutaka kuingia makubaliano na wasafi kupush huduma zao Mondi hawezi kukataa kwasababu eti Diamond karanga hazifanyi vizuri
 
steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
8,051
2,000
Habari ya mjini ni what is future of money and banking system?!!! There we speak about #Cryptocurrency sio kubet mshua
Vijana wa mjini wengi hawajui hizo mambo ila wanajua kubet tu na ndio maana huko kuna wateja wengi kuliko huko unaposema ingawaje unachosema ni sawa ila nako kupigwa ni kulekule hizo coins zikishuka thamani
 
Mayu

JF-Expert Member
May 11, 2010
4,797
2,000
Diamond hawezi kuipa jina Wasafi kampuni isiyo yake.

Wasafi bets ni kampuni inayomilikiwa kwa pamoja kati ya Diamond na mtoto wa Mwai Kibaki.

Diamond hana huo ufala wa kupush biashara ya mtu.
You have a lot to learn mkuu

Diamond karanga ni wahindi waliingia makubaliano na Mond, baada ya bidhaa kufanya vizuri sikoni wahindi wakaona Mondi anavuta parefu kwa kuchangia jina tu wakashindwana

Vingamuzi vya Azam ni wazungu wamekuja na kubaini wakitumia jina la Azam biashara itaenda
Wakaingia makubalino biashara inapaa

Vivyo hivo kwa Wasafi bet
Kuna namna nyingi ya kuingia makubaliano
Anaweza kutoa jina tu na akawa anapata gawio la faida
Anaweza kutoa jina na malipo yakawa sehemu ya hisa zake kwenye kampuni

Kiufupi kutoa jina kuna faida zaidi maana hasara zitakua hazimuhusu
 
Nakwambia tena ukiona limetumika jina Wasafi ujue Diamond ni sehemu umiliki wa biashara.
Inawezekana haupendi iwe hivyo ila ndio ilivyo.
 
Mayu

JF-Expert Member
May 11, 2010
4,797
2,000
Nakwambia tena ukiona limetumika jina Wasafi ujue Diamond ni sehemu umiliki wa biashara.
Inawezekana haupendi iwe hivyo ila ndio ilivyo.
Ungesoma na kuelewa nilicho andika wala usinge nijibu huu utoto
Kwamba mimi sitaki kuwa Dai sio mmiliki?

Mnaakili za kitoto kuhamisha mijadala ionekane tunajadili kupinga Dai hana hela wala mafanikio....... hatupo huko

Hoja ilikua kwamba kwanini Dai anaanzisha biashara wakati Ingine zina suasua?

Akajibiwa jinsi nmna biashara zinavyo anzishwa

Sasa nyinyi mnachotaka kusikia ni kimoja tu “kampuni ni ya Dai” .......... that’s childish

Kanye west leo ni billionaire na hana kampuni ya kutengeneza viatu anatumia brand yake tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom