Je, Unatumiaje AI katika Biashara yako?

Je, Unatumiaje AI katika Biashara yako?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,913
Reaction score
6,603
Habari za wakti huu;
Miaka ya 90 wakati TEHAMA imepamba moto Duniani kwa tuliokuwepo kufahamu namna ya kutumia Computer ilikuwa ni TREND na ni Muhimu.Katika Kipindi waliibuka watu waliotajirika na hata waliofilisika.

Kw sasa hivi tuko katika zama za mbele zaidi ambazo ni zama za AI.Na kwa sasa hivi makampuni yanakimbizana kutengenea AGI(Artificial General Iteligence).Hizi mbio zinakuja na fursa na changamoto mbalimbali.Swala ambalo ninataka tulijadili leo ni Je Unaitumiaje AI?

Nimekuwepo hapa jukwaani kwa muda sana,katika kipindi hiki chote nimekuwa nikishiriki katika mijadala mingi.Hata hivyo kwa muda nimeona Jukwaa katika Ujumla wake alijatumia AI kama ipasavyo.Vilevile nimeona TABIA ya watu ama kukejeli matumizi ya AI au kuita AI kila jambo ambalo wanaona linaonekana kuwa BORA sana.Tabia hii imenifanya nileta Mjadala hapa ili tujadili kwa pamoja namna tunavyotumia AI na namna ambavyo tunaweza kuboresha matumizi ya AI kwa manufaa.

Wapo watu wengi sana ambao wanatumia AI katika shughuli zao ambao hawako tayari kukiri kwamba wanatumia AI,na wapo ambao kama wangeamua kutumia AI kazi zao zingekuwa BORA sana lakini wamechagua kutokutumia AI.Hii inanifanya nijiulize iwapo watu wanaogopa teknolojia hii ama tumechagua kuwa Late Adopters?

Mimi kwa sasa natumia AI kwa Asilimia karibu 70 ya shughuli zangu,katika baadhi ya shughuli natumia AI kwa Asilimia hadi 90 na nyingine natumia AI kwa Asilima 40.Ila hakuna shughuli yoyote ambayo situmii AI.Bado kuna maeneo katika maisha yangu ambapo natumia AI mfano maswali ya Afya,elimu,malezi mawasiliano ya kawaida na hata burudani.Ninatngeneza nyimbo kwa kutumia AI,picha,movies,simulizi za aina mbalimbali n.k.

Andiko hili hapa wakati wa kuliandaa nilishawishika kutumia AI ila kwa heshima ya JF nimechagua kuliandika bila msaada wa AI.Swali ambalo nataka tujiulize leo ni JE unatumiaje AI?

Utumizi wa AI una maeneo mengi sana?Unaweza kuwa mtengenezaji wa suluhu zinazotumia AI au unawezakuongeza uwezo wa AI katika kufanya mambo mbalimbali.Katika utumiaji wako wa AI ni lazima Ujiulize iwapo AI inaongeza Tija.Ni lazima tuondoke katika fikra za kwamba utumiaje wa AI sio jambo la kujivunia na badala yake tuwe tayari kukiri matumizi ya AI na zaidi tuonesha kwa wazi kabisa utumiaji wetu wa AI pale inapotulazima tumeufanyia validation ya kutosha.

Je unatumiaje AI?Karibu tujadili hasa katika biashara na ujasiriamali.Unaweza weka kabisa TOOL unayotumia,namna unavyotumia,changamoto na namna ambayo inakusaidia ila na wengine waendelee kujifunza.Niko hapa kwa ajili ya majadiliano juu ya namna bora kabisa ya kutumia AI.
 
Sasa hvi email zote natumia AI..... Na baadhi ya kazi zangu.

Mfano nina kazi...naipa kwanza AI afu ndo naanza kuiweka vile nataka..

Natumia ChatGPT.

Changamoto.....kuna siku niliipa kazi ya kunichorea ramani haikufanikiwa, sasa sijajua kama kuna app maalumu kwa ajili hyo
 
Changamoto.....kuna siku niliipa kazi ya kunichorea ramani haikufanikiwa, sasa sijajua kama kuna app maalumu kwa ajili hyo
Chanzo cha tatizo: Prompt haikuwa tight enough kuwezesha AI kuja na ramani kamili ya kueleweka kwa jinsi ya uhitaji.

[Nini cha kufanya]
  • Tumia muda mwingi wa kujiuliza nini hasa unataka (matokeo), kwenye hiyo kjazi husika, Andika kwa mtindo wa bullets points
  • Kisha Iambie AI ikutengenezee prompt
  • Kuna vijimaneno inatakiwa uambatanishe mfano: Anza hivi kwa kutumia kanuni za Prompt engineering / Context engineering borehsa hii prompt yangu.
[Kinachofuata] hakiki prompt iliyokupatia iwapo ina makosa. , Anza thread/chat mpya na kisha anza na ile prompt uliyotengenezewa na Ai.

[Matokeo]
- Utapata response iliyo bora zaidi kuliko matarajio yako.
 
Chanzo cha tatizo: Prompt haikuwa tight enough kuwezesha AI kuja na ramani kamili ya kueleweka kwa jinsi ya uhitaji.

[Nini cha kufanya]

[Kinachofuata] hakiki prompt iliyokupatia iwapo ina makosa. , Anza thread/chat mpya na kisha anza na ile prompt uliyotengenezewa na Ai.

[Matokeo]
- Utapata response iliyo bora zaidi kuliko matarajio yako.
Asante sana Mwalimu;
Kimsingi Utumiaji wa AI unahitaji sana mtumiaji awe makini sana na context pamoja na content.Ndio maana Mara nyingi kama kazi yako ni complex ba uzingatie expertise,skill level,goals and expected outcomes.Ili Upate hivyo unaweza itumie AI kukutengenezea Prompt Bora zaidi.Jambo lingine la Muhimu ni kufahamu kwamba KILA AI tool ina eneo ambalo inalimudu zaidi kuliko nyingine.Kuna AI ambazo ni TEXT oriented na zina Reasoning capacity kubwa na kuna ambazo zinamudu zaidi kazi za kisanii kama image,music and video na kuna ambazo zinamuda kazi za kitaaluma n.k.SO cha muhimu ni kuhakikisha pia unamatch Right tool to the right task.
 
Nikiri mimi hutumia AI na naiita rafiki yangu. AI naona ni mkombozi wangu maana nimepunguza gharama kwa kutumia AI. Kubwa zaidi ni mjibuji wa maswali yangu na msahihishaji wa maandiko yangu hata kwa kiswahili
 
Hivi sio kosa kutumia kibiashara maudhui uliyoyatengeneza kwa AI? Mfano nyimbo, machapisho, ramani etc
 
Hivi sio kosa kutumia kibiashara maudhui uliyoyatengeneza kwa AI? Mfano nyimbo, machapisho, ramani etc
Sasa unatakiwa utumie kufanya nini?

Mimi sasa hivi ninafanya kazi zangu kwa asilimia kubwa kwa kutumia AI,

Kutengeneza Ads naanza na AI kisha kisha ndo niende kwingine,kuandika email naanza na AI,kuandaa mkataba naanza na AI hata kuandia Proposal naanza na AI.Hata nikitaka kuandika Post JF naanza na AI
 
Hivi sio kosa kutumia kibiashara maudhui uliyoyatengeneza kwa AI? Mfano nyimbo, machapisho, ramani etc
Na hili hapa na Jibu la AI kwa swali lako

Kisheria na kimaadili, sio kosa kutumia maudhui uliyotengeneza kwa AI kwa ajili ya biashara, lakini kuna mambo machache ya kuzingatia:

  • Haki miliki (Copyright): Sheria za nchi nyingi (na masharti ya zana nyingi za AI) zinasema kuwa maudhui yaliyotengenezwa na AI 100% bila ubinadamu mara nyingi hayana haki miliki ya kipekee. Hii ina maana mtu mwingine anaweza kuyachukua na kuyatumia pia.
  • Masharti ya Zana (Terms of Service): Zana nyingi za kulipia (kama ChatGPT Plus, Midjourney, n.k.) zinakupa haki zote za kibiashara (commercial rights) za kile unachokitengeneza. Ila kwa akaunti za bure, inabidi usome masharti yao kwanza.
  • Kuongeza Mchango wa Kibinadamu (Human Touch): Njia bora zaidi ni kutumia AI kama msingi (draft/skeleton), kisha unafanya marekebisho na kuweka ubunifu wako binafsi. Hii inakusaidia kupata haki miliki kamili na pia kuhakikisha kazi yako ina ubora na upekee wa kibiashara.
Kwa kifupi, tumia AI kuboresha na kurahisisha kazi zako za kibiashara, ila hakikisha unakagua (validation) matokeo kabla ya kuyatoa sokoni!
 
Ewaaaa hiki cha haki miliki ndicho nilichokuwa nakitaka.
Asante sana
 
Back
Top Bottom