Dhana ya uwepo wa Mungu na mbingu

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,640
9,219
Habari wakuu,

Huu mjadala ni mpana sana na upo tangu miaka mingi sana, nitaeleza nadharia ya uwepo wa mbingu na Mungu jinsi ulivyoibuka, nitatumia mifano ya sasa na ya kale ili niweze kueleweka,

Nitaanza na concept ya mbingu. Fikiria maisha jinsi yalivyo magumu, fikiria changamoto za kimaisha unazopitia mfano huna ajira, huna shughuli yeyote, biashara ngumu, huna uwezo wa kununua chakula, unaumwa huna pesa ya kwenda lutibiwa hospitali, umebambikiziwa kesi na wanasiasa, hujapata mtoto, umelima mazao yamepigwa ukame hakuna utakacho vuna, umepata msiba wa mtu unayempenda kafariki ghafla n.k majanga ni mengi

Kumbuka upo Tanzania, bara la Afrika sayari ya tatu iitwayo dunia wengi mnaiita duniani,

Sasa unaambiwa kuna nchi inaitwa mbinguni lakini haijulikani ilipo, Raisi wa hiyo nchi ni mungu, mawaziri ni malaika na kwenye hiyo nchi hakuna changamoto zozote za kimaisha yaani vyakura vipo vya kutosha, mazingira ni mazuri, kuna bustani nzuri, kuna hewa safi, hakuna magonjwa na ukiwa huko hauwezi kufa, huitaji ajira wala kufanya biashara ili uweze kujikimu yaani bata zote ni bureeee ,

Lakini ili uingie kwenye hiyo nchi ni lazima ufe kwanza kisha siku ya mwisho utafufuliwa utafanyiwa interview kwa kuangalia experience ya matendo yako, kama ulitenda mema utaingia huko kama ulitenda mabaya hutaingia kwenye nchi ya mbinguni yaani bata utazisikia tuu na utapewa adhabu ya kuchomwa moto na kufa mara ya pili ila inasemekana kabla hujachomwa utafungwa minyororo miaka elfu moja kwanza ndio uchomwe mpaka kufa.,

kabla raisi wa mbinguni ambaye ni mkombozi atakachokifanya muda mfupi kabla ya zoezi la kuwafufua wafu na kuwafanyia interview

assume siku ya tukio ni mwaka 2021 december. Wale watakao kuwepo siku hiyo wataungana na watakaofufuliwa kwenye kufanyiwa interview ya kuingia katika nchi yenye asali na maziwa na bata zote

Hiki ndicho kinachofanya watu tunasali usiku na mchana ili tupate tiketi ya kuingia mbinguni.​
 
Hii nadharia ilianzia huko nchini israel walikuwa kila wakipigana vita hawashindi, sababu waliamini kuwa wanashindwa vita kwa sababu ya matendo yao mabaya hivyo basi wakaanza kuamini kuwa mkombozi wao atakuja kuwakomboa endapo watatenda mema, na huyo mkombozi wao waliamini ananguvu zisizo za kibinadamu na ndiye atakaye kuja kuwa mfalme wa israel,

Baada ya ujio wa yesu na matendo yake mema na ya kijasiri ya kutokuogopa chochote, raia wengi wakaanza kuamini kuwa huyo ndiye mkombozi wao aliyetabiliwa, kumbuka wakati huo israel ilikuwa chini ya utawala wa kirumi yaani raia wote ni mateka wanaitumilia serikali ya warumi,

Basi taarifa zikamfikia kiongozi wa kirumi hapo israel aliyekuwa akiitwa HERODE (jina silikumbuki vizuri) herode akaona ampasie kesi PONSIO PILATO, huko yesu akahukumiwa kuteswa mpaka kufa,

Kumbuka nchi nzima walikuwa wanaamini yesu ndio mkombozi wao na walijua hatakufa maana ndiye aliyetabiliwa,

Baada ya yesu kuteswa na kufa wakawa suprised kwamba mbona amekufa? Maana yake sio yeye aliyetabiliwa!

Basi hapo ndipo alipoibuka jamaa mmoja aitwaye PAULO, huyu akaja na nadharia kuwa mkombozi aliyetabiliwa ni huyo huyo yesu aliyekufa, ila kilichokufa ni mwili na tayari amekwisha enda ktk nchi itwayo mbinguni huko ili mtu aende inabidi afe kwanza kisha siku ya mwisho atafufuliwa na kwenda huko, ila kikubwa matendo ya mhusika yawe mema ndio tiketi yake ya kuingia huko. Waisrael wote wakaanza kuamini hivyo kuwa mkombozi wao ndio yesu na wao watamfuata huko kwenye nchiaa ya mbinguni.​
 
Kumbuka wakati huo utawala wa kirumi ulikuwa na makoroni mengi kuanzia hapo israel, misri, uturuki, ugiriki, italy (head quarter) n.k na dini yao ilikuwa ni ya kuabudu miungu,

Kiongozi mkuu wa tawala za kirumi akaamua dini ya kikristo (imani ya waisrael) ndio iwe dini official kwenye empire zote za kirumi yaani kuanzia italy, ugiriki, israel, uturuki mpaka misri,

Baadae ukristo ulisambazwa na wamisionari
 
Hilo gereza lipo nchi gani na ukishachomwa moto na kufa maiti yako itazikwa au kutupwa wapi??
Utafungwa minyororo miaka 1000 nilikosea nmerekebisha,

Chanzo cha taarifa kasome biblia
 
Hiyo minyororo unafungwa katika sehemu gani ya mwili na unafungwa minyororo ukiwa katika nchi gani na hiyo minyororo ni aina gani na usipofungwa hiyo minyororo inakuwa vipi???

Je huko kuna msosi??
 
Kamuulize aliyeandika biblia
 
Ungetumia sayansi walau tungeanza kuamini tatizo untumia biblia ambayo ni imani tayar. Kun watu hatuiamn biblia
 
Habari wakuu,

Huu mjadala ni mpana sana na upo tangu miaka mingi sana, nitaeleza nadharia ya uwepo wa mbingu na Mungu jinsi ulivyoibuka, nitatumia mifano ya sasa na ya kale ili niweze kueleweka,

Nitaanza na concept ya mbingu. Fikiria maisha jinsi yalivyo magumu, fikiria changamoto za kimaisha unazopitia mfano huna ajira, huna shughuli yeyote, biashara ngumu, huna uwezo wa kununua chakula, unaumwa huna pesa ya kwenda lutibiwa hospitali, umebambikiziwa kesi na wanasiasa, hujapata mtoto, umelima mazao yamepigwa ukame hakuna utakacho vuna, umepata msiba wa mtu unayempenda kafariki ghafla n.k majanga ni mengi

Kumbuka upo Tanzania, bara la Afrika sayari ya tatu iitwayo dunia wengi mnaiita duniani,

Sasa unaambiwa kuna nchi inaitwa mbinguni lakini haijulikani ilipo, Raisi wa hiyo nchi ni mungu, mawaziri ni malaika na kwenye hiyo nchi hakuna changamoto zozote za kimaisha yaani vyakura vipo vya kutosha, mazingira ni mazuri, kuna bustani nzuri, kuna hewa safi, hakuna magonjwa na ukiwa huko hauwezi kufa, huitaji ajira wala kufanya biashara ili uweze kujikimu yaani bata zote ni bureeee ,

Lakini ili uingie kwenye hiyo nchi ni lazima ufe kwanza kisha siku ya mwisho utafufuliwa utafanyiwa interview kwa kuangalia experience ya matendo yako, kama ulitenda mema utaingia huko kama ulitenda mabaya hutaingia kwenye nchi ya mbinguni yaani bata utazisikia tuu na utapewa adhabu ya kuchomwa moto na kufa mara ya pili ila inasemekana kabla hujachomwa utafungwa minyororo miaka elfu moja kwanza ndio uchomwe mpaka kufa.,

kabla raisi wa mbinguni ambaye ni mkombozi atakachokifanya muda mfupi kabla ya zoezi la kuwafufua wafu na kuwafanyia interview

assume siku ya tukio ni mwaka 2021 december. Wale watakao kuwepo siku hiyo wataungana na watakaofufuliwa kwenye kufanyiwa interview ya kuingia katika nchi yenye asali na maziwa na bata zote

Hiki ndicho kinachofanya watu tunasali usiku na mchana ili tupate tiketi ya kuingia mbinguni.​
Unajuaje kama na mimi nina mawazo kama yako?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom