Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Execute

JF-Expert Member
Sep 21, 2022
3,000
7,285
Huyu jamaa ni mtu wa dua na maombi lakini anasema hakuna Mungu. Ninaamini alipitia changamoto za kimaisha hadi akamchukia Mungu lakini deep down anafahamu uwepo wake.
Scars

Watu tu wanashindwa kuwa waungwana

Mimi kwenye mechi yenu na Medeama niliomba dua msifungwe.

Na kweli mechi ikaisha hamjafungwa matokeo yake tulioonekana tunafurahi matokeo ya aina ile tukaitwa hater.

Yani haijalishi ni kwa kiasi gani unakuwa humble kwa mwingine ila mtu akiamua kuku maindi atakuita tu we ni hater.

Tuendelee kudumisha utamaduni wetu kwa kuombeana mema.
 
Nadhani mkuu wewe umekurupuka. Akisema haamini uwepo wa mungu ungemuuliza anaamini uwepo wa nini?

Pili hapo kwenye hiyo comment yake hajamtaja mungu popote. So kuomba kwake dua ungemuuliza anaomba dua kwa nani na sio kumsingizia kuwa amemuomba mungu.

Pia unatakiwa useme kama dua linaombwa kwa mungu tu au kila mtu anaomba dua anapopaamini. Je anaefanya tambiko kwenye mti au mlima nakufanya dua zake anaomba kwa mungu?
 
Pia unatakiwa useme kama dua linaombwa kwa mungu tu au kila mtu anaomba dua anapopaamini. Je anaefanya tambiko kwenye mti au mlima nakufanya dua zake anaomba kwa mungu
Mungu yoyote yule ni nafasi au cheo kinachopewa yule anayeabudiwa. Hivyo huo mti pia ni mungu ndio maana nchi za Asia wana miungu ambayo wameitengeneza wenyewe kwa mikono yao na wanaiabudu.
 
Huyu jamaa ni mtu wa dua na maombi lakini anasema hakuna Mungu. Ninaamini alipitia changamoto za kimaisha hadi akamchukia Mungu lakini deep down anafahamu uwepo wake.
Scars
So Scars kutumia neno dua maana yake anaamini Mungu?

Maana yake na mimi nitakuwa sahihi kusema hata Wakristo na Waislamu watakuwa wanaabudu Miungu ya kigiriki iwapo tutabaini kuna maneno fulani yamayopingana na dini zenu mkiyatumia?

Kwasababu wamekuwa wakitaja miezi ya mwaka kwa kuiita Januari ambapo kimsingi Januari ni jina la Mungu wa kigiriki aitwaye Janus.

Au niseme mnaabudu miungu ya kirumi kwasababu mmekuwa mkiita mwezi wa tatu "March" wakati hilo ni jina la Mungu wa kivita wa kirumi?

Vipi kuhusiana na siku za wiki Monday, Tuesday, Wednesday, Friday, Thursday, Saturday hadi Sunday ambaye ni Mungu jua?

Hujui kwamba hiyo ni Miungu?

Kwahiyo tunapokuona ukitamka tusemeje sasa? Tuseme unatamka hayo maneno kwasababu unaamini hiyo Miungu?

Au tuseme na nyie mnatuektia kusema mnaamini Mungu na wakati tunawaona mnatumia Dollar ya marekani ambayo ina chata ya kishetani ambayo imeelezwa kwenye vitabu vyenu?


****************************
Kujibu swali lako

Kwa bahati mbaya unaonekana kushindwa kuelewa baadhi ya maneno yana double meaning kwa kuchukua maana ile iliyo kaririwa ambayo imekuwa ikitumika sana kimazoea

Neno dua linaweza kuwa na maana nyingine na kutumika kama "wish" au "hope"

Kumtakia mtu heri ya jambo lolote linaloenda kufanyika mbele hiyo sio dua kwa mtazamo wa kidini ni jambo la kiutu katika morality

Lakini kama upo katika circle ya udini lazima uwe na perception ya tofauti unaweza kusema ni dua

Kwa hiyo hayo ni maswala tu ya utata wa maneno hususani pale inapotokea neno kuwa na maana zaidi ya moja huku maana fulani ndio ikiwa inatumika kimazoea kwenye jambo fulani.
 
"Ulisema uliomba Dua" dua ulimuomba Nani?
Nikikuambia shambani kwangu mi nina panda

Hapo nitakuwa nimemaanisha nini?

Utakuwa umepata tafsiri gani?

Nitakuwa nimemaanisha nimepanda mmea yani "planting"?

Au nimemaanisha nimepanda mti kwa kuukwea juu yake yani "climbing"?

Au nitakuwa nimemaanisha shambani kwangu namiliki mnyama huyu aitwae panda?

1702657168240.png


Hapo utaenda na jibu gani? Na lina takiwa moja
 
Nadhani mkuu wewe umekurupuka. Akisema haamini uwepo wa mungu ungemuuliza anaamini uwepo wa nini?

Pili hapo kwenye hiyo comment yake hajamtaja mungu popote. So kuomba kwake dua ungemuuliza anaomba dua kwa nani na sio kumsingizia kuwa amemuomba mungu.

Pia unatakiwa useme kama dua linaombwa kwa mungu tu au kila mtu anaomba dua anapopaamini. Je anaefanya tambiko kwenye mti au mlima nakufanya dua zake anaomba kwa mungu?
Yani watu wanataka tushindwe kutumia maneno yaliyokuwa na maana nyingine kabla ya dini kwasababu saizi yamemilikiwa na dini kimazoea hivyo tukionekana kuyatumia wanaanza kutu accuse kuwa sisi na wao tupo kitu kimoja

Ni sawa na rainbow color kabla ya mashoga kuiweka kwenye nembo yao. Ilikuwa ni rangi nzuri iliyokuwa ikiwakilisha mambo mema tu.

Ila saizi imejenga tafsiri mpya ukionekana umevaa nguo yenye rangi za rainbow watu watasema ni shoga.

Sasa swali la kujiuliza je ni kweli rainbow maana yake ni ushoga au ni mazoea ya watu kutokana na kuona mashoga wanatumia rangi hizo?
 
Back
Top Bottom