Je, Anthropic principle Inathibitisha uwepo wa Mungu?

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
6,817
11,542
Kimsingi, kanuni ya anthropic ni dhana inayosema kwamba hali yetu ya kuwepo ulimwenguni inategemea hali maalum ya ulimwengu wetu.

Dhana hii inaamini kuwa ulimwengu wetu umetayarishwa kwa njia maalum ili kuwezesha kuwepo kwa maisha. Kwa mfano, inasemekana kuwa sheria za kisayansi zilizopo zimetengenezwa kwa namna maalum ili kufanya uhai uwezekane.

Thamani ya hizi constants (Spidi ya mwanga, π, uzito wa electron, nk)ingebadilika kidogo tu hata kwa desimali moja ya 0.00000000000001 basi maisha yasingetokea kwenye huu ulimwengu na sisi tusingekuwepo.
  1. Kasi ya nuru (speed of light): Hii ni kipimo cha kasi ambacho nuru inasafiri. Iwapo kasi hii ingekuwa tofauti kwa hata kidogo, uwepo wetu kama binadamu na hata maisha yenyewe yasingewezekana.
  2. Msuguano wa gravitational (gravitational constant): Hii ni kipimo cha kiwango cha nguvu ya graviti inayovuta vitu kwa pamoja. Kama msuguano huu ungekuwa tofauti kwa hata kidogo, uwepo wa sayari, nyota na ulimwengu wote usingewezekana.
  3. Kiwango cha oksijeni (oxygen level): Kiwango hiki cha oksijeni katika anga yetu ni muhimu sana kwa uhai. Iwapo kiwango hiki kingekuwa cha juu au cha chini sana, uwepo wa uhai usingewezekana.
  4. Mwelekeo wa Dunia (Earth's axial tilt): Mwelekeo huu unahusiana na mzunguko wa Dunia kuzunguka jua na unachangia katika kuwezesha uwepo wa maisha duniani.
  5. Kiwango cha utando wa ulimwengu (cosmological constant): Kiwango hiki kinahusiana na kiwango cha upanuzi wa ulimwengu na iwapo kiwango hiki kingekuwa tofauti kwa hata kidogo, uwepo wa maisha duniani ungewezekana
Kanuni ya anthropic inaamini kwamba kama hali ya ulimwengu wetu ingekuwa tofauti, basi hatungekuwepo sisi kama binadamu au maisha yoyote kwa ujumla. Dhana hii inaamini kuwa sheria za kisayansi na hali ya ulimwengu wetu zinaakisiwa na uwepo wetu, na kwamba uwepo wetu unategemea hali maalum ya ulimwengu wetu.

Kwa hiyo, kanuni ya anthropic ni dhana inayotumika kuelezea kwa nini ulimwengu wetu unafaa kwa uhai. Inaamini kuwa ulimwengu wetu umetayarishwa kwa njia maalum ili kuwezesha uwepo wetu, na hali ya ulimwengu wetu imechangia sana katika kuleta uhai uliopo.

Baadhi hutumia hii principle kuonesha kuwa Ulimwengu haukutokea kwa ajali au bahati bali kuna mpishi aliyekaaa akaandaa viungo na kuupika ulimwengu ili maisha yawepo, ambaye mpishi huyo ni Mungu.
Ndiyomaana constants nyingi kwenye ulimwengu ni perfectly fine tuned ili kusapoti maisha

Lakini wengine hupinga kwa kutoa hoja kama zifuatazo
  1. Multiverse Theory: Wapinzani wa nadharia ya fine-tuning wanadai kuwa kuna uwezekano wa kuwepo kwa ulimwengu mwingine mbali na wetu, na kwamba uwepo wa hali maalum kwenye ulimwengu wetu unaweza kuwa ni matokeo ya bahati tu. Hawa wanasema kuwa kuna uwezekano kuwa kuna ulimwengu mwingine ambao hauwezi kuwepo uhai.
  2. Ufahamu Wetu Ulio Hafifu: Wanasayansi wengine wanasema kuwa tunafahamu kidogo sana kuhusu ulimwengu wetu na kwamba vipimo vyetu havitoshi kuweza kuthibitisha nadharia ya fine-tuning. Wanadai kuwa huenda kuna mambo mengi zaidi ambayo hatufahamu na ambayo yanachangia katika uwepo wa maisha.
  3. Bahati: Wengine wanadai kuwa uwepo wa maisha ni matokeo ya bahati tu na kwamba hakuna haja ya kufikiria uwepo wa nguvu ya kubuni ulimwengu.
  4. Nadharia zingine: Wapinzani wa nadharia ya fine-tuning wanaamini kuwa kuna nadharia zingine ambazo zinaweza kutoa maelezo ya uwepo wa uhai duniani, kama vile nadharia ya evolution.
Hizi ni baadhi ya hoja ambazo zinatolewa na wapinzani wa nadharia ya fine-tuning. Hata hivyo, wanaounga mkono nadharia hii wanadai kuwa vipimo vya asili vinatoa uthibitisho wa kutosha kuwa ulimwengu wetu umetayarishwa kwa njia maalum ili kuwezesha uwepo wa uhai. Wanaamini kuwa uwepo wa hali maalum kwenye ulimwengu wetu sio matokeo ya bahati, bali ni matokeo ya nguvu ya kubuni ulimwengu
 
Ukweli ni kwamba, Anthropic principle haina uhusiano wowote na uwepo au kutokuwepo kwa Mungu. Ni nadharia ya kisayansi inayoeleza hali ya kipekee ya ulimwengu tunamoishi.
Uhusiano unaonekana pale inapofikika kuwa jinsi constants mbalimbali zisizo na uhusiano zenyewe kwa zenyewe zimeunganishwa kutengeneza uhai ambapo mojawapo ingekosewa kidogo tu basi uhai usingekuwepo, hiyo inaashiria kuna outside force/intelligent design iliyohusika katika kuuandaa ulimwengu tunaoishi
 
Kwa kila kilichopo ndano ya hii Dunia nyuma Yake Kuna nguvu( supreme being) ambayo iliwezesha kila kitu kuwa katika Hali Yake.

Huko angani Kuna mpangilio maalum wa nyota,Mwezi na jua.Nyota zimewekwa kwa mfumo ambao unazizuia zizigongane na Mwezi usigongane na jua.
 
Allahu akbar
 
Na mie naomba kuchangia,
Hizi nadharia za kisayansi sio za ukweli zote wala hazithibitishi uwepo wa mungu badala yake ndio zinatupotosha na kutuchanganya na kutujengea akilini mazingira ya uncertainty yaani kutokuwa na uhakika na kitu chochote na tusiweze kuthibitisha kitu chochote.

Tuanze hapo kwenye points zako tano za thamani ya constants
1) Mwangaza:
mwangaza hauna kasi yeyote wala hausafiri kutoka sehemu moja kwenda nyengine mwangaza una nguvu, yaani ni kama smaku mwangaza ni hivyovyo, hatupimi smaku kwa speed yake ya kuvuta kitu ila tunapima kwa nguvu zake
Mwangaza una field of energy kama ilivyo magnetic filed of energy, kwa hio kwa mfano ukiwasha taa mwangaza unajaa katika field of energy yake kisha unaisha hapo hapo, hauwezi kusafiri na kutoka nje ya field of energy yake, na smaku ni hivyo hivyo.
Hii dhana ya kuwa mwangaza unasafiri imejengwa kwa sababu ya kuaminishwa kua jua lipo umbali wa 53 mil km, ndio tunaambia mwangaza unasafiri Masada hayo mpaka hapa duniani kwa dakika nane, uongo mtupu,
kaa kwa makini ufikirie umbali wa 53 mil km kama akili yako itaweza kupata jawabu au kama macho yako yanaweza kuona kitu kilicho zaidi ya km laki mbili, kumbuka dunia nzima wanasema ina circumstance ya km 25 alfu.

2) gravitational forces
Huu uongo mwengine, gravity ni theory na haijawahi kuthibitishwa uwepo na haitawahi kuthibitishwa kwa sababu ni jambo la kutunga haliwezi kuwa halisi na kuthibitishika.
Hii dhana ya gravity kuzuia nyota zote,mwezi , watu wote, bahari nzima,majumba yote na kila kitu duniani na nje ya dunia ambapo uzi to wake vitu hivi havina mfano, lakini hii gravity inashindwa kulizuia bofu lisipae angani, ndege wanaruka kwa uhuru na ndege zinazoruka angani zimeweza kujengwa na nguvu za kuishinda gravity,
Kama utafikiria kwa makini na kama gravity ni ukweli basi vitu vizito ndio vingekuwa vinaelea hewani kwa sababu gravity ingetakiwa kutumia nguvu kubwa kuvizuia vitu vizito chini,na vitu nyepesi ndio vingenasa kwenye gravity haraka sana bila ya nguvu kubwa,lakini matokeo yake ni vise versus vizito vinaganda ardhi ni na vyepesi vinaelea,dunia haina gravity ina electro magnetic forces ambayo ina balance kila kitu. Na hii electro magnetic force inasababishwa na mzunguko wa jua na mwezi, jua ni positive na mwezi ni negative na dunia ni earthing. Au kwa maana nyengine jua ni proton, mwezi ni electron na ardhi ni neutron,ndio maana ukiona radi na mimweso inapiga mwisho wake unaisha ardhini kwa sababu ardhi haina charge ni neutral na radi ni electric charge kwa hio ina-release kwenye neutral
Ya 3 ntaruka ina uhalisi
4)earth axial tilt na mzunguko wa dunia.
Hiki ni kichekesho yaani level ya ujinga tulojengewa binadamu imefikia viwango vya hatari sana ya kuweza kukubali utoto wa aina hii.

Dunia haina axial tilt, wala haizunguki na haina motion ya aina yeyote, wala sio duara wala haielei hewani, dunia nzima hakuna mtu Anajua dunia ni kitu gani kiuhalisia, wala ipo wapi wala ipo lini na wakati gani,vitu hivi havijulikani na binadamu yeyote,
hao ambao wanatulazimisha tufahamu wanayotaka wao wanatuandikia vitabu na kutuaminisha na kutujengea uhalisi wa vitabuni, na sio uhalisi wa kweli.
Ifikirie kwa makini uhalisi wa dunia kuzunguka kwa 1000 mph ifikirie hio speed na sisi binadamu na wanyama wote, bahari kuganda kwenye mgongo wa dunia,ndege zinazoruka angani,
Eti ni constant ndio mana hatuihisi,mtu akishakugeuza msukule hatumii nguvu kubwa kukudanganya wala hatumii tena nguvu kukutawala,atakwambia jambo la kijinga tu na utaamini kila kitu, sababu akili zetu washaziharbu zote na hazina nguvu zake za asili.
Mie bora niishie hapa kwa sasa
Pengine ntarudi tena baadae
Ila tu nijibu kitu kimoja, uwepo wa mungu hauhitaji udhibitisho wa vitabu vya science wala hauhitaji uthibitisho wa vitabu vya dini.
Uhai wetu ni uthibitisho,nature yote ni uthibitisho na mengi mengineyo yanathibitisha bila ya kuambiwa wala kufundishwa na mtu
 
Wow these are some very wild theories.:rolleyes::rolleyes:

Nipo interested kukuelezea kwa kina Zaidi jinsi Hivyo vitu unavyovipinga vinafanya kazi, lakini ninadoubt kwamba utakuwa open minded enough kunielewa.

Kitu ambacho nachoweza kusema kuhusu vitu vyote Hivyo na hayo mafundisho yote ya kisayansi na kwanini nayaamini ni kwamba;
Historically speaking science works.

Kupitia hizo Imani unazoita ujinga, wanasayansi wanatengeneza roketi,umeme,mabomu,stallite,meli nk.
Wewe unasemaj hakuna gravity ila wao wanatumia formula za gravity kutengeneza rocket, wew unasema mwanga hausafiri ila wanatumia speed ya mwanga kwenye calculations za kutengeneza atomic bomb nk. nk.

Kwahyo kama tunaongelea strictly practicability na applicability ya hizi Imani kwenye real world. Sayansi ni namba moja.
 
Science ina mambo mengi mazuri imefanya uvumbuzi na uchambuzi wa vitu vingi,hii haimaanishi kuwa kila kitu science ikisema ni ukweli,
Katika kueleza hali halisi na uhalisi wa kitu ukitafuta jawabu kupitia science utaishi maisha yako yote in a dream-like state of mind, na hutawahi kujua uhalisi wako mwenyewe na uhalisi wa kitu chochote kilicho natural duniani, dunia, bahari,maji,miti anga,mwezi,jua,nyota,life,time nk, hivi vitu hutaweza kuvijua uhalisi wake kupitia science,kikubwa science itakujengea ideas za uhalisi wa kila kitu akilini na haitakuwa uhalisi wa kweli na hutaweza ku-disapprove
 
Back
Top Bottom