Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Watu wanazungumzia muundo wa serikali nyie mnalingalisha na chama ambao viongozi wake wanachaguliwa kwa uchaguzi? Sie tunahoji teuzi mbali mbali ambazo mamlaka yake yako kwa mtu mmoja na hahojiwi na yeyote na anapaswa kujali Utanzania tu.

Halafu Chadema kimekuwa kioo cha serikali kiasi kuwa kila kitu ikihojiwa serikali mnakimbilia kuuliza huko Chadema hili au lile mnafanyaje? Hivi mshaona mtu anahangaika na muundo wa CCM ukoje? Hayo ni yenu huko ndani hayawahusu wasio wanaccm. Ndio maana hata wale viongozi wenu vijana wa UVCCM ambao kesho ndio wa ccm hakuna mwenye habari na zile tabia zao za kwenda mapumzikoni Mombasa.

Mtajijua wenyewe kama wanaenda huko au mtaamua kuwashughulikia wenyewe.

Muundo wa chama sio suala la kitaifa bali muundo wa Serikali ni jambo la kitaifa linalowahusu watanzania wote
 
Mbowe-m/kiti-Kaskazini
John mrema-mkurugenzi wa bunge-kaskazini
John mnyika NKM-Kaskazini
Joseph selasini-Mkurugenzi wa mifeza-kaskazini
Sumaye-Kamati kuu-Kaskazini
Lema-kamati kuu kaskazini
Lowassa-mwenye chama-kaskazini
Ole sosopo-kaskazini
Grace kiwelu-viti maalum-kaskazini
Rose kamili-viti maalum-kaskazini
Hlf ukiangalia vzri si ajabu utakuta wote ni walutheri....
 
Zitto anawachora sana hawa jamaa. Balozi wa Japan na Zitto wamekuwa pamoja Kigoma kwa karibu siku tatu.

Kilichowapeleka ni kuangalia namna gani mkoa ule unaweza kufunguka kwa maana ya fursa kuzifikia dunia nzima.

Zitto anayo mawazo ya kuigeuza Kigoma kuwa tourist destination nyingine ya Tanzania. Hivyo wanavyomtukana mitandaoni, yeye anawacheka kimoyomoyo.

Ndio maana kamfananisha Lissu na zwazwa, kwa sababu yeye Zitto anaitazama dunia katika mtazamo wa kimaendeleo, halafu anashangazwa na mtu ambaye anawazia demokrasia kuliko maendeleo.

Jimbo la uchaguzi la Zitto Kabwe litakuwa tofauti sana kimaendeleo kulinganisha na jimbo la Tundu Lissu, ndani ya miaka minne au mitano ijayo.
Idadi ya kesi walizoshitakiwa na idadi ya siku walizoingia lockup kwa makosa ya kipumbavu....matusi....uchochezi nk ndo mtaji wao wa kisiasa!kazi majimboni mwao wameshasahau!tusubiri 2020!zitto hakukosea kumuita yule jamaa punguani.....hayawani!
 
Wadau na wanaJF kwa mwenye safu au orodha ya uongozi wa chadema atuwekee hapa ili tuiangalia kama haina udini,undugu,ushemeji au ukanda.

UPDATE 1
Tuanze na Wenyeviti wa Chadema
Sasa Hapa unataka kusema nini? Kwamba kama kunaudini,ukabila au undugu ndo turuhusu nchi yetu iwe hivyo? Mbona watu wengine mnakuwa malofa na wapumbuvu kuliko wale aliowasema Hon.Mkapa,Nani analazimishwa kuwa mwanachama wa Chadema na mambo yao,otherwise use me wewe ni jinga kweli kama kuna lako lilivyo
 
Wadau na wanaJF kwa mwenye safu au orodha ya uongozi wa chadema atuwekee hapa ili tuiangalia kama haina udini,undugu,ushemeji au ukanda.
Mkuu jinga lao,sitaki kuamini kuwa "user name" yako inaakisi uelewa wako! Naamini wewe ni mwelevu zaidi ya hiyo user name.Chadema wawe wakanda,wakabila,wanaukoo au vyovyote walivyo hiyo si hoja,ukanda,ukabila,undugu,ushemeji na unyumba wao ni fursa kwa watanzania kuufahamu ulaghai wao!

Watanzania wa leo hawasubiri kuambiwa "tazama kule,muone yule", wanayatazama mambo kwa marefu na mapana yake. Kama chama cha siasa kimejikita katika hayo uliyoyasema,nafikiri kitakuwa kimewapunguzia kazi watanzania na hawatakuwa na shida ya kuhangaika nacho!

Kwa miaka mingi ccm na serikali yake waliitumia fursa ya ukanda,ukabila na udini kama siraha ya kupambana na washindani wao kisiasa,walifanya hivyo kwa CUF na wakafanya hivyo kwa Chadema.Siku zinaenda kasi mno, leo hii ile silaha waliyoitumia kuwaanfamiza washindani wao, imegeuka na kuanza kuwaangamiza wenyewe!

Hata kama ukweli haukirwi hadharani,harufu za ukanda,udini na ukabila zimeanza kusikika ndani ya pua za wapenda umoja na Mshikamano.Sasa hata ndani ya chama minong'ono ya ukanda na ukabila inasikika kila kona.Udugu unalinyemelea kwa kasi taifa letu,haya si mambo mepesi kuyajadili lakini acha tufungue vinywa ili vifua vipunguze uzito wa hoja nzito vilivyobeba, ukweli ni kwamba sasa chama chetu na serikali yake kimeanza kufuata mkondo uleule tuliowaaminisha watanzania kuwa si mkondo sahihi,sasa kuna ukanda,undugu,ukabila na udini ndani ya chama na serikali yetu tukufu!

Tuwaache Chadema na wenzao wajikite kwenye hayo,ili sisi turudi kwa wananchi na kuwaeleza ubaya wa Sera zenye mlengo huo,lakini kama nasi tumeiacha silaha yetu tuliyoitumia kuwaangamiza washindani wetu na sasa tumeamua kujiangamiza wenyewe kwa silaha ileile,basi tuache unafiki wa kuwaona wenzetu wakanda, wakabila na wadini, huku nasi tumeyageuza hayo kuwa kigezo kikuu katika "vetting" ya viongozi wetu, ahsante.
 
Wadau na wanaJF kwa mwenye safu au orodha ya uongozi wa chadema atuwekee hapa ili tuiangalie(kwa jicho la lissu) kama haina udini,undugu,ushemeji au ukanda.

UPDATE 1
Tuanze na Wenyeviti wa Chadema

Chadema siyo nchi ni chama, mbona mmekuwa na mtazo wa kitoto kulinganisha chama na nchi?
 
Watu wanazungumzia muundo wa serikali nyie mnalingalisha na chama ambao viongozi wake wanachaguliwa kwa uchaguzi? Sie tunahoji teuzi mbali mbali ambazo mamlaka yake yako kwa mtu mmoja na hahojiwi na yeyote na anapaswa kujali Utanzania tu...
Unajenga ukuta kulinda uovu wa chama chako. Chama chenye wabunge zaidi ya 100, madiwani kibao, na kinaomba ridhaa ya kuongoza dola kikiwa na mambo ya ovyo kisihojiwe!

We unafikiri watu ni mbumbumbu. Kwa fikra kama yako ndo maana mnashindwa kumuhoji mbowe kwa nini kamleta EL kugombea urais ilhali ni fisadi papa na ni makapi toka ccm, ama kwa nini anakua m/kiti wa maisha tofauti na spirit za awali za chama chenu.
 
Bob Nyanga Makani ni mmoja wa waasisi wa CHADEMA, ni Msukuma, Mwislamu kutoka Kutoka Shinyanga na katibu mkuu wa Kwanza wa CHADEMA...
Bob Makani Msukuma lakini mkewe mchaga na dada wa Mkiti. Tusidanganyane hapa!
 
Natoa tu tahadhari.

Zamani ilisemwa Chadema ni chama cha kaskazini ( wachagga) kwa kuwa wanachama wake wengi pamoja na viongozi walitokea upande huo wa Moshi - Arusha.

Lakini alipokuja mzee Lowassa Chadema ikabahatika kuingiza watu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania na hivyo ile dhana ya ukanda na ukabila ikafutika.

Kwa sasa tumeshuhudia wanachadema kutoka mikoa karibia yote na hata Arusha wakihamia CCM, ni Kilimanjaro pekee upande wa Moshi na Rombo ndio bado wana imani na Chadema.

Chadema chukueni tahadhari Tafadhali.

Kazi Iendelee!
 
Back
Top Bottom