Dhana ya Mlango wa 8 kama wamaanishavyo Waswahili

Dhana ya Mlango wa 8 kama wamaanishavyo Waswahili

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,708
Reaction score
1,733
Wakuu,

Naomba kufahamu nini maana ya mlango wa 'nane'. Hii imekuja baada ya dada mmoja kutaka kumfahamu bosi wake kama ni mlango wa nane, nilipomuuliza ana maana gani alinishangaa sana.

Pamoja na kufahamu maana ya mlango wa nane pia nitafurahi pamoja na milango mingine kwa idadi na maana yake.

Disclaimer:
Mimi nilikaa darasani kujifunza elimu ya nyota (Astrology) lakini si-practice na wala siiamini. Hapa nitakumegea kidogo nilichojifunza.

Katika utabiri wa nyota (Astrology) kuna nyumba au milango 12 jumla (au kwa kizungu zinaitwa HOUSES).

Hii milango inashabihiana na zodiac signs (makundi ya nyota kwenye njia ya jua au ecliptic kama vile Virgo (Mashuke), Leo, Scorpion, nk.)

Sasa wakati unapozaliwa ile nyumba (au mlango) ambao jua ndipo lilipo, kwa mfano Germini (au mapacha) ndio mlango wako wa kwanza (First House). Mlango huu wa kwanza unakupa personality yako. Sayari na mwezi (hasa mwezi) zilivyojipanga kwenye huu mlango wako wa kwanza ndio una-finetune hiyo personality yako (mtu wa aibu au machachari au mpendwa na watu burebure tu, nk.)

Hii milango (houses) ni hii

Aires, Taurus, Germini, Cancer, Leo, Virgo, Libra, Scorpion, Sagittarius, Capricorn, Pisces, Aquarius

Sasa kwa mfano: Kama umezaliwa chini ya nyota (Mlango, au house) ya Germini, basi

Germini ni mlango wako wa kwanza
Cancer ni mlango wako wa pili
Leo ni mlango wako wa tatu
.
.
Capricorn ni mlango wako wa nane
.
.
Taurus ni mlango wako wa kumi na mbili

Kila mlango unatawala kitu fulani maishani mwako (kama ulivyo mlango wa kwanza kutawala personality yako)

Sasa mlango wa nane unatawala uzazi na kifo. Lakini huu ndio mlango ambao, kutegemea ni sayari gani zilikuwepo kwenye huu mlango na zilijipangaje wakati unazaliwa unaweza kukufanya uwe na bahati au mikosi.

Kwa hiyo watu wakisema kuwa mtu huyu ni wa mlango wa nane wanamaanisha kuwa mipangilio wa sayari na mwezi kwenye mlango wake wa nane wakati anazaliwa umempa haiba ya nuksi, mikosi, bahati mbaya, na si mtu wa kushirikiana nae kwa sababu atakuangamiza.

Hapa chini nitaweka link itakayokueleza hii milango (Houses) na ni mambo gani yanatawaliwa na hii milango.

Enjoy.

The 12 Astrological Houses: their Meaning

Nnavyofaham mm ni kwamba huwa ni watu wenye kelele xana na huwa hawatulii,ukiambiwa yule mwanamke ni mlango wa nane hafai kuoa atakusumbua mpaka ujute kwann ulioa
Poa mkuu. Je kuna idadi rasmi ya milango hiyo na maana yake?
 
Hili kwangu ni geni sana wajuzi wafafanue vyema tupate kuelewa
 
Ni watu ambao wanawake zao hawaolewi nje ya ukoo wao kama vile
Kwa wachagga ni wamachame
wapare ni washana
Tanga ni wabondei
Kama wewe hutoki katika makabila hayo tajwa basi usije ukaoa kwenye hao niliyowataja. Hutapata amani na mafanikio maishani mwako. I stand to be corrected.
 
Hayo ni mambo ya kishirikina ktk suala la nyota, yaani wataalam wa mambo ya unajimu wanawagawanya watu ktk milalango mbali mbali, na nilipata kuskia mtu wa group hilo, (mlango wa nane) huwa anatajwa km mtu wa mikosi sana
 
Mie hao ndiyo nawataka na hasa kama ni MZIGO wa maana kwani kila nikifika sehemu basi kila mtu atatuona na kuanza kutoa mate jinsi ZIGO lilivyobeba na wote wanabaki kunionea WIFU kuwa "Jamaa linafaidi AROO!!!!"

Hivi Wamakonde nao wamo? Makonde wanafujo na SHOW OFF ya maneno kila walipo. I Love you Makonde girls.

.......ukiambiwa yule mwanamke ni mlango wa nane hafai kuoa atakusumbua mpaka ujute kwann ulioa
 
haki ya Mungu!!

nijuavyo mimi! mlango wa nane ni natoa mfano:

unaweza kuwa na msichana wa kazi au mke, lakini akishika sahani kavunja, akishika chupa kavunja, akipikia jiko la gesi siku mbili mara limeharibika, rimoti zimepotezwa betry, sofa limeunguzwa au lumechanwa, yaani mlango wa nane hauna maendekeo zaidi ya hasara.
 
Mie hao ndiyo nawataka na hasa kama ni MZIGO wa maana kwani kila nikifika sehemu basi kila mtu atatuona na kuanza kutoa mate jinsi ZIGO lilivyobeba na wote wanabaki kunionea WIFU kuwa "Jamaa linafaidi AROO!!!!"

Hivi Wamakonde nao wamo? Makonde wanafujo na SHOW OFF ya maneno kila walipo. I Love you Makonde girls.

Love you too......UTUWACHEEE lakiniii
 
Ni watu ambao wanawake zao hawaolewi nje ya ukoo wao kama vile
Kwa wachagga ni wamachame
wapare ni washana
Tanga ni wabondei
Kama wewe hutoki katika makabila hayo tajwa basi usije ukaoa kwenye hao niliyowataja. Hutapata amani na mafanikio maishani mwako. I stand to be corrected.

kwa wapare sio washana wa aina zote
wapo washana wa aina nyingi ila inayo tajwa kuwa hivyo ni vala va nyumba nyiru..!!
(Japo huwa swala 'mlang wa kanae' halina mashiko kwa wapare...!!.) kama kuna mpare mwingine anaelewa hii ishu zaidi ya hapo natamani aongeze

cc mshana jr
 
Love you too......UTUWACHEEE lakiniii

nasikia kwenu mnakula panya nahuwa zinauzwa stendi kabisaaa..!!
Ila nawapenda kwasababu moja na ya pekee yani kupitia unyagoni yale mafunzo Duuuh very applicable ... !!!! ngoja niishie hapo..!!
 
haki ya Mungu!!

nijuavyo mimi! mlango wa nane ni natoa mfano:

unaweza kuwa na msichana wa kazi au mke, lakini akishika sahani kavunja, akishika chupa kavunja, akipikia jiko la gesi siku mbili mara limeharibika, rimoti zimepotezwa betry, sofa limeunguzwa au lumechanwa, yaani mlango wa nane hauna maendekeo zaidi ya hasara.

Yes ume eleza vizuri...!! Hata uwe tajiri vipi utafilisika tu...!! Kwa makabila ya tanga wanaita DUSI
 
nasikia kwenu mnakula panya nahuwa zinauzwa stendi kabisaaa..!!
Ila nawapenda kwasababu moja na ya pekee yani kupitia unyagoni yale mafunzo Duuuh very applicable ... !!!! ngoja niishie hapo..!!

Kweli n'jomba, kwetu panya analiwa hadi sasa hivi navyocomment hapa...Analiwa zaidi bara hasa Masasi na Newala...na sababu kuu ni uhaba wa mboga, hamna mito na wako mbali na bahari...

Ukifika Mtwara mjini, Mnazi bay, Msanga Mkuu, Kilambo usijaribu hata kuulizia panya, Huku ni pwani, utapata samaki wa kila aina, huku ulizia pweza, viyokolo, chaza, papa nk

Bout unyagoni....no comment...ila Mtwara raha, apendaye na aje.
 
kwa wapare sio washana wa aina zote
wapo washana wa aina nyingi ila inayo tajwa kuwa hivyo ni vala va nyumba nyiru..!!
(Japo huwa swala 'mlang wa kanae' halina mashiko kwa wapare...!!.) kama kuna mpare mwingine anaelewa hii ishu zaidi ya hapo natamani aongeze
cc mshana jr
Washana zamani ndio walikua wanatengeza zana kama mapanga, majembe, shoka etc ndio maana ya neno kushana.
Hawa washana hawakupenda utaalam wao wa kushana ujulukane kwa watu wengine ili waendelee kuvuna kutokana na kuuza zana kwa wapare wengine, wasambaa na baashi ya wachagga. Ili watu wengine waogope kushana, walihusisha utaalam huu na imani za kishirikina, hivyo watu wa koo nyingine wakawa wanaogopa kuoa au kujichanganya na koo za washana kwasababu ya imani zao za kishirikina. Mpaka leo wapare wachawi wanapatikana kwenye koo za kishana zaidi.

Sijui kama mtoto wa mjini Mshana jr anayafahamu haya..
 
Ni watu ambao wanawake zao hawaolewi nje ya ukoo wao kama vile
Kwa wachagga ni wamachame
wapare ni washana
Tanga ni wabondei
Kama wewe hutoki katika makabila hayo tajwa basi usije ukaoa kwenye hao niliyowataja. Hutapata amani na mafanikio maishani mwako. I stand to be corrected.

Upo sawa!
 
Back
Top Bottom