UZUSHI Deusdedit Kakokonwa TPA akamatwa nyumbani na begi lenye USD 1,625,800

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
ELkeKMCXkAE-y2C.jpg


Kuna madai kuwa Takukuru wameingia nyumbani kwa Kakoko leo ghafla na kumkuta na begi lenye $1,625,800 taslimu baada ya kusimamishwa kazi jana!

Haijulikani hizo alizichota lini, lakini kama ni kweli inawezekana alikuwa akizichota pole pole kwa muda mrefu kidogo na huenda sasa hivi ana 'vijisenti' vingi sana huko Jersey au Switzerland kama yule mzee.


Mkurugenzi wa TAKUKURU akanusha madai haya
 
Tunachokijua
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo amethibitisha kumshikilia kwa mahojiano Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Tanzania (TPA) Deusdedit Kakoko. Pia Brigedia Mbungo amekanusha picha na video zinazosambaa mitandao zikionyesha fedha ikidaiwa zimekutwa nyumbani kwa Injinia Kakoko.

Brigedia Mbungo amesema; "Hapana huo ni uongo, taarifa za kukutwa na pesa nyumbani kwake siyo sahihi, ni watu nadhani ni maadui zake wanajaribu kutengeza hoja ya kuonyesha alikuwa na hizo fedha."

Aliongeza kuwa, "Kakoko anashikiriwa na sisi (TAKUKURU) hilo halina ubishi na tunamshikiria kwa sababu za kiuchunguzi kwahiyo tunaufanya uchunguzi lakini tunahitaji na yeye awepo, unajua kwa mfano unapokwenda kumpekua mtu ni zoezi la uchunguzi, sasa huwezi kumpekua wakati yeye hayupo lazima awepo".
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom