Sooth
JF-Expert Member
- Apr 27, 2009
- 3,922
- 5,626
Kesi si alishinda na yuko mtaani? Mimi natamani siku moja masuala ya maslahi na dhuluma dhidi ya Waislamu yajadiliwe kwa uwazi tena kupitia mifumo rasmi ya Serikali. Manung'uniko kila siku yanarudisha nyuma umoja wetu maana mara nyingi tunatuhumiana na tunaojibu tuhuma sio watu rasmi.Labda kesi inam keep busy?
Ilifika mahali ukiwa mkristo huwezi kukosoa waziwazi utawala wa JK. Likewise, leo ukiwa muislam ukakosoa utawala wa sasa utaonekana unakosoa sababu yuko dini tofauti. Binafsi naamin tuna maslahi mengi zaidi kuliko ya dini yanayotufanya tuwe na mtizamo tofauti. Kuna watu ni wapinzani kindakindaki, watahoji kila linalofanywa na CCM. Kuna wengine kwao ukanda/ukabila ndo kila kitu, atatetea kila kinachofanywa na kiongozi mkuu wa kabila lake. So let's not be too quick to judge.