Dereva wa UDOM akamatwa kwa madai ya kummwagia Kemikali Afisa Mtendaji

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
255
Screenshot_20230630-142003.jpg


Dereva wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Lusajo Makiwelu, anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwamwagia kemikali watu wawili akiwemo mtalaka wake, Witness Nguvalwa (31) na mtoto wake mwenye umri wa miezi sita (jina limehifadhiwa).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, alipozungumza na Mwananchi jana Juni 29, akisema lilitokea juzi wakati mwanamke huyo na mtoto wake wakiwa wanasubiri daladala eneo la Maghorofani jijini hapa.

Amesema wamemshikilia dereva huyo kama mshukiwa baada ya mtu asiyejulikana kummwagia mtalaka wake tindikali.

"Ni kweli taarifa hizo zipo tulipata taarifa hizo na tulifanya ufuatiliaji hiyo jana ( juzi) majira ya usiku na huyo mtuhumiwa tayari ametiwa mbaroni, kwa sasa tunaendelea na mahojiano," ameeleza Kamanda Martin Otieno.

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Witness ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Idedelomkazi wilayani Mufindi mkoani Iringa, amesema mkasa huo ulimkuta aliposhuka kituo cha Maghorofani akitokea Mafinga mkoani Iringa alipokuwa akisubiri usafiri wa kumpeleka atakofikia.

Amesema alikuja mkoani Dodoma kuleta wito wa Mahakama ya Mwanzo ya Mafinga kwa aliyekuwa mumewe ambaye walitenganishwa na mahakama hiyo.

"Safari yangu ilianza saa 3:00 asubuhi na Gari ya Shabiby nikitokea Mafinga lengo likiwa ni kuleta wito Mahakama ya Mwanzo ya Dodoma.

"Safari ilienda vizuri hadi nilipofika kituo cha mabasi Maghorofani niliposhuka kusubiri daladala au bajaji ili niende kukabidhi wito huo,” amesema.

Amesema akiwa katika kituo hicho, alipita mwanaume mmoja ambaye hakumfahamu akiwa ameshika kichupa mkononi kilichokuwa na kimiminika na mara baada ya kumsalimia alimwagia usoni.

“Alichofanya ni kunisalimia tu dada habari na kabla sijamjibu akanimwagia tindikali. Kwa muda nilibanwa na pumzi lakini nikajitahidi nikaomba msaada kwa watu waliokuwa pembeni na kituo hicho,” amesema.

Amesema madereva bajaji na bodaboda walimsaidia na kumfikisha kituo cha polisi, ambapo alipewa PF3 na kisha walimpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma ambako amelazwa.

Witness amesema alikuwa akimpelekea Makiwelu wito wa mahakama uliolenga kugawana mali walizochuma pamoja baada ya ndoa yao kuvunjwa na Mahakakama ya Mwanzo ya Mafinga mwaka juzi.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Baraka Mponda amesema walimpokea mama huyo na mtoto wake wa miezi 6 juzi jioni wakiwa wamejeruhiwa usoni kwa kumwagiwa kemikali.

Dk Mponda amesema majeruhi hao walifika wakiwa kwenye maumivu makali, mama akiwa ameathirika maeneo ya usoni, shingoni na begani na usoni kwa upande wa mtoto.

Amesema majeruhi hao wameendelea kupatiwa matibabu zaidi hospitali hapo.

Chanzo: Mwananchi
 
Watu msianze kuhukumu kwamba hicho kitendo amekifanya mumewe wa zamani,nani amejua kama huyo aliyemmwagia hiyo tindikali siyo bwana'ake nje ya ndoa iliyovunjika na amepata data akitoka kumdai mumewe alivyochuma nae atarudi na kwake kumtia umaskini?

Anaonekana alikuwa siyo haba kwa kubadilisha mabwana maana mwaka juzi tu karudi na mtoto wa miezi sita kufuata mafao alikoachika,haiyumkiniki huyo mwanamke ni malaya alishawahi kuwa na mabwana kadhaa hapo Dodoma so wakawa wanatafuta namna ya kumfikia wakapata data yupo ndiyo wakamfanyia hivyo?
 
Wanaume wa hovyo hao!! Una kazi Yako!! Mwanamke umezaa nae!! Mmezinguana !! Kwani mkiachana Salama Kuna nn!!
Ushamba mzigo
 
Afu eti unakuja mgawane mali
Kuna mmoja hapa naona alianza kumvuruga jamaa muda sana mara amtoroke anaenda kuliwa mikoani huko mara apigwe mtungo na wateja wake,yaan vurugu haziishi

Baadae jamaa ikabid aoe kidem kidogo akakipangisha jiran,basi mke wa jamaa akaanzisha kesi za ustawi wa jamii eti hapewi matumiz,ikaamuliwa jamaa amkabidhi duka,duka likafirisika,alivyokosa pa kushika akaenda mahakaman kuomba ndoa ivunje na kwel akafanikiwa,ikaamuliwa wagawane nyumba na viwanja na mali zingine

Jamaa kachanganyikiwa basi amekuwa ni mtu wa kumtafutia dawa anayamwaga humo ndani anapoishi huyo mwanamke,mwanamke nae anajiamin sana wala hata aogopi yupo tu ila ninavyowaona kuna mtu anaweza kufa kabisa
 
Umeachana na mumeo Tena inawezekana chanzo ni wewe.

Umepata bwana na umezaa nae. Maana mtoto ana miezi sita na ndoa ilivunjika mwaka juzi.

Bado unataka kumfilisi mtalaka wako eti mgawane mali.
Kuna matatizo yakujitakia.
Tamaa za Mali

Utakuta hapo alikuwa yuko na dume lingine,likamshawish I kwenda kudai Mali hayo ndiyo yamemkuta sasa

Ova
 
Kuna mmoja hapa naona alianza kumvuruga jamaa muda sana mara amtoroke anaenda kuliwa mikoani huko mara apigwe mtungo na wateja wake,yaan vurugu haziishi...

It really pains. Alafu inakuwaje unafanya project kubwa kubwa na hii jinsia!!.

Katika mahusiano wanawake ni smart sana ila hawana akili na wanaume intelligent sana but si smart. Ukiwa smart na intelligent utakuwa unasikia vilio tu kwa majirani.
 
Back
Top Bottom