Kwenye usafiri wowote kunaweza kutokea hatari au dharura yeyote..Nakumbuka nikiwa Kwenye safari fulani ya gari moshi ilitokea sintofahamu ndani ya mabehewa abiria wakawa wanataka kwenda kutoka nje huku treni iko kwenye mwendokasi lakini bahati nzuri treni ikasimama katikati ya pori na hiyo sintofahamu ikawa 'solved' na safari kuendelea.Sasa wadau nauliza dereva wa treni hupataje taarifa kama kuna hatari na yeye huwa mbali na mabehewa na anakuwa peke yake.