Dereva wa Basi la Mwendokasi adaiwa kuwapitiliza Vituo Abiria baada ya kukasirishwa

Dereva akawasha Gari kutoka Magomeni hakusimama hata kituo kimoja kwa hasira akaenda kuwashusha Abiria wote Kimara Mwisho hapo Kuna walemavu kibao, akashuka akapotea kusikojulikana, likatokea bonge la fujo pale, watu warudishwe walipotokea fujo kubwa sana, ikabidi Gari achukue Dereva mwingine awarudishe watu waliopitilizwa vituo
Hao madereva wangekuwa wanapimwa mkojo na akili kwasababu kuna siku walimbana mkono mama mmoja aliyekuwa anashuka huku anamkokota mwanayem na siku nyingine walimbana mzee mmoja Ubungo terminal, ila akili zao haziko sawa sijui wanapewaje hizo kazi
 
Screenshot from 2024-03-19 15-11-43.png

Mleta mada hebu tuambie huyu ameshuka kituo gani
Tuna uhakika atakuwa msaada kwenye uchunguzi wa hii kadhia
 
Sitosahau miaka miwili iliyopita nilitaka kupanda mwendo kasi maeneo ya stand ya zamani ya Ubungo. Nilitoa Tsh.5,000 yule dada kwa nyodo akanijibu hiyo pesa sipokei imechakaa.

Nilimuuliza wewe unaipekeka wapi zaidi ya benki? Akajibu nipe hela nyingine hiyo imechoka sana. Ikabidi nitoe Tsh.10,000 kwenye waleti nimpe. Cha ajabu akadai chenji inasumbua. Nikaona isiwe tabu huenda ana siku mbaya. Nikaenda dirisha lingine nikahudumiwa vizuri.

Wafanyakazi wa mwendokasi badilikeni.
 
Dereva katoka Gerezani akiwa na hasira gari limejaa milango hadi inataka kupasuka, Akasimama Faya watu wakawa wanamwambia kwa jinsi Gari ilivyojaa sana unatuumiza funga fungua fuata utaratibu sababu gari ni express kama ilivyoandikwa simama manzese kama ilivyo taratibu

Dereva akasimama na Magomeni kwa hasira, hapo gari imejaa vibaya sana na ni express, watu wakaanza kelele tena unatuumiza huku mlangoni na hakuna wakushuka na wala wakupakia, wakwamwabia wapo wakushuka manzese

Dereva akasimama anaanza kuzozana na abiria Kwa hasira

Dereva akawasha Gari kutoka Magomeni hakusimama hata kituo kimoja kwa hasira akaenda kuwashusha Abiria wote Kimara Mwisho hapo Kuna walemavu kibao, akashuka akapotea kusikojulikana, likatokea bonge la fujo pale, watu warudishwe walipotokea fujo kubwa sana, ikabidi Gari achukue Dereva mwingine awarudishe watu waliopitilizwa vituo

View attachment 2938988

Huu mradi unauliwa na wafanyKazi wenyewe ni shida
Si waliajiriwa Wanajeshi ili kuokoa pesa....

Haya ndo matokeo
 
Wampe Bahkresa uone
 
Back
Top Bottom