Dereva lori la mafuta ahukumiwa jela miaka minne na faini milioni 16

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Mahakama ya Mkazi Wilaya ya Iringa imemfunga jela miaka minne pamoja na kulipa fidia ya shilingi 16,050,000 dereva wa lori la mafuta la Kampuni ya Panone And Co. Ltd, Faid Mussa Manis baada ya kupatikana na hatia katika kesi jinai namba 2019 iliyokuwa ikimkabili yeye na wenzake 6.

Akisoma hukumu hiyo jana Machi 17, 202 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Iringa, Emmy Nsangalufu alisema kuwa Mahakama hiyo baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo pasipo shaka imejiridhisha na kuwatia kumtia hatiani dereva huyo na wenzake watano kwa kosa la wizi wa kuaminika.

Washtakiwa waliofikishwa Mahakamani hapo pamoja na Manis ni Abasi Seleman Finde maarufu kwa jina la Mchina , Frankl Manjir , Gerald John Mlelwa , Adam Kitururu Mzava ,Leonard Mwambela na Gaspa Juvenari Shirima.

Alisema kuwa washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa makosa matatu ambayo ni kula njama ambalo kosa lililohusisha washtakiwa wote saba, kosa la pili ambalo llilimhusu dereva pekee ni wizi wa kuaminika wakati kosa la tatu lililowahusu washtakiwa namba 2 na 7 ni wizi wa vitu vya kwenye gari zikiwemo lita 7200 za mafuta .

Hivyo, alisema kutokana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo mahakama hiyo imemtia hatiani kwa kumfunga jela miaka miwili dereva Manis kwa kosa la kwanza la kula njama na kosa la pili la wizi wa kuaminika inamhukumu kifungo cha miaka miwili na kufanya dereva huyo kutumikia jela miaka minne pamoja na kulipa fidia ya shilingi 16 ,050,000.

Mshtakiwa namba 2 namba 4 ,6 na 7 wakikutwa na hatia ya kosa la kuiba vitu vya kwenye gari hilo ambapo kila mmoja atafungwa jela miaka miwili pamoja na kulipa fidia ya shilingi 16 ,050,000 za mafuta yaliyopotea lita 7200.

Hata, hivyo alisema mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka yoyote na kuwaachia huru washtakiwa wawili kati ya saba ambao ni namba 3 na tano ambao ni Frankl Manjir na Adam Kitururu Mzava wakiachiwa huru .

Katika hukumu hiyo mahakama hiyo imewafunga washtakiwa wanne kati ya watano bila kuwepo mahakamani hapo baada ya mmoja kati yao kuruka dhamana hatua za awali kabisa na wengine kutofika kupokea uamuzi wa hukumu hiyo hivyo mahakama imeagiza wasakwe na wakipatikana wapelekwe gerezani.

Washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na wakili Rwezaura Kaijage ambaye aliomba mahakama hiyo kuwapunguzia adhabu wateja wake hao huku upande wa jamhuri ukiongozwa na wakili Alice Thomas na Jackline Nurga ambao waliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia ya kukosa uaminifu kwa mali za matajiri na serikali kwani vitendo vya wizi kama huo vimezidi kuongezeka nchini.


Source: Matukio Daima Blog
IMG-20220318-WA0027.jpg
 
Kwa system ya polisi hapa bongo jinsi ilivyo, kama hao watuhumiwa wapo smart kuwakamata ni ngumu sana
 
Alipaswa achapwe na viboko Kumi kila siku atakayokaa Jela.. Wizi sometimes ni aina Fulani ya Roho mbaya pia
 
Pale alternative inapogeuka kuwa shubiri.
Maisha ya Kitanzania kila mmoja hutafuta alternative way ku survive, ila ukibanwa ndipo unaonekana mbaya.
Hata hao police, mahakimu na huyo mmiliki wa mafuta wana alternative ways za ku survive tena za unyama zaidi ya huo wizi
 
Ila madereva wa bongo ni wezi na wanatia hasra mnoo.Yani ni shida.Huwa wanawatia hasara Waarabu na Wahindi wakijua hawatafuatilia kesi mahakamani.Mjifunze kuiba au kutengeneza matukio kwa akili nyingi.
 
Wazee wa kufaulisha

Wenzao zamani walikuwa wanafaulisha

Mafuta Alafu mbeleni wanaenda liangusha gari..

Sema Miaka ya sahv technolojia mambo ya gps imewaletea balaa

Ova
Ukishamimina mafuta yote pale nyororo Basi maeneo yakaribu na mbaramaziwa lazima gari idondoshwe na iungue kabisa
 
Back
Top Bottom