Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kumlawiti mke wake

Dexta

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
1,756
4,144
Mahakama ya Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Boniface Mtweve(28) mkazi wa kata ya Lugarawa kwa kosa la kumlawiti mke wake (27) ambaye jina lake limehifadhiwa.

Awali akisomewa shitaka hilo na mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Isaac Ayeng'o ilielezwa kuwa mwanamke huyo alienda kwenye harusi na kuchelewa kurudi nyumbani kwake ambapo aliporejea majira ya usiku alimkuta mumewe nje akimsubiri huku akiwa amekasirika.

Amesema kuwa mtuhumiwa huyo alimuamuru mkewe kuingia ndani na alipoingia akaanza kimfokea kuwa ametoka kwa wanaume na hakuwa kwenye harusi hivyo anataka amuoneshe kuwa yeye ni ndiye mwanaume ndani ya nyumba ambapo akachukua mafuta na kumfanyia kitendo hicho kitu ambacho ni kinyume cha sheria kifungu namba 154(1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Ameongeza kuwa kulipokucha mkewe alitoa taarifa kituo cha polisi na kisha mtuhumiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani ambapo alikana shitaka hilo lakini baada ya kufanyika uchunguzi na kutolewa ushahidi wa pande zote mbili mtuhumiwa alikutwa na hatia na katika utetezi wake aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwani ana watoto wadogo wanaomtegemea.

Kutokana na utetezi huo hakimu huyo aliyapokea maombolezo yake kisha kumhukumu kifungo hicho cha miaka 30 jela huku mwendesha mashtaka huyo Asifiwe Asajile akisema adhabu hiyo iwe fundisho kwa wale wote wenye tabia hizo kwani kitendo hicho ni cha kikatili na udhalilishaji.

Screenshot_20240112-171715_Facebook.jpg

#WasafiDigital
 
Jamaa kazingua,

Sijajua kama mke alitarajia adhabu hio
Kama alitarajia basi alikua anahitaji uhuru
Yeah inawezekana ndio miongoni mwa wale charge zikishafika mahakamani na shauri kufunguliwa na baada ya hukumu/Amri ya Mahakama wanaanza kulia wakiomba waume zao wasamehewe😄😄
Au vinginevyo ni kama ulivyosema alikuwa akihitaji uhuru. Kuna mibazazi kitaa itamfuata kuomba utelezi baada ya njia kutanuliwa tayari 🤣🙌
 
Awali akisomewa shitaka hilo na mwendesha mashtaka Asifiwe Asajile mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo Isaac Ayeng'o ilielezwa kuwa mwanamke huyo alienda kwenye harusi na kuchelewa kurudi nyumbani kwake ambapo aliporejea majira ya usiku alimkuta mumewe nje akimsubiri huku akiwa amekasirika.
Huko Iringa na Njombe ndio maana Ukimwi uko juu sana.

Watu huko wameweka Ngono kama kipaumbele kwao kama Nguzo muhimu kuliko hata Oxygen.

Yule kijana wiki iliyopita pia alifungwa Maisha Jela kwa kumuua Mkewe kisa wivu wa ngono.
 
Back
Top Bottom