mxyo16
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 1,243
- 760
hahahaha nimecheka aisee! hii mitoto nikuburuza tu mkuu. akirudi mwenyewe atasema asante. Hiyo shuguli ya magazine, imenikumbusha waliokua wanasababisha moto kwenye lile shamba la miti la taifa, dah tulikua tunakoma maafande sijui na gongo zao sigara wanawasha moto makusudi aisee at least mara moja kwa wiki mbili kwenda kuzima moto kwa majani saa saba za usiku mpaka 11.Duh, nilikuwa Makutupora...Duh, aisee pale palikuwa na shughuli nzito ya kuchimba mitaro ya mizabibu, na shamba lile la mtama mfupi sijui serena...sisahau shughuli ya kuchunga mbuzi....nakumbuka siku moja alikuwa anakuja kiongozi mkubwa, basi ikabidi tuwapige mswaki wale mbuzi...duh aisee, shughuli nzito, mbuzi anavyopiga kelele wakati wa kumpiga mswaki...Ila sitasahau tukio la mwenzetu mmoja alikuwa 'fala' yule tumekwenda 'field' zaidi ya kilomita 15 hivi sasa wakati wa kurudi tumekaribia kambi aaaah kumbe yule 'fala' amepoteza 'magazine' , mama yangu inabidi tuanze kurudi tena tulikotoka, aaah yaani tuna-comb kila kitu, watu wanalia wengine wanatambaa..duh, aisee...very 'interesting'..tukikutana sasa na ma-comrade over a bottle of beer, duh mazungumzo safi....That was a good training...I l loved it...miezi kadhaa iliyopita li-toto langu moja likawa linasitasita kwenda JKT kwa mujibu wa sheria, basi 'nika-liburuza' mpaka mlalakuwa na 'kuliandikisha'....
kama umepita lile eneo la mafinga kwenda mbeya baada ya iringa nadhani unajua lile sshamba la miti ile inawaka kama karatasi wakati ni mibichi....ni changa moto kwelikweli.