Demokrasia na uhuru wa vyama vya siasa una raha yake

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,666
8,582
Kusema ukweli demokrasia na uhuru wa vyama vya siasa kufanya kazi zake kwa uhuru kuna raha yake.

Mama Samia rais wetu, wewe tayari ni rais huna cha kupoteza, huhitaji teuzi wala ajira yeyote. Ajira uliyonayo ni ya juu kabisa, hakuna ajira zaidi ya urais hivyo huna cha kupoteza wala kuogopa. Nakuomba ufungulie uhuru kamili wa kila kitu.

Kwanza nakuomba wape watanzania katiba mpya. Unaweza kusubiri ukawapa mwezi mmoja kabla ya kuondoka ofisini kama unahisi utashindwa kuenjoy kikamilifu utamu wa hii katiba iliyopo. Kwa sasa unaweza kuendelea kufaidi utamu wa hii katiba iliyopo halafu mwenzi mmoja kabla ya kukiachia kitu cha urais unaachia katiba mpya pia, inaanza kutumika rasmi ili atakayekuja asitupande kichwani.

Cha pili, mama nakuomba uendelee kuwapa watanzania uhuru wa kujiachia nchini mwao ila tu wasivuke mipaka na kuvunja sheria. Nimeona mapokezi ya Mbowe kule Shinyanga nimefurahi sana, ingekuwa enzi zile hayo mapokezi yasingeruhusiwa, mama zetu wale wangepigwa na kudhalilishwa. Hongera sana mama kwa hili. Nimeona nyuso za akina mama zina bashasha, wakiimba kwa furaha na kwa uhuru, hongera sana mama kwa kurudisha tabasamu la mama zetu.

Cha tatu, nakuomba urudishe fao la kujitoa. Huo ni uhuru mwingine ambao wafanyakazi wanauhitaji. Kufutwa fao la kujitoa limeangamiza ndoto za vijana wengi wanaopenda kujiajiri na kuajiri watanzania wenzao. Mama nakuomba wape vijana uhuru wa kutumia hela yao. Sheria ya kuwapangia namna ya kutumia hela yao ni ya kiuonevu.

Cha mwisho, endeleza mazuri yote na uyakamilishe aliyoyaacha mtangulizi wako.


Cha mwisho kingine, hivi hakuna kauteuzi kidogo na mimi ukanipa?
 
Katiba mpya mama hawezi kuuitoa kama sadaka kwa kusukumwa na nafsi yake.

Mama amezungukwa na wenye uchu wa madaraka ambao muda wote wanaangalia kalenda ili kujua lini mama anatoka wao waingie wafaidike na katiba mbovu iliyopo.

Hawataruhusu mama aibadilishe ili hao wenye uchu waje waukose ulaji.

Katiba hudaiwa kwa nguvu, haiombwi.
 
Katiba mpya mama hawezi kuuitoa kama sadaka kwa kusukumwa na nafsi yake.

Mama amezungukwa na wenye uchu wa madaraka ambao muda wote wanaangalia kapenda ili kujua lini mama anatoka wao waingie wafaidike na katiba mbovu iliyopo.

Hawataruhusu mama aibadilishe ili hao wenye uchu waje waukose ulaji.

Katiba hudaiwa kwa nguvu, haiombwi.
Nimeshauri aitoe akiwa anatoka madarakani. Hana cha kupoteza.
 
Tundu lissu sijui nimemkosea nini kule Twitter kanichapa tofali Tundu nisamehe.
 
Nimeshauri aitoe akiwa anatoka madarakani. Hana cha kupoteza.
Tatizo ni anaowaacha, wao Wana cha kupoteza. Na kwa kuwa usalama na shughuli zote za mama zinategemea watu, na watu ni wao, itakuwa ngumu sana kama wao hawajaafiki.
 
CCM wanajua100% kuwa hawakubaliki...kwa hiyo kinga yao kuu ni Katiba iliyopo..ukitaja katiba mpya ni sawa na kuwaminya sehemu za siri.
 
Back
Top Bottom