Degree with Honours

Degree with Honours

Konzogwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2008
Posts
434
Reaction score
164
Salam wana jamvi! Dogo angu kapata LOWER SECOND WITH HONOURS. Hivi nini maana yake na inafaida gani katika life applications
 
Sasa si ungemuuliza, ila mpe pongezi maana hajawahi kupata supplimentary na hiyo ndio maana ya honour.
 
si kweli kuwa hajawahi pata sup, wapo waliopata na wana honours, pia wapo waliopata gpa inayopaa still wanayo honours , so wajuvi wa mambo watakuja dadavua zaidi
 
Najua wataka usikie ni UDOM maana swali lako nimelishtukia. Jaribu kucomment kwa perspective ya kisomi kwa sababu elimu ya University ni Universal, so nadhani swali la ni chuo kipi unataka kuleta redundant points.
SAUT hawanaga honours!
 
Salam wana jamvi! Dogo angu kapata LOWER SECOND WITH HONOURS. Hivi nini maana yake na inafaida gani katika life applications

Jibu la haraka haraka.
Hii ina maana katika kuhitimu mafunzo (shahada) yake ameshika nafasi ya tatu.

Shahada zipo kwenye viwango hivi na nitavifafanua baadae:

  1. 1st class honors au (Summa cum laude): Nafasi ya juu kabisa (ya kwanza)
  2. Upper 2nd class honors au (Magna cum laude): Nafasi ya pili
  3. Lower 2nd class honors au (Cum laude): Nafasi ya tatu
  4. Pass (au Thank-you Oh Lord degree a.k.a. “gentleman degree”)
  5. Fail (umefeli au kushika mkia)
​
LOWER SECOND WITH HONORS inamaana gani?
Inamaanisha kuwa katika masomo ya kozi yake amejitahidi na kupata GPA (Grade Point Average) ya wastani wa B+ kwa masomo yote. Hii GPA sio kiashiria cha mafanikio yake kwenye maisha au kazini. Kwa mwajiri hii ina maana huyu kijana akimpa jukumu unaweza kutegemea ufanisi mzuri zaidi ya wastani (better than average performance). Aina ya shahada iliyopo kwenye cheti chako itakusaidia tu kufungua milango katika kutafuta ajira.

Inawezakana kabisa mwanafunzi mwenye pass (B) degree akawa na ufanisi wa A+ kazini na 1st class honor (A+) degree holder akawa na ufanisi duni kazini.

Hii GPA inakokotolewaje?
Nitakupa mfano hai ninaoufahamu mimi kwa hapa nilipo. (Utaratibu huu unaweza kutofautiana na sehemu nyingine).

Kuanzia mwaka wa kwanza mpaka mwanafunzi anamaliza shahada yake kila somo akilimaliza atapewa alama ya A, B, C, D, F kufuatia na ufaulu wake. Kila alama ina uzito wake (huu uzito unatofautiana kutoka shule hadi shule) kama ifuatavyo:

A+ = 5.0
A =4.5
A- =4.0
B+ =3.5
B =3.0
B- =2.5
C+ =2.0
C =1.5
C- =1.0
D+ =0.5
F =0

Zaidi ya kila alama kuwa na uzito wake, pia kila somo linapewa uzito kulingana na ugumu au umuhimu wake katika hiyo shahada.
Kwa mfano: Kama unafanya shahada ya uchumi (Economics), basi somo linalochambua sera za kiuchumi (MONETARY/FISICAL policies) litakuwa na uzito mkubwa kuliko somo la mwaka wa kwanza kama Introduction to Microeconomics. Uzito wa somo pamoja na uzito wa alama aliyopata mwanafunzi ndivyo vinavyotumika kukokotoa (weighted average) GPA. (Kama utataka mfano wa kukokotoa weighted average nitonye nitakuwekea)

Hivi ndio viwango vya shahada kufuatia GPA yake atakapomaliza shahada yake:

4.00-5.00 - 1st class honors au (Summa cum laude): Nafasi ya juu kabisa (ya kwanza) [A-, A, A+]
3.80-3.99 - Upper 2nd class honors au (Magna cum laude): Nafasi ya pili [upper B+]
3.5-3.79 - Lower 2nd class honors au (Cum laude): Nafasi ya tatu [lower B+]
2.5-3.49 - Pass (Thank-you Oh Lord degree a.k.a. “gentleman degree”)
< 2.5 - Fail
 
maana yake ni kuwa toka aanze mwaka wa kwanza hajawahi kushuka Gpa ya inamaanisha kila semister ilikua inapanda Gpa yake

Hata mimi ninajua hivyo Honourable degree inatolewa kwa mtu ambae GPA yake imekuwa ikipanda kila mwaka, hata kama aliwahi kusup anapewa. Sasa sijui kwa vyuo vingine wanafanyaje.
 
Sasa si ungemuuliza, ila mpe pongezi maana hajawahi kupata supplimentary na hiyo ndio maana ya honour.

Acha uongo maana honour sio sup na wala haina uhusiano na sup unaweza ukawa na sup na ukapata honour na unaweza ukakosa sup na ukawa 1st class ila usiwe na honours vilevile honour ni gpa inayo panda hata ikiwa lower.
 
Najua wataka usikie ni UDOM maana swali lako nimelishtukia. Jaribu kucomment kwa perspective ya kisomi kwa sababu elimu ya University ni Universal, so nadhani swali la ni chuo kipi unataka kuleta redundant points.
mbona hujiamini wewe kijana wa kizazi cha mulugo,nani kakwambia mimi nataka UDOM,au umepelekwa huko UDOM afu unajuta sana,naomba nijibu swali langu kasoma chuo gani ndo tuendelee na mambo mengine,kama hutaki basi usiwe unaleta posts zako za kidwanzi humu JF.
 
Jibu la haraka haraka.
Hii ina maana katika kuhitimu mafunzo (shahada) yake ameshika nafasi ya tatu.

Shahada zipo kwenye viwango hivi na nitavifafanua baadae:

  1. 1st class honors au (Summa cum laude): Nafasi ya juu kabisa (ya kwanza)
  2. Upper 2nd class honors au (Magna cum laude): Nafasi ya pili
  3. Lower 2nd class honors au (Cum laude): Nafasi ya tatu
  4. Pass (au Thank-you Oh Lord degree a.k.a. "gentleman degree")
  5. Fail (umefeli au kushika mkia)
&#8203;
LOWER SECOND WITH HONORS inamaana gani?
Inamaanisha kuwa katika masomo ya kozi yake amejitahidi na kupata GPA (Grade Point Average) ya wastani wa B+ kwa masomo yote. Hii GPA sio kiashiria cha mafanikio yake kwenye maisha au kazini. Kwa mwajiri hii ina maana huyu kijana akimpa jukumu unaweza kutegemea ufanisi mzuri zaidi ya wastani (better than average performance). Aina ya shahada iliyopo kwenye cheti chako itakusaidia tu kufungua milango katika kutafuta ajira.

Inawezakana kabisa mwanafunzi mwenye pass (B) degree akawa na ufanisi wa A+ kazini na 1st class honor (A+) degree holder akawa na ufanisi duni kazini.

Hii GPA inakokotolewaje?
Nitakupa mfano hai ninaoufahamu mimi kwa hapa nilipo. (Utaratibu huu unaweza kutofautiana na sehemu nyingine).

Kuanzia mwaka wa kwanza mpaka mwanafunzi anamaliza shahada yake kila somo akilimaliza atapewa alama ya A, B, C, D, F kufuatia na ufaulu wake. Kila alama ina uzito wake (huu uzito unatofautiana kutoka shule hadi shule) kama ifuatavyo:

A+ = 5.0
A =4.5
A- =4.0
B+ =3.5
B =3.0
B- =2.5
C+ =2.0
C =1.5
C- =1.0
D+ =0.5
F =0

Zaidi ya kila alama kuwa na uzito wake, pia kila somo linapewa uzito kulingana na ugumu au umuhimu wake katika hiyo shahada.
Kwa mfano: Kama unafanya shahada ya uchumi (Economics), basi somo linalochambua sera za kiuchumi (MONETARY/FISICAL policies) litakuwa na uzito mkubwa kuliko somo la mwaka wa kwanza kama Introduction to Microeconomics. Uzito wa somo pamoja na uzito wa alama aliyopata mwanafunzi ndivyo vinavyotumika kukokotoa (weighted average) GPA. (Kama utataka mfano wa kukokotoa weighted average nitonye nitakuwekea)

Hivi ndio viwango vya shahada kufuatia GPA yake atakapomaliza shahada yake:

4.00-5.00 - 1st class honors au (Summa cum laude): Nafasi ya juu kabisa (ya kwanza) [A-, A, A+]
3.80-3.99 - Upper 2nd class honors au (Magna cum laude): Nafasi ya pili [upper B+]
3.5-3.79 - Lower 2nd class honors au (Cum laude): Nafasi ya tatu [lower B+]
2.5-3.49 - Pass (Thank-you Oh Lord degree a.k.a. "gentleman degree")
< 2.5 - Fail

JF ni hazina,
tatizo tu haina uhusiano na pay master general!
 
kwa hapa bongo anayepewa honour ni yule aliyemaintain au gpa ya kupanda bila kudrop.
 
upper B+ and lower B+: how are they different????????????
 
Najua wataka usikie ni UDOM maana swali lako nimelishtukia. Jaribu kucomment kwa perspective ya kisomi kwa sababu elimu ya University ni Universal, so nadhani swali la ni chuo kipi unataka kuleta redundant points.

Kila chuo kina quality yake (jinsi ya kutoa hizo degee/diploma) we taja hicho chuo kama huoni shida.
 
mbona hujiamini wewe kijana wa kizazi cha mulugo,nani kakwambia mimi nataka UDOM,au umepelekwa huko UDOM afu unajuta sana,naomba nijibu swali langu kasoma chuo gani ndo tuendelee na mambo mengine,kama hutaki basi usiwe unaleta posts zako za kidwanzi humu JF.

Asiwe analeta posti ambazo hajiamini nazo.
 
Back
Top Bottom