tycoonff
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 928
- 1,310
In GPA assessment, B+ ranges between 3.5 and 3.99. Thus:
Lower B+ is between 3.50 and 3.79
Upper B+ is between 3.80 and 3.99
Mzumbe Upper second ranges between 3.5 and 4.3
In GPA assessment, B+ ranges between 3.5 and 3.99. Thus:
Lower B+ is between 3.50 and 3.79
Upper B+ is between 3.80 and 3.99
kwa hapa bongo anayepewa honour ni yule aliyemaintain au gpa ya kupanda bila kudrop.
Mzumbe Upper second ranges between 3.5 and 4.3
Salam wana jamvi! Dogo angu kapata LOWER SECOND WITH HONOURS. Hivi nini maana yake na inafaida gani katika life applications
mbona hujiamini wewe kijana wa kizazi cha mulugo,nani kakwambia mimi nataka UDOM,au umepelekwa huko UDOM afu unajuta sana,naomba nijibu swali langu kasoma chuo gani ndo tuendelee na mambo mengine,kama hutaki basi usiwe unaleta posts zako za kidwanzi humu JF.
PercentageJibu la haraka haraka.
Hii ina maana katika kuhitimu mafunzo (shahada) yake ameshika nafasi ya tatu.
Shahada zipo kwenye viwango hivi na nitavifafanua baadae:
​
- 1st class honors au (Summa cum laude): Nafasi ya juu kabisa (ya kwanza)
- Upper 2nd class honors au (Magna cum laude): Nafasi ya pili
- Lower 2nd class honors au (Cum laude): Nafasi ya tatu
- Pass (au Thank-you Oh Lord degree a.k.a. gentleman degree)
- Fail (umefeli au kushika mkia)
LOWER SECOND WITH HONORS inamaana gani?
Inamaanisha kuwa katika masomo ya kozi yake amejitahidi na kupata GPA (Grade Point Average) ya wastani wa B+ kwa masomo yote. Hii GPA sio kiashiria cha mafanikio yake kwenye maisha au kazini. Kwa mwajiri hii ina maana huyu kijana akimpa jukumu unaweza kutegemea ufanisi mzuri zaidi ya wastani (better than average performance). Aina ya shahada iliyopo kwenye cheti chako itakusaidia tu kufungua milango katika kutafuta ajira.
Inawezakana kabisa mwanafunzi mwenye pass (B) degree akawa na ufanisi wa A+ kazini na 1st class honor (A+) degree holder akawa na ufanisi duni kazini.
Hii GPA inakokotolewaje?
Nitakupa mfano hai ninaoufahamu mimi kwa hapa nilipo. (Utaratibu huu unaweza kutofautiana na sehemu nyingine).
Kuanzia mwaka wa kwanza mpaka mwanafunzi anamaliza shahada yake kila somo akilimaliza atapewa alama ya A, B, C, D, F kufuatia na ufaulu wake. Kila alama ina uzito wake (huu uzito unatofautiana kutoka shule hadi shule) kama ifuatavyo:
A+ = 5.0
A =4.5
A- =4.0
B+ =3.5
B =3.0
B- =2.5
C+ =2.0
C =1.5
C- =1.0
D+ =0.5
F =0
Zaidi ya kila alama kuwa na uzito wake, pia kila somo linapewa uzito kulingana na ugumu au umuhimu wake katika hiyo shahada.
Kwa mfano: Kama unafanya shahada ya uchumi (Economics), basi somo linalochambua sera za kiuchumi (MONETARY/FISICAL policies) litakuwa na uzito mkubwa kuliko somo la mwaka wa kwanza kama Introduction to Microeconomics. Uzito wa somo pamoja na uzito wa alama aliyopata mwanafunzi ndivyo vinavyotumika kukokotoa (weighted average) GPA. (Kama utataka mfano wa kukokotoa weighted average nitonye nitakuwekea)
Hivi ndio viwango vya shahada kufuatia GPA yake atakapomaliza shahada yake:
4.00-5.00 - 1st class honors au (Summa cum laude): Nafasi ya juu kabisa (ya kwanza) [A-, A, A+]
3.80-3.99 - Upper 2nd class honors au (Magna cum laude): Nafasi ya pili [upper B+]
3.5-3.79 - Lower 2nd class honors au (Cum laude): Nafasi ya tatu [lower B+]
2.5-3.49 - Pass (Thank-you Oh Lord degree a.k.a. gentleman degree)
< 2.5 - Fail
ukikua utaacha kjana wewe wa kizazi cha mulugo,unaparamia paramia tu comments za watu,kaa pembeni dogokwani ukijua chuo kitakusaidia nini, hizi grade si ni standard Au GPA ya chuo chako ulicho soma ndo ya maana sana. ucha ulimbukeni kijana.
Wa bogo bwana mnashabikia vitu ambavyo sio vya msingi kabisa. halafu weweunae uliza chuo gani unaonyesha jinsi gani usivyo jua mambo, umeulizwa swali kama unajua jibu hujui acha watu wengine wajibu au unataka tukuone upo japo kuwa huna mchango wala msaada
hizi ndio nazifahamu mimi hata mzumbe wanatumia hizo,na witj honours kutokana na condition za haoopo juuExtract ya UDSM angalia kuna tofauti ya nani anapata honours degrees between thegeneral regulations na zile za College ya Sheria.
"UNDERGRADUATE PROSPECTUS 2013/2014
GENERAL UNIVERSITY UNDERGRADUATE EXAMINATION REGULATIONS pg14
12.6 The Grade Point Average (GPA) for the degree shall be computed by dividing the total score in 12.5 by the total weight obtained under 12.3 and truncating down to one decimal point.
12.7 The final classification shall be as follows:
First Class A (5.0-4.4)
Upper Second Class B+ (4.3-3.5)
Lower Second Class B (3.4-2.7)
Pass C (2.6-2.0)
12.8 Award of Honours Degree:
A degree with honours shall be awarded to a candidate obtaining a First or Second class upper division where the candidate has passed all examinations at first sitting; without supplementary examination or carry over in any particular academic year.
School of Law UDSM pg 209
16.2 The Board of Examiners shall recommend the award of a degree with honours to a candidate obtaining a 1[SUP]st[/SUP] Class, 2nd Class Upper Division or 2nd Class Lower Division where he has passed all his examinations at first sitting, meaning, without supplementary or carry over in any particular academic year."
Law Enforcement programme has an identical regulation 22.2 pg212
Sitashangaa kama kuna variation between chuo na chuo.
kasoma chuo gani????? ili tudondoshe comments kutokana na status ya chuo alichosoma
first year nina 3.8 na second year 3,8 and third year 4,0 lakini sijapata hons panakuaje hapo au siqualify
In GPA assessment, B+ ranges between 3.5 and 3.99. Thus:
Lower B+ is between 3.50 and 3.79
Upper B+ is between 3.80 and 3.99
Percentage
range
70%
–
100%
60%
-
69.9%
50%
–
59.9%
40%
-
49.9%
35%
–
39.9%
0-
34.9%
Letter
grade
A B+ B C D E
Points 5 4 3 2 1 0
PASS FAIL
Degree 58. The degree classification
Classification
GPA Range Degree Classification
4.4 – 5.0 First class
3.5 - 4.3 Second Class- Upper Division
2.7 - 3.4 Second Class – Lower Division
2.0 -2.6 Pass
hapa chuoni ninaposoma first class inaanzia 4.4
na ukikamatwa masomo zaidi ya matatu kwa tunaosoma ma 5 una disco. inamaana GPA zinatofautiana kila chuo
Hata mimi ninajua hivyo Honourable degree inatolewa kwa mtu ambae GPA yake imekuwa ikipanda kila mwaka, hata kama aliwahi kusup anapewa. Sasa sijui kwa vyuo vingine wanafanyaje.
tuwe tunajitahidi kucomment atleast kama mkuu alivo comment bila kuleta matatizo.nimekupata mkuiuunakubaliana na wewe. Hii ndio criteria tuliokuwa tunaitumia nilipokuwa udsm, i.e., 100-70 = a, and so on... Ambayo kwa maoni yangu naiona ni subjective.
Nilipo sasa tunautaratibu mwengine ambao ninadhani ni more objective.
Tuna-grade along the course curve (not class curve).
Tuwe tuna comment kama mkuu hapo juuu alivofanya na katoa analysis nzuri
rationale: tunaamini kwamba over the years wanafunzi wanaopitia hilo darasa wana-represent the population, na an average grade ni b. Kwa mfano kwenye somo langu course average kwa sasa ni 79%. Kwa hiyo wanafunzi wakifanya mtihani wa somo hili atakaepata 79% ni b. Grade za juu au chini zinarekebishwa kwa kutumia multiples of standard deviation. Nasisitiza kuwa tunatumia course average na sio class average. Hii course average is a moving average ambayo inarekebishwa kadiri miaka inavyoendelea.
objectivity: hii ina maana kama mwalimu ana tabia ya "kuwakamata" wanafunzi kwa mitihani ya kuviziana halafu course average ya darasa lake ikashuka hadi 45%, basi b-grade itakuwa 45%. Hii itakuwa ni njia mojawapo ya huyo mwalimu kujiuliza kuwa kulikoni. Kama katika kipindi cha miaka kadhaa (say 10) wanafunzi wanapata alama za chini kiasi hicho tatizo liko wapi. Pia kama hii class average itakuwa juu sana (85-90%) basi mwalimu anapaswa kujiuliza kama mitihani yake ni kigezo kizuri cha kutofautisha kati ya vilaza na vichwa.
gpa na degree classification
utaona hapa kuwa itakuwa vigumu kulinganisha kiwango cha shahada (kwa mfano second-class, upper division) kati ya vyuo viwili vinavyotumia taratibu tofauti katika utoaji wao wa grades.
kwani ukijua chuo kitakusaidia nini, hizi grade si ni standard Au GPA ya chuo chako ulicho soma ndo ya maana sana. ucha ulimbukeni kijana.
Wa bogo bwana mnashabikia vitu ambavyo sio vya msingi kabisa. halafu weweunae uliza chuo gani unaonyesha jinsi gani usivyo jua mambo, umeulizwa swali kama unajua jibu hujui acha watu wengine wajibu au unataka tukuone upo japo kuwa huna mchango wala msaada